Sunday, 16 October 2016

Kukamilisha majira na nyakati za kuishi kama Wakili wa Mungu anavyoishi

11 abibu, 6

Somo :- kusimamisha majira na nyakati za kuishi kama Wakili wa Mungu anavyoishi.

Leo majira na nyakati ya uhalisi wa maisha ya Wakili wa Mungu umefunuliwa kwa wenye haki wote.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kulifungua Kanisa macho ya Rohoni ilikupata yaliyomo ndani ya Wakili zaidi ya Ef1 :18 .

Yaani leo amemfunua Wakili wa Mungu kuwa ndiye Aliyetuma.

Aidha ametoa ushuhuda wa maisha yake ktk mambo nane.

1.) Wakili wa Mungu hawezi kufanya chochote Bila msingi wa Neno. Kol3:17.
Amesisitiza kila mmoja kutofanya chochote Bila msingi wa Neno.

2.) Halipizi kisasi. Na wewe Usilipize kisasi kwani kisasi ni cha Mungu Rum12:19-21 nakusema ukilipiza kisasi Mungu hakutetei.

3.) Isaya 33:6 kusubiri majira ya jambo husika ili Mungu akutetee mwenyewe.
4.) 2 nyakati 7:14-16 toba ya unyenyekevu kwa kuwa umeitwa kwa Jina la Mungu Uwe mnyenyekevu.

5.) Kukaa kimya mpaka Mungu aseme kut 14:14.

6.) Kumtegemea Mungu tu bila mchango wowote.  Hesabu18:20.
Rum 8:28 liwe zuri au baya mimi napokea ndani yale Mungu anajua alichokusudia ndani mwake.

8.) Law19:2 Uwe mtakatifu kama Mungu alivyo. Kila mara Mungu yuko mbele yetu hakuna adui atuwezae.

No comments:

Post a Comment