Friday, 28 October 2016

THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA MOJA YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

24 Abibu, 6
Somo:-  THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA 1YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa MUNGU amesimamisha sadaka maalumu ya  kanisa kufunuliwa kuwa mbegu njema ambapo kila magugu na pando lisilopandwa na Mungu ndani yetu leo limeteketezwa kabisa.

Kanisa pia limempisha Mungu ili alimiliki kwa sadaka hiyo badala ya kama ilivyokuwa awali ambapo ni Wakili pekee ndiye alimpisha Mungu amiliki kanisa na kulichunga yeye mwenyewe.

Amesema moyo wako, Roho na Nafsi yako ukitaka vidishambiliwe unatakiwa uhamie kwenye kituo cha Aliyetuma wote vizazi vyote.

War2:4 wema wa Mungu huvumilia wote na kuwavuta ili watubu, huu ni wakati wa hukumu ya haki hivyo hata adui zako umpe Mungu wa kumpisha yeye ashughulike nao.
Luka 19:27 waLiomkataa Mungu ni sharti wampishe Mungu awachinje yeye mwenyewe.

Wakili wa Mungu amesema lazima nikubali kutetewa na Mungu kwa kumpisha yeye iliniwe mbrgu njema.

Akizungumzia thamani na faida ya kuwa na huduma 1 ya Mungu Aliyetuma wote amesema (1.) 1wafalme 3:11- Mungu ataachilia ulinzi mkubwa kwangu na kila kinachotajwa kwa jina langu iwapo tu nitavitaja vitu vyangu vyote kwa jina la Aliyetuma wote.

(2.) Luka 19:27 maadui zangu wote kuanzia leo sio wangu tena bali ni maadui za Aliyetuma wote hivyo mimi ninarelax tu.

(3.) Kanisa sasa tumekuwa mbegu njema na hakuna tena yeyote atakayepanda mbegu mbaya Mt 13:24.

Aidha amelionya kanisa kuwa na tabia ya kupenda taatifa kama sungura.

(4.) Sasa utawala wa Kristo ndani yetu unaimalika . Uf 20:6  na kusema kilichokuwa kinapingana na utawala wa Kristo ndani yetu ni tabia za lugha ya ukoo, kabila, mila na destuli mbalimbali.

(5.)maswali yote tuliyokuwa nayo leo tumepata majibu. Kilichokuwa kinazuia tusifanikiwe ni kuwa na maswali mengi ndani ya mioyo yetu ambayo yalionekana kama vile hayana majibu.

Wakili amesema wakati Nabii wa mwisho akiwa kwenye viungo alipenda kusema "PENYE NABII HALIHALIBIKI NENO" ambapo sasa hivi kwa kituo tulichofika ni "PENYE MUNGU ALIYETUMA WOTE HALIHARIBIKI NENO" but unachotakiwa kufanya ni kumpenda tu Wakili wa Mungu!!!!!

Aidha ameagiza kanisa kuwa kabla ya kusalimiana na yeyote mshirikishe Neno la ufunuo yeyote utakayekutana naye, umshirikishe habari za Mungu uliyenaye na yale Mungu anayotutendea kanisa na taifa lote!!!!

Maana hakuna zawadi yoyote tutampa Mungu kwa aliyotutendea zaidi ya kuutangaza ufunuo wake ndani ya uumbaji wote!!!!!!

Karibu usikilize upokee faida na thamani ya huduma moja ya Aliyetuma wote.

No comments:

Post a Comment