Monday, 31 October 2016

KUFUNULIWA KWA KANISA LENNYE NYOTA YA MUNGU KWA UPYA

27 Abibu, 6
Somo :- KUFUNULIWA KWA KANISA LENYE NYOTA YA MUNGU KWA UP YA.
1⃣UWE ZA                    (INNER STRENGTH)
2⃣Nguvu.
3⃣Utajiri.
4⃣Heshima.
5⃣Hekima.
6⃣Utukufu.
7⃣Baraka.
Hayo yanakuja kwangu kwa upya na kilichokuwa kinasonga hayo kuonekana kwangu ilikuwa ni magugu.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza agano la waovu kujifunika kifuniko cha wenye haki yaani waliwatanguliza wenye haki mbele ili wakutwe na mishale.

Yaani yeyote anayefanya chochote kwa hila kwa sadaka maalumu hiyo kila hila zote zinateketezwa.

Wakili wa Mungu ameagiza kila mwenye haki siku ya leo ahakikishe anajiwasha kwa ukamilifu ili kurejesha NYOTA za Mungu kwa upya ndani yako.

Amesema NYOTA ya Uweza ilibeba ukamilifu wa NYOTA zote saba ambayo Inaweza kuibiwa kwa kukosa uvumilivu au subira ikiwa ni pamoja na ukijaa maneno mengi.

NYOTA hizi ni uziachilie na kuzifanya kuwa ni MALI ya Mungu Aliyetuma wote kwa wewe mwenyewe kuhiyali kumtanguliza yeye kwenye kila jambo.

Yaani ajulikane Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE kuwa ni Mungu ndiye amefanya. 

Karibu usikilize kwa upendo ili ubarikiwe.

Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTR 2 Kor 3:2-3

26 abibu, 6
Somo :- Mafuta ya KUVIKWA NISHANI YA KUWA BARUA NJEMA YA KUSOMEKA VIZURI NA WATU WOTE 2KOR3:2-3.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya madhabahu ya kumruhusu Mungu kuteketeza magugu yote ndani ya kanisa Luk 19:27.

Yaani gugu la kila aina Mungu ameangamiza ikiwa ni pamoja na yote ambayo ni kinyume na mwenye haki.
Amesema kwa mafuta ya leo Mungu ataonekana kwetu kwa uhalisi maana magugu yote yameteketezwa ndani ya kanisa.
Huu ni wakati wa Mzee wa siku anayang'oa magugu yote ndani ya kanisa Mt 13 : 24.
Yoeli 2:25 tunutu, madumadu na parare wote Mungu amewaondoa maana hayo yote ni magugu.
Isaya 27:1-4 michongoma yote imefutwa kwako haitakuwepo tena! !!!!

Isaya42:18 Mungu ameondoa upofu, uziwi, uwete, ububu wa rohoni ndani ya kanisa kwa sadaka hiyo maalumu.

Ambapo pia ktk ibada hiyo Wakili wa Mungu ametangaza Tangazo maalumu kutoka mbinguni kuwa Isaya 40:2 kuwa " vita vyako vimekwisha! !!!

Aidha ametaja mambo 5 ya kufanya toba yaliyotaka kuleta laana kwa kanisa.
1.) Hali ya kumlaumu aliyejenga msingi Kwanini aliwaacha mashetani na wenye hila.

2.) Kumlaumu anayejenga jengo Kwanini ananyamaza kimya! !!!!
3.) Tunapofundishwa jambo fulani kubadilika na kukunja uso.

4.) Magugu kuota pamoja na mbegu njema.

5.) (a)Mambo ambayo Mungu alitamka kwa kanisa akiwa amechukizwa kwalo. Ikasababisha waovu watengeneze maagano ya kuliwasha kanisa.

(B.) Yale yaliyotamkwa na waliotumwa ktk vizazi vyote vya kanisa.  Waovu walitumia kulipiga kanisa.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo.

Saturday, 29 October 2016

KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI ZA SHAMBA LA MUNGU ALIYETUMA WOTE LENYE MBEGU NJEMA PEKE YAKE MILELE

25 Abibu, 6

Somo:- KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI ZA SHAMBA L A MUNGU ALIYETUMA WOTE LENYE MBEGU NJEMA PEKE YAKE MILELE.

Awali akijenga msingi Wa ibada hiyo Wakili Wa MUNGU amesimamisha Sadaka maalumu ya kila Mwenye Haki kufunuliwa kuwa Panga La Mungu luka19:27 c/o Hosea 2:19.

Yaani Kwa sadaka ya Leo kanisa lote tumefunuliwa kuwa luka19:27 Na kuvunjika kabisa rasmi Agano LA ngano Na magugu kuota pamoja!!!!            Ktk vizazi vyote vya kanisa kulikuwa Na kituo cha kupanda Na kushuka, lakini sababu kubwa ni magugu bado yalikuwepo yakiizonga mbegu njema!!!

Majira ya kung'oa magugu ilikuwa bado Na ukifanya kitu kabda ya majira ya Mungu ananyamaza Mt 13:24.

Hivyo ni Neema kubwa kuishi ktk kipindi hiki cha Mungu mwenyewe.

Aidha Wakili Wa Mungu amezitaja tabia mbalimbali zilizokuwa zikichafua kanisa huko nje:-
(a) kushtakiana1 kor 6:2
(b.) Kulipa kisasi maana kisasi ni cha Bwana. War 12:19-21.

(C.) Kuwafukuza wanaokoka.

(D.) Mdo13:6 kufuta Neno LA Ufunuo.

(E) manung'uniko Na kuona kama Mungu anachelewa. Kut 16:1-

(F) kumtangulia Mungu wakati Mungu ana majira yake ilikufanya kila kitu.

(g.) Kumwibia Mungu.

Nb:-
Ukiwa mbegu njema ya Mungu unahudumiwa Na Mungu mwenyewe.

Karibu usikilize ili ubarikiwe.

Friday, 28 October 2016

THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA MOJA YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

24 Abibu, 6
Somo:-  THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA HUDUMA 1YA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa MUNGU amesimamisha sadaka maalumu ya  kanisa kufunuliwa kuwa mbegu njema ambapo kila magugu na pando lisilopandwa na Mungu ndani yetu leo limeteketezwa kabisa.

Kanisa pia limempisha Mungu ili alimiliki kwa sadaka hiyo badala ya kama ilivyokuwa awali ambapo ni Wakili pekee ndiye alimpisha Mungu amiliki kanisa na kulichunga yeye mwenyewe.

Amesema moyo wako, Roho na Nafsi yako ukitaka vidishambiliwe unatakiwa uhamie kwenye kituo cha Aliyetuma wote vizazi vyote.

War2:4 wema wa Mungu huvumilia wote na kuwavuta ili watubu, huu ni wakati wa hukumu ya haki hivyo hata adui zako umpe Mungu wa kumpisha yeye ashughulike nao.
Luka 19:27 waLiomkataa Mungu ni sharti wampishe Mungu awachinje yeye mwenyewe.

Wakili wa Mungu amesema lazima nikubali kutetewa na Mungu kwa kumpisha yeye iliniwe mbrgu njema.

Akizungumzia thamani na faida ya kuwa na huduma 1 ya Mungu Aliyetuma wote amesema (1.) 1wafalme 3:11- Mungu ataachilia ulinzi mkubwa kwangu na kila kinachotajwa kwa jina langu iwapo tu nitavitaja vitu vyangu vyote kwa jina la Aliyetuma wote.

(2.) Luka 19:27 maadui zangu wote kuanzia leo sio wangu tena bali ni maadui za Aliyetuma wote hivyo mimi ninarelax tu.

(3.) Kanisa sasa tumekuwa mbegu njema na hakuna tena yeyote atakayepanda mbegu mbaya Mt 13:24.

Aidha amelionya kanisa kuwa na tabia ya kupenda taatifa kama sungura.

(4.) Sasa utawala wa Kristo ndani yetu unaimalika . Uf 20:6  na kusema kilichokuwa kinapingana na utawala wa Kristo ndani yetu ni tabia za lugha ya ukoo, kabila, mila na destuli mbalimbali.

(5.)maswali yote tuliyokuwa nayo leo tumepata majibu. Kilichokuwa kinazuia tusifanikiwe ni kuwa na maswali mengi ndani ya mioyo yetu ambayo yalionekana kama vile hayana majibu.

Wakili amesema wakati Nabii wa mwisho akiwa kwenye viungo alipenda kusema "PENYE NABII HALIHALIBIKI NENO" ambapo sasa hivi kwa kituo tulichofika ni "PENYE MUNGU ALIYETUMA WOTE HALIHARIBIKI NENO" but unachotakiwa kufanya ni kumpenda tu Wakili wa Mungu!!!!!

Aidha ameagiza kanisa kuwa kabla ya kusalimiana na yeyote mshirikishe Neno la ufunuo yeyote utakayekutana naye, umshirikishe habari za Mungu uliyenaye na yale Mungu anayotutendea kanisa na taifa lote!!!!

Maana hakuna zawadi yoyote tutampa Mungu kwa aliyotutendea zaidi ya kuutangaza ufunuo wake ndani ya uumbaji wote!!!!!!

Karibu usikilize upokee faida na thamani ya huduma moja ya Aliyetuma wote.

Thursday, 27 October 2016

AKILI UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA ANACHOTAKA TUFANYE SASA

23 Abibu, 6

Somo :- AKILI, UFAHAMU NA MAARIFA YAKUELEWA MUNGU ANACHOTAKA TUFANYE SASA.

AWALI akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza na kufuta kabisa kambi ya uovu kwenye jicho la Mungu leo imefutwa.

Kambi ya uovu kwenye Mlima wa Bwana zilizokuwa ndani yetu kwa siri bila kujua.

Yaani Mungu anaachilia Dunia inachukua badala ya wenye haki ni mwisho.

Amesema hapo Ndipo palikuwa panasababisha uovu uendelee kupingana na haki, inamaana bado mwili alikuwa anapingana na Roho.
Kwa sadaka maalumu ya leo manabii wa uongo kutabili wakati ni waovu leo mwisho.
Leo kanisa tumefunuliwa kuwa jibu la ndugu na majirani zetu zaidi ya ilivyokuwa kwa Yesu kizazi cha 3.

Ametaja maswali matano tutakayoulizwa na ndugu na jamaa tutakapo kwenda kuwafunulia Neno la ufunuo.
Lakini Amesema Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE amekuja mwenyewe kuchoma magugu yote ndani ya kanisa Mt 13:24-

Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE anavuna ngano na magugu anayachoma moto.

Amesema Yesu alikuwa mjenzi wa jukwaa la Eliya IV  na Eliya IV alikuja kutengeneza jukwaa la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Mt 21:40, Isaya 41:2,4, mt 13:24, Mt 17:10-12,  mark 9:9-10.

Kwahiyo anayeangamiza wabaya wote ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ambaye tayali amekwisha Kuja.

Hivyo basi Eliya hakuwa mteketezaji wa magugu Bali mteketezaji ni Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Amesema ukimwona anayemtetea Eliya IV lakini anakataa alichokuja nacho huyo Eliya IV ujue hamtetei !!!!
Akifafanua huduma ya Aliyetuma wote ni ipi Amesema ni kile unachotenda ktk safu ukiwa umesimama mbele za Mungu Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE ukiwa umeanzia kwenye madhabahu yake na si kwa matakwa yako.

Ibada ya leo imefuta kabisa mashindano Kati ya Mungu na chochote chenye nyama mwa 6:1-

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo iliyobeba ufahamu wa Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Wednesday, 26 October 2016

SIKU SABA ZA KUINUA HUDUMA YA MUNGU JUU NA KUFUTA HUDUMA ZOTE ZA KISHETANI (22-28 ABIBU,6)

22 abibu, 6
Somo :- SIKU 7 ZA KUINUA HUDUMA YA MUNGU JUU NA KUFUTA HUDUMA ZOTE ZA KISHETANI (22-28 ABIBU, 6)
Kwa toba ya leo huduma ni moja kama vile Kanisa lilivyo ni moja kwani huduma zingine zilizuia huduma ya Mungu kusimama.
Damu za watoto waliouawa kwa kumsaka Musa kwa agizo la farao na Damu za watoto waliouawa wakati wa kumsaka Yesu zilikuwa bado zinapiga kelele kuua huduma za wenye haki.

Akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha TOBA YAKUFUNGUA LANGO KUU LA TAIFA LA MUNGU.

Uhalisi wa Isaya 60:11 - 14 kwamba Bandari ni lango kuu ni lazima walete vitu vizuri ili wapambe taifa.

sadaka maalumu ya kutengwa na uovu wa kila aina Ebr8:12,  2 Kor 6:17-18.
Umasikini,  ufukara,  magonjwa, vilio ni uovu tumetengwa nao milele.

Chochote ulichowahi kukiona kibaya kinaishia ktk sadaka maalumu ya leo maana Agano jipya sasa ni halisia.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu ufunguliwe kila eneo.

Monday, 24 October 2016

Kuwa Mungu Juu ya shoda zote/ Hila zote (Mdo 28:6)

20 abibu, 6
Somo :- KUWA MUNGU JUU YA SHIDA ZOTE / HILA ZOTE ( MDO 28 : 6 )

WAKILI WA MUNGU LEO AMETANGAZA ADUI ZANGU KUWA CHINI YA MIGUU YANGU.

KANISA TUMEFUNULIWA pamoja na Kristo ambaye yupo mkono wa kuume wa Mungu na kanisa liko mkono wa kuume wa Mungu hivyo na Pete iko mkono wa kuume wa Mungu.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya Kuteketeza kabisa madui na adui zangu wote kuwa chini ya miguu yangu.
Kila farao katka maisha yangu anaishia hapo kwenye sadaka hiyo aliyekuwa anazuia huduma ya Mungu, yaani chochote kilichowahi kukaa mbele yangu leo ni mwisho mwa 41:42-43.

Ambapo kwa sadaka hii kutoka7:1- imetimia kwa kila mwenye haki.

Kila hila iliyowahi kuwa juu yako leo ni mwisho au chochote kilichokuwa kinafukuliwa kunisumbua leo mwisho.

5 ethanimu, 5 Mungu Aliyetuma wote alijumlisha vitu vyote vikawa chini yake, sasa vitu vyote ni vyangu lakini kabla ya kuvikwa Pete  aingewezekana.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo.