Showing posts with label 18 Abibu 6. Show all posts
Showing posts with label 18 Abibu 6. Show all posts

Monday, 24 October 2016

Kusimamisha majira na nyakati za kanisa lisiloenda kinyume na Mungu (lisilo na wachawi)

18 abibu, 6
Somo :- kusimamisha majira na nyakati za kanisa lisiloenda kinyume na Mungu (lisilo na Wachawi)

1 petro 1:10-12 mitume na manabii nao walitamani kuishi majira hii lakini hawakuweza kwa kuwa haikuwa majira yao.

Leo imesimamishwa majira ambayo Mungu hatarajii mimi na wewe "the pool" kwenda kinyume maana hiki ni kizazi chake mwenyewe hatarajii anguko!!!
Mungu alitamani siku zote aabudiwe hata kwa kerubi lakini alimgeuka na kitendo cha Mungu kuabudiwa kwa muda mfupi hakujisikia vizuri.

Ktk kila kizazi kanisa lilienda kinyume na Mungu.

Hakuna jambo lolote linatokea ambalo Mungu halijui.
Tumeingia mkataba na Mungu hatutakwenda kinyume nae, maana tunajiamini na ndivyo iliyochangamana! !!!!!

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu Yoh 6:56 kuteketeza waliotumeza na tuliowameza kizazi cha 1 hadi kizazi cha 4.

Ambayo tuliyameza na yaliyotumeza ikiwa ni pamoja na misingi yote mibaya, mahali tulipowahi kupapenda au tulichowahi kukipenda kinachoendelea kuzuia mahali pa Mungu kuabudiwa na kutumiliki.

Aidha Wakili wa Mungu aliagiza kila mmoja kuorodhesha kile kilichokuwa bado kimemmeza na yeye amekimeza ambacho kinammiliki ili kiteketezwe kwa sadaka hiyo ili kumruhusu Mungu mwenyewe atumiliki.

Karibu usikilize ibada hii muhimu kwako uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii.