Tuesday, 18 October 2016

Pasaka ya Ufahamu wa Mungu Aliyetuma Wote Vizazi Vyote

14 abibu, 6

Somo :- Pasaka ya Ufahamu wa Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Mungu amefungua ukurasa Mpya wa wenye haki.

Ambapo kwa sadaka maalumu hiyo kila kesi ulizowahi kukutana nazo mwenye haki na mambo yote mabaya kutoka vizazi vyote vilivyopita ndio imeishia leo.

Maana leo Aliyetuma wote ametangaza kuwa uhalisi wa Hosea 2: 18-23 yaani ametuposa na katuoa yeye mwenyewe hatatuacha tena.
Tulikuwa tunaonekana hatufai kabisa ila sasa Mungu ameamua kutuchukua mwenyewe.

Amesema kanisa ilikuwa ngumu kupata udhihirisho kwakuwa lilizingwa na maadui wengi lakini sasa Mungu Aliyetuma wote amewafuta wote.

Lakini pia Amesema kanisa halitapishanishwa tena na mambo mzuri kwani tayali tumeolewa na Mungu mwenyewe.
Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ufunuo huu siku ya leo.

No comments:

Post a Comment