Monday, 31 October 2016

Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTR 2 Kor 3:2-3

26 abibu, 6
Somo :- Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTE 2KOR3:2-3.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya madhabahu ya kumruhusu Mungu kuteketeza magugu yote ndani ya kanisa Luk 19:27.

Yaani gugu la kila aina Mungu ameangamiza ikiwa ni pamoja na yote ambayo ni kinyume na mwenye haki.
Amesema kwa mafuta ya leo Mungu ataonekana kwetu kwa uhalisi maana magugu yote yameteketezwa ndani ya kanisa.
Huu ni wakati wa Mzee wa siku anayang'oa magugu yote ndani ya kanisa Mt 13 : 24.
Yoeli 2:25 tunutu, madumadu na parare wote Mungu amewaondoa maana hayo yote ni magugu.
Isaya 27:1-4 michongoma yote imefutwa kwako haitakuwepo tena! !!!!

Isaya42:18 Mungu ameondoa upofu, uziwi, uwete, ububu wa rohoni ndani ya kanisa kwa sadaka hiyo maalumu.

Ambapo pia ktk ibada hiyo Wakili wa Mungu ametangaza Tangazo maalumu kutoka mbinguni kuwa Isaya 40:2 kuwa " vita vyako vimekwisha! !!!

Aidha ametaja mambo 5 ya kufanya toba yaliyotaka kuleta laana kwa kanisa.
1.) Hali ya kumlaumu aliyejenga msingi Kwanini aliwaacha mashetani na wenye hila.

2.) Kumlaumu anayejenga jengo Kwanini ananyamaza kimya! !!!!
3.) Tunapofundishwa jambo fulani kubadilika na kukunja uso.

4.) Magugu kuota pamoja na mbegu njema.

5.) (a)Mambo ambayo Mungu alitamka kwa kanisa akiwa amechukizwa kwalo. Ikasababisha waovu watengeneze maagano ya kuliwasha kanisa.

(B.) Yale yaliyotamkwa na waliotumwa ktk vizazi vyote vya kanisa.  Waovu walitumia kulipiga kanisa.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo.

No comments:

Post a Comment