Monday, 31 October 2016

KUFUNULIWA KWA KANISA LENNYE NYOTA YA MUNGU KWA UPYA

27 Abibu, 6
Somo :- KUFUNULIWA KWA KANISA LENYE NYOTA YA MUNGU KWA UP YA.
1⃣UWE ZA                    (INNER STRENGTH)
2⃣Nguvu.
3⃣Utajiri.
4⃣Heshima.
5⃣Hekima.
6⃣Utukufu.
7⃣Baraka.
Hayo yanakuja kwangu kwa upya na kilichokuwa kinasonga hayo kuonekana kwangu ilikuwa ni magugu.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza agano la waovu kujifunika kifuniko cha wenye haki yaani waliwatanguliza wenye haki mbele ili wakutwe na mishale.

Yaani yeyote anayefanya chochote kwa hila kwa sadaka maalumu hiyo kila hila zote zinateketezwa.

Wakili wa Mungu ameagiza kila mwenye haki siku ya leo ahakikishe anajiwasha kwa ukamilifu ili kurejesha NYOTA za Mungu kwa upya ndani yako.

Amesema NYOTA ya Uweza ilibeba ukamilifu wa NYOTA zote saba ambayo Inaweza kuibiwa kwa kukosa uvumilivu au subira ikiwa ni pamoja na ukijaa maneno mengi.

NYOTA hizi ni uziachilie na kuzifanya kuwa ni MALI ya Mungu Aliyetuma wote kwa wewe mwenyewe kuhiyali kumtanguliza yeye kwenye kila jambo.

Yaani ajulikane Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE kuwa ni Mungu ndiye amefanya. 

Karibu usikilize kwa upendo ili ubarikiwe.

Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTR 2 Kor 3:2-3

26 abibu, 6
Somo :- Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTE 2KOR3:2-3.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya madhabahu ya kumruhusu Mungu kuteketeza magugu yote ndani ya kanisa Luk 19:27.

Yaani gugu la kila aina Mungu ameangamiza ikiwa ni pamoja na yote ambayo ni kinyume na mwenye haki.
Amesema kwa mafuta ya leo Mungu ataonekana kwetu kwa uhalisi maana magugu yote yameteketezwa ndani ya kanisa.
Huu ni wakati wa Mzee wa siku anayang'oa magugu yote ndani ya kanisa Mt 13 : 24.
Yoeli 2:25 tunutu, madumadu na parare wote Mungu amewaondoa maana hayo yote ni magugu.
Isaya 27:1-4 michongoma yote imefutwa kwako haitakuwepo tena! !!!!

Isaya42:18 Mungu ameondoa upofu, uziwi, uwete, ububu wa rohoni ndani ya kanisa kwa sadaka hiyo maalumu.

Ambapo pia ktk ibada hiyo Wakili wa Mungu ametangaza Tangazo maalumu kutoka mbinguni kuwa Isaya 40:2 kuwa " vita vyako vimekwisha! !!!

Aidha ametaja mambo 5 ya kufanya toba yaliyotaka kuleta laana kwa kanisa.
1.) Hali ya kumlaumu aliyejenga msingi Kwanini aliwaacha mashetani na wenye hila.

2.) Kumlaumu anayejenga jengo Kwanini ananyamaza kimya! !!!!
3.) Tunapofundishwa jambo fulani kubadilika na kukunja uso.

4.) Magugu kuota pamoja na mbegu njema.

5.) (a)Mambo ambayo Mungu alitamka kwa kanisa akiwa amechukizwa kwalo. Ikasababisha waovu watengeneze maagano ya kuliwasha kanisa.

(B.) Yale yaliyotamkwa na waliotumwa ktk vizazi vyote vya kanisa.  Waovu walitumia kulipiga kanisa.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo.

Saturday, 29 October 2016

KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI ZA SHAMBA LA MUNGU ALIYETUMA WOTE LENYE MBEGU NJEMA PEKE YAKE MILELE

25 Abibu, 6

Somo:- KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI ZA SHAMBA L A MUNGU ALIYETUMA WOTE LENYE MBEGU NJEMA PEKE YAKE MILELE.

Awali akijenga msingi Wa ibada hiyo Wakili Wa MUNGU amesimamisha Sadaka maalumu ya kila Mwenye Haki kufunuliwa kuwa Panga La Mungu luka19:27 c/o Hosea 2:19.

Yaani Kwa sadaka ya Leo kanisa lote tumefunuliwa kuwa luka19:27 Na kuvunjika kabisa rasmi Agano LA ngano Na magugu kuota pamoja!!!!            Ktk vizazi vyote vya kanisa kulikuwa Na kituo cha kupanda Na kushuka, lakini sababu kubwa ni magugu bado yalikuwepo yakiizonga mbegu njema!!!

Majira ya kung'oa magugu ilikuwa bado Na ukifanya kitu kabda ya majira ya Mungu ananyamaza Mt 13:24.

Hivyo ni Neema kubwa kuishi ktk kipindi hiki cha Mungu mwenyewe.

Aidha Wakili Wa Mungu amezitaja tabia mbalimbali zilizokuwa zikichafua kanisa huko nje:-
(a) kushtakiana1 kor 6:2
(b.) Kulipa kisasi maana kisasi ni cha Bwana. War 12:19-21.

(C.) Kuwafukuza wanaokoka.

(D.) Mdo13:6 kufuta Neno LA Ufunuo.

(E) manung'uniko Na kuona kama Mungu anachelewa. Kut 16:1-

(F) kumtangulia Mungu wakati Mungu ana majira yake ilikufanya kila kitu.

(g.) Kumwibia Mungu.

Nb:-
Ukiwa mbegu njema ya Mungu unahudumiwa Na Mungu mwenyewe.

Karibu usikilize ili ubarikiwe.

Friday, 28 October 2016

THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA MOJA YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

24 Abibu, 6
Somo:-  THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA 1YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa MUNGU amesimamisha sadaka maalumu ya  kanisa kufunuliwa kuwa mbegu njema ambapo kila magugu na pando lisilopandwa na Mungu ndani yetu leo limeteketezwa kabisa.

Kanisa pia limempisha Mungu ili alimiliki kwa sadaka hiyo badala ya kama ilivyokuwa awali ambapo ni Wakili pekee ndiye alimpisha Mungu amiliki kanisa na kulichunga yeye mwenyewe.

Amesema moyo wako, Roho na Nafsi yako ukitaka vidishambiliwe unatakiwa uhamie kwenye kituo cha Aliyetuma wote vizazi vyote.

War2:4 wema wa Mungu huvumilia wote na kuwavuta ili watubu, huu ni wakati wa hukumu ya haki hivyo hata adui zako umpe Mungu wa kumpisha yeye ashughulike nao.
Luka 19:27 waLiomkataa Mungu ni sharti wampishe Mungu awachinje yeye mwenyewe.

Wakili wa Mungu amesema lazima nikubali kutetewa na Mungu kwa kumpisha yeye iliniwe mbrgu njema.

Akizungumzia thamani na faida ya kuwa na huduma 1 ya Mungu Aliyetuma wote amesema (1.) 1wafalme 3:11- Mungu ataachilia ulinzi mkubwa kwangu na kila kinachotajwa kwa jina langu iwapo tu nitavitaja vitu vyangu vyote kwa jina la Aliyetuma wote.

(2.) Luka 19:27 maadui zangu wote kuanzia leo sio wangu tena bali ni maadui za Aliyetuma wote hivyo mimi ninarelax tu.

(3.) Kanisa sasa tumekuwa mbegu njema na hakuna tena yeyote atakayepanda mbegu mbaya Mt 13:24.

Aidha amelionya kanisa kuwa na tabia ya kupenda taatifa kama sungura.

(4.) Sasa utawala wa Kristo ndani yetu unaimalika . Uf 20:6  na kusema kilichokuwa kinapingana na utawala wa Kristo ndani yetu ni tabia za lugha ya ukoo, kabila, mila na destuli mbalimbali.

(5.)maswali yote tuliyokuwa nayo leo tumepata majibu. Kilichokuwa kinazuia tusifanikiwe ni kuwa na maswali mengi ndani ya mioyo yetu ambayo yalionekana kama vile hayana majibu.

Wakili amesema wakati Nabii wa mwisho akiwa kwenye viungo alipenda kusema "PENYE NABII HALIHALIBIKI NENO" ambapo sasa hivi kwa kituo tulichofika ni "PENYE MUNGU ALIYETUMA WOTE HALIHARIBIKI NENO" but unachotakiwa kufanya ni kumpenda tu Wakili wa Mungu!!!!!

Aidha ameagiza kanisa kuwa kabla ya kusalimiana na yeyote mshirikishe Neno la ufunuo yeyote utakayekutana naye, umshirikishe habari za Mungu uliyenaye na yale Mungu anayotutendea kanisa na taifa lote!!!!

Maana hakuna zawadi yoyote tutampa Mungu kwa aliyotutendea zaidi ya kuutangaza ufunuo wake ndani ya uumbaji wote!!!!!!

Karibu usikilize upokee faida na thamani ya huduma moja ya Aliyetuma wote.

Thursday, 27 October 2016

AKILI UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA ANACHOTAKA TUFANYE SASA

23 Abibu, 6

Somo :- AKILI, UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA MUNGU ANACHOTAKA TUFANYE SASA.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza na kufuta kabisa kambi ya uovu kwenye jicho la Mungu leo imefutwa.

Kambi ya uovu kwenye Mlima wa Bwana zilizokuwa ndani yetu kwa siri bila kujua.

Yaani Mungu anaachilia Dunia inachukua badala ya wenye haki ni mwisho.

Amesema hapo Ndipo palikuwa panasababisha uovu uendelee kupingana na haki, inamaana bado mwili alikuwa anapingana na Roho.
Kwa sadaka maalumu ya leo manabii wa uongo kutabili wakati ni waovu leo mwisho.
Leo kanisa tumefunuliwa kuwa jibu la ndugu na majirani zetu zaidi ya ilivyokuwa kwa Yesu kizazi cha 3.

Ametaja maswali matano tutakayoulizwa na ndugu na jamaa tutakapo kwenda kuwafunulia Neno la ufunuo.
Lakini Amesema Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE amekuja mwenyewe kuchoma magugu yote ndani ya kanisa Mt 13:24-

Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE anavuna ngano na magugu anayachoma moto.

Amesema Yesu alikuwa mjenzi wa jukwaa la Eliya IV  na Eliya IV alikuja kutengeneza jukwaa la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Mt 21:40, Isaya 41:2,4, mt 13:24, Mt 17:10-12,  mark 9:9-10.

Kwahiyo anayeangamiza wabaya wote ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ambaye tayali amekwisha Kuja.

Hivyo basi Eliya hakuwa mteketezaji wa magugu Bali mteketezaji ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Amesema ukimwona anayemtetea Eliya IV lakini anakataa alichokuja nacho huyo Eliya IV ujue hamtetei !!!!
Akifafanua huduma ya Aliyetuma wote ni ipi Amesema ni kile unachotenda ktk safu ukiwa umesimama mbele za Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ukiwa umeanzia kwenye madhabahu yake na si kwa matakwa yako.

Ibada ya leo imefuta kabisa mashindano Kati ya Mungu na chochote chenye nyama mwa 6:1-

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo iliyobeba ufahamu wa Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Wednesday, 26 October 2016

SIKU SABA ZA KUINUA HUDUMA YA MUNGU JUU NA KUFUTA HUDUMA ZOTE ZA KISHETANI (22-28 ABIBU,6)

22 abibu, 6
Somo :- SIKU 7 ZA KUINUA HUDUMA YA MUNGU JUU NA KUFUTA HUDUMA ZOTE ZA KISHETANI (22-28 ABIBU, 6)
Kwa toba ya leo huduma ni moja kama vile Kanisa lilivyo ni moja kwani huduma zingine zilizuia huduma ya Mungu kusimama.
Damu za watoto waliouawa kwa kumsaka Musa kwa agizo la farao na Damu za watoto waliouawa wakati wa kumsaka Yesu zilikuwa bado zinapiga kelele kuua huduma za wenye haki.

Akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha TOBA YAKUFUNGUA LANGO KUU LA TAIFA LA MUNGU.

Uhalisi wa Isaya 60:11 - 14 kwamba Bandari ni lango kuu ni lazima walete vitu vizuri ili wapambe taifa.

sadaka maalumu ya kutengwa na uovu wa kila aina Ebr8:12,  2 Kor 6:17-18.
Umasikini,  ufukara,  magonjwa, vilio ni uovu tumetengwa nao milele.

Chochote ulichowahi kukiona kibaya kinaishia ktk sadaka maalumu ya leo maana Agano jipya sasa ni halisia.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu ufunguliwe kila eneo.

Monday, 24 October 2016

Kuwa Mungu Juu ya shoda zote/ Hila zote (Mdo 28:6)

20 abibu, 6
Somo :- KUWA MUNGU JUU YA SHIDA ZOTE / HILA ZOTE ( MDO 28 : 6 )

WAKILI WA MUNGU LEO AMETANGAZA ADUI ZANGU KUWA CHINI YA MIGUU YANGU.

KANISA TUMEFUNULIWA pamoja na Kristo ambaye yupo mkono wa kuume wa Mungu na kanisa liko mkono wa kuume wa Mungu hivyo na Pete iko mkono wa kuume wa Mungu.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza kabisa madui na adui zangu wote kuwa chini ya miguu yangu.
Kila farao katka maisha yangu anaishia hapo kwenye sadaka hiyo aliyekuwa anazuia huduma ya Mungu, yaani chochote kilichowahi kukaa mbele yangu leo ni mwisho mwa 41:42-43.

Ambapo kwa sadaka hii kutoka7:1- imetimia kwa kila mwenye haki.

Kila hila iliyowahi kuwa juu yako leo ni mwisho au chochote kilichokuwa kinafukuliwa kunisumbua leo mwisho.

5 ethanimu, 5 Mungu Aliyetuma wote alijumlisha vitu vyote vikawa chini yake, sasa vitu vyote ni vyangu lakini kabla ya kuvikwa Pete  aingewezekana.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo.

Uhalisia wa Kanisa,Kizazi na Taifa la Mungu

19 Abibu, 6
Somo :- UHALISIA WA KANISA,  KIZAZI NA TAIFA LA MUNGU.

Walawi19:1 - 2,  Walawi11:44-45, kut 16:9 kanisa limetakiwa kuwa takatifu kama Mungu alivyo. Mungu amenifunua kuwa ufalme wa kikuhani na Taifa lake takatifu.

Ktk vizazi vyote Mungu alitamani apate kusanyiko la watakatifu sio tu kwa Kiongozi wa kizazi peke yake.
Mpaka akaleta amri kumi akajenga madhabahu bustani ya Edeni,  akaleta Eliya Ad2 kwa toba isiyoya kawaida lakini haikuwezekana.

Kwa kuwa tumekubali kuolewa na Mungu inamaana tumehamia kwenye maskani ya Mungu mwenyewe Zaburi 15:1-

Na ndani ya maskani ya Mungu hatutaondoshwa milele na hakuna magonjwa, madeni, kesi wala mambo mabaya yote.

Mti wa ujuzi wa mema na mabaya hautakuwepo tena ndani ya kanisa, pia Jina la Mzee wa siku litaonekana kwenye paji la uso wangu ufunuo 22:1-3.

Ufunuo 21:3 maskani ya Mungu ipamoja nami na mambo yote ameyafunua kuwa mapya Ambapo sasa kanisa limeketishwa mkono wa kuume wa Mungu mwenyewe!!!mdo2:34.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na Mungu Aliyetuma wote.

Kusimamisha majira na nyakati za kanisa lisiloenda kinyume na Mungu (lisilo na wachawi)

18 abibu, 6
Somo :- kusimamisha majira na nyakati za kanisa lisiloenda kinyume na Mungu (lisilo na Wachawi)

1 petro 1:10-12 mitume na manabii nao walitamani kuishi majira hii lakini hawakuweza kwa kuwa haikuwa majira yao.

Leo imesimamishwa majira ambayo Mungu hatarajii mimi na wewe "the pool" kwenda kinyume maana hiki ni kizazi chake mwenyewe hatarajii anguko!!!
Mungu alitamani siku zote aabudiwe hata kwa kerubi lakini alimgeuka na kitendo cha Mungu kuabudiwa kwa muda mfupi hakujisikia vizuri.

Ktk kila kizazi kanisa lilienda kinyume na Mungu.

Hakuna jambo lolote linatokea ambalo Mungu halijui.
Tumeingia mkataba na Mungu hatutakwenda kinyume nae, maana tunajiamini na ndivyo iliyochangamana! !!!!!

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu Yoh 6:56 kuteketeza waliotumeza na tuliowameza kizazi cha 1 hadi kizazi cha 4.

Ambayo tuliyameza na yaliyotumeza ikiwa ni pamoja na misingi yote mibaya, mahali tulipowahi kupapenda au tulichowahi kukipenda kinachoendelea kuzuia mahali pa Mungu kuabudiwa na kutumiliki.

Aidha Wakili wa Mungu aliagiza kila mmoja kuorodhesha kile kilichokuwa bado kimemmeza na yeye amekimeza ambacho kinammiliki ili kiteketezwe kwa sadaka hiyo ili kumruhusu Mungu mwenyewe atumiliki.

Karibu usikilize ibada hii muhimu kwako uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii.

Thamani na Faida ya Kuolewa na Mungu Aliyetuma wote Vizazi Vyote

17 Abibu, 6
Somo :- Thamani na Faida ya kuolewa na Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka yenye kibali, shukrani zenye kibali zinazoleta manukato na harufu nzuri takatifu mbele za Mungu.

Ilikufuta mbegu chafu iliyochangamana na mbegu takatifu na kuondoa mbegu chafu ili yochangamana na wenye hila.

Waliokuwa na Lengo la kutoboa Safina tuliyopanda kanisa pamoja na kufuta maji machafu yote Ambapo kwa sadaka hii maalumu inamleta Malaika wa ufunuo 8:3-5 mwenye moto, radi na umeme na tetemeko na kufuta kabisa hayo yote ndani ya Safina tuliyopanda wenye haki.
Aidha Wakili wa Mungu amekemea tabia ya kuleta sadaka mbele za Mungu ikiwa imekunjwa au kuviligwa mkononi na kusema maana ya kukunja na kuviliga fedha ni kuonesha kuwa wewe huna kitu na ni masikini wakati wewe ni Tajiri na fedha ya Goshen Ina Thamani kubwa.

Hata hivyo Wakili ameagiza kanisa kujiandaa kutoa sadaka maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kanisa kuolewa na Mungu maana ni jambo lililotamaniwa ktk vizazi vyote.
Pia kanisa amelitaka kujiandaa kwa ibada ya siku ya 5 kuveshana Pete ya agano mkono wa kuume kwa waliokwenye maagano ya kichwa na kanisa Sambamba na mabinti sayuni ilikuonesha uhalisi wa kanisa kuolewa na Mungu.
Amezitaja Thamani na Faida ya kuolewa na Mungu Aliyetuma wote kuwa ni 1.)Mungu hawezi Kukubali kufiwa na kanisa wake tena.

2.) Hutavuliwa tena mavazi hadharani na waliokushindwa.

3.) Sasa kanisa litamuelewa Mungu maana hakuna aliyeolewa ambaye hamjui kichwa wake yupoje.

4.) Imefutwa kuvuka kanisa pamoja na kundi lingine lisilo sawa.

5.) Kwa kuwa umeolewa na Mungu wewe amini tu utapokea kutoka kwa Aliyetuma wote.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii.

Thursday, 20 October 2016

16 Abibu, 6

2.kukata
Tamaa 3.kutamani
kurudi kwny masufuria ya nyama na kula matikiti ya misri. #Eliya mtishbi 1.kuvunja
madhabahu ya Bwana 2.kumwacha
kiongozi peke yake #maisha ya jeshi la yesu 1:kukataa
kumwombea kiongozi kwa kisingizio cha KUCHOKA 2.Kupenda
kulakula au kupenda vitu *marko 10:28-30.#maisha /tabia za jeshi la Eliya Ad2 M. M...1.hila2.ushetani3.kupenda
vitu 4.kutoelewa5.kusshangaa

Wednesday, 19 October 2016

Siku 7 za ukurasa Mpya wa Kanisa likiwa limeolewa na Mungu Mwenyewe (15-21)Isaya 33:17-24.

15 abibu, 6
Somo :- Siku 7 za ukurasa Mpya wa Kanisa likiwa limeolewa na Mungu mwenyewe (15-21) Isaya 33 : 17-24.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Mungu kuhuluku giza/ubaya wa kila aina Isaya 45:7-8

Kila ubaya, maovu yote na giza lote Mungu amehuluku ktk maisha yetu.

Yaani sadaka hii ni kufuli la mambo yote mabaya ktk maisha yetu Mwa 7:16b.

Kanisa kuanzia sasa ni kao la raha hatuta tanga tanga tena! !!!!
Shida zote za vizazi zilizokuwa zikitufuatilia kuanzia jana Mungu amezifuta hatutaziona tena! !!!
Mimi ni wa Mungu na yeye ni wangu milele! !!!!

Kulikuwa na kipindi cha Uumbaji wa:-
1111 Mwa1:1
1111 mwa 8:13
1111 Luka 2:21
1111 28 adari, 2011

Leo 1111 ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE! !!!!! Imesimama kwa uhalisi wake.

1111 ktk vizazi vyote 4 vilivyopita kila ilipotokea Uumbaji huo waliharibu.

Sasa hivi tuna 1111 ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE na ili wasiingie hapo kuharibu,  Mungu ameweka kufuli.
2 Sam 7:10-11 Mungu amenistarehesha mbele za adui zangu na mahali aliponiweka sitatolewa tena!!!!
Leo ni sikukuu ambayo hajawahi kutokea! !!!

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo. ..........👏

Tuesday, 18 October 2016

Pasaka ya Ufahamu wa Mungu Aliyetuma Wote Vizazi Vyote

14 abibu, 6

Somo :- Pasaka ya Ufahamu wa Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Mungu amefungua ukurasa Mpya wa wenye haki.

Ambapo kwa sadaka maalumu hiyo kila kesi ulizowahi kukutana nazo mwenye haki na mambo yote mabaya kutoka vizazi vyote vilivyopita ndio imeishia leo.

Maana leo Aliyetuma wote ametangaza kuwa uhalisi wa Hosea 2: 18-23 yaani ametuposa na katuoa yeye mwenyewe hatatuacha tena.
Tulikuwa tunaonekana hatufai kabisa ila sasa Mungu ameamua kutuchukua mwenyewe.

Amesema kanisa ilikuwa ngumu kupata udhihirisho kwakuwa lilizingwa na maadui wengi lakini sasa Mungu Aliyetuma wote amewafuta wote.

Lakini pia Amesema kanisa halitapishanishwa tena na mambo mzuri kwani tayali tumeolewa na Mungu mwenyewe.
Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ufunuo huu siku ya leo.

Monday, 17 October 2016

Kanisa na Taifa kulindwa na Mungu kama Wakili wa Mungu anavyolindwa

13 abibu, 6
Somo :- Kanisa na taifa kulindwa na Mungu kama Wakili wa Mungu anavyolindwa!
Leo Wakili wa Mungu alianza ibada kwa kulifutia kabisa madeni yote kwa kuligawia kanisa mchele uliokuwa madhabahuni hapo.
Akimaaanisha kanisa Zima kufutiwa madeni wenye haki wote.

Lakini pia imesimamishwa Sadaka maalumu ya Kanisa kutetewa na Mungu kwa kila kitu.
Yaani vinavyoonekana na visivyoonekana vitasimama kukutetea mwenye haki.
Kutetewa na Mungu kama Wakili wa Mungu anavyotetewa na kila kitu.

Ambapo ameita sadaka maalumu hiyo na mafuta Kanisa tuliyopakwa leo yanaitwa "NIGUSE UONE"

Mstari wa leo tuliofundishwa ni "Heri uniguse mimi kuliko umguse Miaka 1000 maana hautasamehewa" Neno lililosemwa na Eliya Ad2 Mungu wa majeshi.

Sunday, 16 October 2016

Kukamilisha majira na nyakati za kuishi kama Wakili wa Mungu anavyoishi

11 abibu, 6

Somo :- kusimamisha majira na nyakati za kuishi kama Wakili wa Mungu anavyoishi.

Leo majira na nyakati ya uhalisi wa maisha ya Wakili wa Mungu umefunuliwa kwa wenye haki wote.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kulifungua Kanisa macho ya Rohoni ilikupata yaliyomo ndani ya Wakili zaidi ya Ef1 :18 .

Yaani leo amemfunua Wakili wa Mungu kuwa ndiye Aliyetuma.

Aidha ametoa ushuhuda wa maisha yake ktk mambo nane.

1.) Wakili wa Mungu hawezi kufanya chochote Bila msingi wa Neno. Kol3:17.
Amesisitiza kila mmoja kutofanya chochote Bila msingi wa Neno.

2.) Halipizi kisasi. Na wewe Usilipize kisasi kwani kisasi ni cha Mungu Rum12:19-21 nakusema ukilipiza kisasi Mungu hakutetei.

3.) Isaya 33:6 kusubiri majira ya jambo husika ili Mungu akutetee mwenyewe.
4.) 2 nyakati 7:14-16 toba ya unyenyekevu kwa kuwa umeitwa kwa Jina la Mungu Uwe mnyenyekevu.

5.) Kukaa kimya mpaka Mungu aseme kut 14:14.

6.) Kumtegemea Mungu tu bila mchango wowote.  Hesabu18:20.
Rum 8:28 liwe zuri au baya mimi napokea ndani yale Mungu anajua alichokusudia ndani mwake.

8.) Law19:2 Uwe mtakatifu kama Mungu alivyo. Kila mara Mungu yuko mbele yetu hakuna adui atuwezae.

Mafuta ya Kila Mwenyehaki Kuwa Barua inayosomeka vizuri ndani ya Kanisa,Taifa na Mataifa

12 abibu, 6
Somo :- Mafuta ya kila mwenye haki kuwa Barua inayosomeka vizuri ndani ya kanisa, taifa na mataifa.

Wakili wa Mungu akihitimisha ibada hiyo amesimamisha sadaka maalumu ya mwenye haki kusomeka vizuri kwenye Uumbaji wote.

Aidha amefunua mambo 15 yatakayosababisha kanisa tusomeke kama barua nzuri.

1.) Kutambua aliyebeba Mafuta. Nakusema aliyebeba Mafuta sio rafiki yako, mjomba wako wala binamu yako.

2.) Kuambatana naye Aliyebeba Mafuta. 1nyak 11:1-2 Amesema kumtambua aliyebeba Mafuta hakuna mtihani ila mtihani upo ktk kuambatana nae.

3.) Isaya 61:6 unyenyekevu.  Kama huna unyenyekevu Mungu hawezi kwenda na wewe.
4.) Isaya 1:19 ilikula mema ya nchi lazima Uwe na UTII.

5.) Kutembea na Neno la madhabahuni kumb 12:5-7

6.) Kukubali kujaa shukrani majira na nyakati zote Dan6:10
7.) Upendo war 5:3-5

8.) Kukubali kujifunza kwa aliyebeba Mafuta.  Ebra6:12.
9.) Kuwa na hakika ya Neno Isaya 55 : 11

10.) Uwe mtoaji kama Mungu mwenyewe alivyo mtoaji Mdo 20:15
11.) Lazima kulitendea kazi Neno
12.) Kukubali yeyote ambaye ni kusudi la Mungu.  1wath 5:15.
13.) Lazima umwinue mwingine unaposikia amepatwa na shida. Mith 24:17.
14.) Kumwacha Mungu afanye sio wewe maana ndiye anayetumiliki. 1 Kor 15 : 25-28.
15.) Kuwa na Akiba njema ndani ya moyo wako.  Mt 12:32-33.

Wakili wa Mungu alihitimisha ufunuo huo Kwakusema ktk hayo yote yanabebwa na Neno 1 la kuwa MWAMINIFU. LUk17:

Friday, 14 October 2016

Thamani na Faida ya Ufahamu wa Mungu Mwenyewe kabla ya kuumba Kerubi

10 abibu, 6
Somo :- Thamani na Faida ya ufahamu wa Mungu mwenyewe kabla yakuumbwa kwa kerubi.

Wakili wa Mungu Awali akijenga msingi wa ibada hiyo amesimamisha sadaka maalumu ya kufuta na kukausha kabisa maji ya msiba kwa wenye haki Isaya30:20.

"God has flashed out all waters of affliction"  Ambapo kila mnuko na harufu mbaya ya maneno ya uzushi na uongo Aliyetuma wote amefuta!!!

Aidha Wakili wa Mungu ametaja kanuni za kufuata ili kupata Thamani na Faida ya ufahamu wa Mungu mwenyewe kabla yakuumbwa kwa kerubi.

1.) Lazima nimjue aliyebeba Mafuta ya kuongoza kizazi. Usipomfahamu huyo ufahamu hauingii kwako na Mungu anakukataa.  1 Sam 10:1-. Maana kumjua mtakatifu ni ufahamu.

2.) Uambatane naye huyo aliyepakwa mafuta. Kwani matatizo yapo hapo kwenye kuambatana na aliyepakwa mafuta. 2 falme 2:2 wana wa manabii wanajifanya wanajua.

3.) Kutambua majira iliyopo sasa.  Ibada halisi sio jengo au nyumba Bali ni Kutambua kuwa moyo wako ni mbinguni na ndimo Mungu anaishi.

Waabuduo halisi huwa hawaangalii vitu maana Mungu ndiye mwenye vitu vyote.

Mungu katika vizazi vyote anatafuta Nafsi inayomtafuta yeye

9 adari, 6
Somo :- Mungu ktk vizazi vyote anatafuta Nafsi inayomtafuta yeye.

Wakili wa Mungu Amesema ktk umbaji wa Mungu tangu mwanzo ni kutafuta nafsi ambayo inayomjua yeye.

Amesema kama nafsi yako ipo upande wa shetani huwezi kumsikiliza Mungu.

Ameongeza kuwa kikichokuwa kinawapa ugumu kwa waliotumwa ni Nafsi sio kumtafuta Mungu.
Ameagiza kila mmoja kutubu kwa kukosa nafsi inayokataa kumjua Mungu maana Mungu anataka nafsi inayofuta.
Mungu anataka nafsi zote za Dunia kumjua Mungu maana ni kipindi Mungu anaandika sheria zake mioyoni mwetu.

Wote tugeuke nafsi inayofuta Mungu maana huwezi kumtafuta Mungu usifanikiwe.

Kituo cha Ufahamu kabla ya wazo la Mungu kumuumba Kerubi

8 abibu, 6
Somo :- Kituo cha Ufahamu kabla ya wazo la Mungu kumuumba Kerubi.

Wakili wa Mungu Awali akijenga msingi wa ibada hiyo amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza na kufuta kabisa aibu ya aina yoyote.

Amesema sasa ni majira ya kuweka maarifa ya Neno kinywani maana kanisa sasa tumefunuliwa kuwa ni makuhani/ mjumbe wa Bwana.

Majira ya kizazi cha Mungu imefika hivyo hata kama Miaka1000 (au yoyote) atake asitake lakini ilikuwa ni lazima zaidi ya 1 Kor 15:25-28.
Amesema hakuna mwenye nguvu ya kuzuia kizazi cha Mungu.
Haina maana MUNGU alishindwa kuacha kumuumba kerubi hapana Bali alitaka kutupa Somo sisi tutakaoishi kwenye kizazi chake,  kwamba yeye Ana nguvu kiasi gani.
Audio clip 0620719507

Monday, 10 October 2016

Uumbaji Mpya wa Akili Ya Mwenye Haki

6 abibu, 6
Somo :- Uumbaji Mpya wa Akili ya mwenye Haki.

Wakili wa Mungu Amesema kila kizazi ilikuwa lazima kipitie anguko lakini sio sasa hivi.

Mungu badala ya kukimbia mlima wake Bali sasa anauwa hakimbii tena.

Wakili wa Mungu Amesema kwa sasa hivi hata mlima wa Bwana ukichafuliwa Mungu hakimbii maana kwa toba ya Mungu mwenyewe hawezi tena kukimbia mlima wake.

Aidha amesisitiza kanisa kuacha mazoea ya tuliyowahi kumfahamu Mungu Bali sasa Mungu ni ufahamu.

Hata hivyo ameagiza kila mmoja aungane na Malaika wa Uumbaji Mpya wa Mungu mwenyewe Ezekiel 36:26-
Pamoja na kuungana na Malaika wa utekelezaji wa Neno la Mungu litokalo kwenye kinywa cha Mungu mwenyewe Isaya 55:11.

Ikiwa ni pamoja sasa Pete ya agano inavaliwa mkono wa kulia sio kushoto tena.

Sunday, 9 October 2016

kituo cha utajiri na heshima ndani ya Kanisa.

5 abibu, 6
Somo :- kituo cha utajiri na heshima ndani ya Kanisa.

Wakili wa Mungu leo amefunua kweli kuhusu mkono wa kushoto ambao uliibiwa kwa kanisa.

Lakini kwa ibada ya leo Mungu amerejesha mikono yote miwili ndani ya kanisa ambayo imebeba utajiri, heshima na maisha marefu.
Kuhusu utajiri huu mkubwa uliopo ndani ya mikono yako mwenyewe Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupone.

Audio clip ya ibada hii inapatikana kupitia Neema Gavrieli +255 620 71 95 07

Thursday, 6 October 2016

THAMANI NA FAIDA YA UHALISI WA KIZAZI CHA MUNGU

3 abibu, 6
Somo :- Thamani na Faida ya uhalisi wa kizazi cha Mungu.

Kwa kizazi hiki kanisa tumerejea mahali pa kabla ya wazo la kumuumba Kerubi.
Mazoea yote tuliyowahi kuwanayo yanafutwa.  Wengine tuna mazoea ya mifumo ya maisha ya waliotumwa na kutamani na Miaka 1000 awe hivyo hayo mazoea lazima yaondoke maana anaishi tu kadri Mungu anavyoagiza.

Wakili Amesema kwenye kizazi cha Mungu mabadiliko makubwa ni lazima yatokee na Mungu ataenda kutukarabati mwonekano wa kila hali mpaka sisi tutashangaa.

Miaka 1000 ya kutawala na Kristo sasa ndio inaanza kwa uhalisi.
Yale makusudi yote ya Mungu ya tangu mwanzo sasa yanaenda kutimia kwa uhalisi.
Kanisa sasa tunakwenda bega kwa bega na Mungu.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya kufuta mitego na mashimo kwa wenye haki na kuita sadaka ya Isaya 24:16-20.

HONGERA KWA KUHAMA KITUO