Thursday, 27 October 2016

AKILI UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA ANACHOTAKA TUFANYE SASA

23 Abibu, 6

Somo :- AKILI, UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA MUNGU ANACHOTAKA TUFANYE SASA.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza na kufuta kabisa kambi ya uovu kwenye jicho la Mungu leo imefutwa.

Kambi ya uovu kwenye Mlima wa Bwana zilizokuwa ndani yetu kwa siri bila kujua.

Yaani Mungu anaachilia Dunia inachukua badala ya wenye haki ni mwisho.

Amesema hapo Ndipo palikuwa panasababisha uovu uendelee kupingana na haki, inamaana bado mwili alikuwa anapingana na Roho.
Kwa sadaka maalumu ya leo manabii wa uongo kutabili wakati ni waovu leo mwisho.
Leo kanisa tumefunuliwa kuwa jibu la ndugu na majirani zetu zaidi ya ilivyokuwa kwa Yesu kizazi cha 3.

Ametaja maswali matano tutakayoulizwa na ndugu na jamaa tutakapo kwenda kuwafunulia Neno la ufunuo.
Lakini Amesema Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE amekuja mwenyewe kuchoma magugu yote ndani ya kanisa Mt 13:24-

Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE anavuna ngano na magugu anayachoma moto.

Amesema Yesu alikuwa mjenzi wa jukwaa la Eliya IV  na Eliya IV alikuja kutengeneza jukwaa la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Mt 21:40, Isaya 41:2,4, mt 13:24, Mt 17:10-12,  mark 9:9-10.

Kwahiyo anayeangamiza wabaya wote ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ambaye tayali amekwisha Kuja.

Hivyo basi Eliya hakuwa mteketezaji wa magugu Bali mteketezaji ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Amesema ukimwona anayemtetea Eliya IV lakini anakataa alichokuja nacho huyo Eliya IV ujue hamtetei !!!!
Akifafanua huduma ya Aliyetuma wote ni ipi Amesema ni kile unachotenda ktk safu ukiwa umesimama mbele za Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ukiwa umeanzia kwenye madhabahu yake na si kwa matakwa yako.

Ibada ya leo imefuta kabisa mashindano Kati ya Mungu na chochote chenye nyama mwa 6:1-

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo iliyobeba ufahamu wa Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

No comments:

Post a Comment