17 Abibu, 6
Somo :- Thamani na Faida ya kuolewa na Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka yenye kibali, shukrani zenye kibali zinazoleta manukato na harufu nzuri takatifu mbele za Mungu.
Ilikufuta mbegu chafu iliyochangamana na mbegu takatifu na kuondoa mbegu chafu ili yochangamana na wenye hila.
Waliokuwa na Lengo la kutoboa Safina tuliyopanda kanisa pamoja na kufuta maji machafu yote Ambapo kwa sadaka hii maalumu inamleta Malaika wa ufunuo 8:3-5 mwenye moto, radi na umeme na tetemeko na kufuta kabisa hayo yote ndani ya Safina tuliyopanda wenye haki.
Aidha Wakili wa Mungu amekemea tabia ya kuleta sadaka mbele za Mungu ikiwa imekunjwa au kuviligwa mkononi na kusema maana ya kukunja na kuviliga fedha ni kuonesha kuwa wewe huna kitu na ni masikini wakati wewe ni Tajiri na fedha ya Goshen Ina Thamani kubwa.
Hata hivyo Wakili ameagiza kanisa kujiandaa kutoa sadaka maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kanisa kuolewa na Mungu maana ni jambo lililotamaniwa ktk vizazi vyote.
Pia kanisa amelitaka kujiandaa kwa ibada ya siku ya 5 kuveshana Pete ya agano mkono wa kuume kwa waliokwenye maagano ya kichwa na kanisa Sambamba na mabinti sayuni ilikuonesha uhalisi wa kanisa kuolewa na Mungu.
Amezitaja Thamani na Faida ya kuolewa na Mungu Aliyetuma wote kuwa ni 1.)Mungu hawezi Kukubali kufiwa na kanisa wake tena.
2.) Hutavuliwa tena mavazi hadharani na waliokushindwa.
3.) Sasa kanisa litamuelewa Mungu maana hakuna aliyeolewa ambaye hamjui kichwa wake yupoje.
4.) Imefutwa kuvuka kanisa pamoja na kundi lingine lisilo sawa.
5.) Kwa kuwa umeolewa na Mungu wewe amini tu utapokea kutoka kwa Aliyetuma wote.
Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii.