Tuesday, 3 January 2017


THAMANI NA FAIDA YA KUACHANA NA UMBO LA KWANZA LENYE UHARIBIFU.


Wakili wa MUNGU amesema Hatma ndio kusudi la kila mmoja ambalo amemkusudia kwani majira hii Kanisa linatakiwa kuwa juu ya Umbo ambalo ulianza nalo.

Kuna jinsi MUNGU atakutoa kwenye Umbo la kwanza maana kila ulichonacho kina nafsi na mahali MUNGU alipotupeleka ni juu sana mahali alipotukusudia tangu mwanzo.

Aidha Wakili ameongoza Wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kutengwa na mwanzo wa umbo lenye uharibifu.

Hatahivyo  ametaja sababu za MUNGU kutupeleka juu zaidi ya viungo kuwa ni pamoja na kututenga na wale ambao wamekataa kuhama vituo na kutupeleka mahali ambapo hakuna umbo.

Maana tukiwa na umbo ni rahisi kupigwa na Yule mnyama mwenye umbo lisiloeleweka maana mahali tulipo ni juu ya viungo nilivyoanza navyo. Watoto wapo juu ya viungo vilivyoanza.

Nitaanza kupendeza zaidi. Maumivu ya kizembe zembe hutayasikia ndipo utakapo kuwa juu umehama kituo.

Hatma ya ila Mwenye haki atendaye kwa haki 1Yoh 5:8-9

Kumkamilisha MUNGU. Maana MUNGU ni MUNGU lakini bila Kristo na Kanisa hakamiliki. Ukamilifu wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa.

Umoja wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa. Namba 1 aliyokusudiwa na MUNGU na inakamilishwa na Kanisa. Hiyo namba 1 ni Kanisa.

Kwahiyo kama ulikuwa huliombei Kanisa sasa utaliombea. hatma 1 halisi ni kumkamilisha MUNGU.

Kuhakikisha Kristo anatawala na Kanisa  juu ya nchi.

Uf 20:6. Ufu 22:4 watamuona uso kwa uso akiwa nyumbani kwako, shambani kwako nk.

Ukitembea kwa mguu
                    Kwa ndege}
                    Kwa gari  
MUNGU ataonekana hivyo hivyo.

Haya yalikuwa hayawezekani mpaka utoke kwenye umbo la 1 la uharibifu na uingie juu zaidi  pasipo kuwa na umbo lililotangulia.

Mwa 18:1 ilitokea Israel kwa Ibrahimu majira hi MUNGU anataka tuonekane kila mahali tukiwa na MUNGU na Kristo.

Math 19: 23-25 Israel ya mwilini ndio ilikuwa urthi wake. Hawataki taifa hili liitwe urithi wa MUNGU. Hawataki Hatma halisi ya Kanisa kwani utajiri halisi utaonekana ndani ya taifa kwa sababu ya nguvu ya hatma ya Kanisa.

Ukikutana na anayezuia mafanikio haya utafanyaje? utampeleka kwa MUNGU amtambue yeye mwenyewe.

Hivyo shukrani zetu zibadilike ili haya yote yatokee kwa amri moja halisi.

Watakusalimia kwa heshima. Wataona wewe ndiye chanzo cha thamani nzuri. Hazina lulu na juya.

Milionea, trionea na bilionea huwa wanajifanya ndio madini, fedha, uchumi.

Kama umekubali kuwa na zaidi ya umbo la 1 basi utaonekana kuwa thamani halisi.

*NB:-*Karamu ya leo imegeuzwa kuwa ni Sheria ya Roho wa Uzima inayonitenga kabisa na sheria ya mauti.

Somo:AMRI MOJA HALISI.

Wakili alianza kwa kymshukuru Mungu kwamba Dan 2:35-44 imetimia , Zaidi sana alisema naanza kwa kusoma Zaburi 114:1-6 Kwa amri mmoja 1.Bahari itakimbia kwetu 2.Yordan imefutwa kabisa 3.milima lazima iruke kama kondoo waume 4.Nchi lazima itetemeke 5.vilima lazima viruke 6.miamba yote imesagika na kuwa ziwa LA maji 7.Jiwe gumu kuwa chem chem KITUO HIKI ni cha AMRI MOJA HALISI Mabaya yote Leo ni mwisho mwisho MAMBO YA KUSIMAMISHA SHUKRAN:na kufuta kabisa 1.Mataifa yote yaliapa kuwa Dan 2:35-44 haiwezi kutokea Goshen 2.sadaka mbali mbali zimetokea ili isay 2 2 isitimie 3.viapo na makufuru vimetamkwa kwa Taifa na kanisa wasifanye Kazi pamoja yaani math 21: 41-43 isitimie 4.kulikuwa na hila za kila namna kuwa kanisa LA kweli halitakubalika kamwe Goshen ingawa limetokea hapo 5.saini mbali mbali za kuzuia kanisa LA kweli kupokelewa 6.uumbaji wote kusainishwa kiunajimu kuwa usikubali kanisa wala Wakili wa Mungu 7.Mashindano makuu na Mungu ndani na NNE ANza shukrani sasa . Leo umbo LA kerubi Leo limefutwa kabisa Na maumbo ya kila aina . Futa na wew hayo yote kwa shukrani

HATMA MOJA HALISI


Wakili wa MUNGU amefunua kuwa ilikupata hatma moja halisi ni lazima kutubu kwaajili ya kufuta Agano la mfanano milele na kufuta umbo la kwanza milele.

Wakili wa MUNGU amesema Leo kitabu kinaandikwa na tofauti kati ya mwenye haki na mwovu lazima ijulikane. 2.) anayemtumikia Bwana na asiyemtumikia lazima ajulikane.

3.) Sasa  mimi nimeachiliwa kuwa hazina ya MUNGU. Amesema MUNGU anataka wote tuwe na hatma moja halisi. Na iwapo tukiwa na hatma moja hakuna mwenye kumkanyaga mwingine.

Kila mmoja nyumbani kuwa na amani na furaha kwa afya nzuri itokayo Madhabahuni. Hatma moja halisi ni zaidi ya viungo. Na ukishatoka kwenye umbo la kwanza utaona ugonjwa uliokuwa unakusumbua unakukimbia.

Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya Madhabahu iliyosimamisha hatma moja halisi zaidi ya viungo.

Sadaka hiyo inakutoa kwenye hatma ya kwanza na kukupeleka hatma moja halisi. Inakutoa kwenye umbo la kwanza na kukupeleka kwenye juu ya viungo.

Hata umbo la kwanza la MUNGU, Kristo, Wakili wa MUNGU,  kizazi na Taifa tunatoka hapo na kuwekwa kwenye hatma moja halisi juu ya viungo.

Efeso 1:18  macho ya mioyo yetu yatiwe akili yapate kuona. Kushukuru kwaajili ya kuwa:-
+ Mti wa uzima.

+Na njia ile iendayo uzimani tunayo.

+Hakuna anayepita katika njia hiyo.

 Awali akijenga msingi Wakili wa MUNGU amevitaja na kufafanua vituo ambavyo Kanisa tumepita katika mwezi siwani mwaka 6.

Friday, 4 November 2016

THAMANI NA FAIDA YA MUNGU ALIYETUMA KUSIMAMISHA JUU YA WALIOTUMWQ

3 Zivu, 6

Somo :- THAMANI NA FAIDA YA MUNGU ALIYETUMA WOTE KUSIMAMA JUU YA WALIOTUMWA.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha Sadaka maalum ya Hakuna aliye juu ya Toba ya Mungu Aliyetuma wote vizazi vyote ambayo inafuta kufa na mauti zote.

Aidha katka ibada hiyo Wakili  ametangaza kufutika kabisa ugonjwa wa kufisha uliokaa ndani ya moyo wa mtu uliosumbua waliotumwa ktk vizazi vyote yer 17:9-10.

Sasa moyo hauna ugonjwa wa kufisha tena kwani Aliyetuma wote vizazi vyote anakaa ndani ya moyo akiwa juu ya wote.

Hatahivyo atangaza kurejeshwa Kwa vitu waliotumwa waliondoka navyo na haikuwa rahisi kuvipata mpaka ilibidi aje yeye mwenyewe Aliyetuma wote ili virudishwe na Mungu.

Musa:-
ile nguvu ya kuvuka bahari ya shamu Kwa utayali yaani ile nguvu ya mafuta makubwa ya kuvuka kila eneo Kwa ushindi mkubwa.

Joshua:-
ile nguvu ya uhodari na ushujaa ambapo sasa kila mahali nitakuwa na uhodari na ushujaa wa wivu wa Bwana.

Eliya Mtishibi:-
Ile nguvu ya kushusha moto wa Mungu ambapo sasa Aliyetuma wote ameachilia moto mkubwa wa kuteketeza maadui wa Kanisa.

Elisha II:-
Mji huu sio na njia hii sio yaani sasa kila anayeniwinda atapotea njia yeye mwenyewe.

Yesu:-
Nguvu ya kufuatwa na makutano mkubwa ya watu ambapo sasa makutano mengi na makubwa kuja kwa Aliyetuma wote vizazi vyote.

Petro:-
Nguvu ya kivuli kuponya imerejea sasa kivuli cha mwenye haki kuponya na kuwaleta Kwa Mungu.

Paulo:-
Nguvu ya kuona vitu vyote kama mavi.  Yaani marejesho ya kutokamatwa na kupenda vitu.

Eliya Ad2:-
Utiisho wa Mungu.  Nguvu ya Utiisho wa Mungu imerejea ndani ya Kanisa milele.

Karibu usikilize Kwa upendo uhame vituo vya Ufahamu.

Thursday, 3 November 2016

SIFA ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

2 zivu, 6

Somo:- SIFA ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

WAKILI wa Mungu leo amefunua sifa zaidi ya 22 ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE na kusema kuwa majira imefika ambapo miungu yote imekwisha angamizwa kwani sasa MUNGU ni moja tu Aliyetuma wote vizazi vyote.

Alianza ibada hiyo Kwa toba ya kina Kwa kuliongoza Kanisa zima ya kufuta roho ya miungu ndani ya Kanisa kutokana na waliokalia kiti cha Mungu Yosh7:1

Lakini awali akijenga msingi wa ibada hiyo alisimamisha Sadaka  maalum ya kupendelewa na Mungu Aliyetuma wote vizazi vyote kwani 1petro 1:10-12 manabii walitafuta kujua haya yatakuwa lini wakafunuliwa si kwao bali kwaajili yetu kizazi cha Mungu.

War 2:11 inasema Mungu hana upendeleo lakini Kwa Wakili wa Mungu na Kwa Kizazi cha Mungu tumependelewa.

Hatahivyo atangaza tarehe rasmi ya kukabidhi jengo la wodi ya kufunulia watoto tuliyojenga ktk jiji la Kristo kigoma zamani kuwa Itakuwa 14 zivu, 6 tuwe tumefika huko.

Nauli ni 100,000/- kwenda na kurudi na vyumba vya kulala ni kuanzia 10, 000/- hadi 20,000/-kwa chumba.

Hata hivyo bado hazina 5 zinahitajika ilikukamilisha milango na madilisha ya jengo hilo hivyo tunatakiwa kuchangia haraka iwezekanavyo ilitufanikishe.

Karibu uhame kituo

Tuesday, 1 November 2016

KIZAZI CHA MUNGU ALIYETUMA Yoh 9:7

28 abibu, 6
Somo :- KIZAZI CHA MUNGU NI ALIYETUMA YOH9:7

Wakili wa Mungu leo ametangaza rasmi kuwa SILOAMU NI ALIYETUMA SIO TENA ALIYETUMWA.

Amesema kuna ufahamu, hekima,  ufunuo na Neno la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE 1kor15:25-28.

Na kuna ambayo hakusema kupitia waliotumwa ktk vizazi vyote lakini amekuja nayo mwenyewe.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya kusimamisha madhabahu ya kizazi cha Mungu Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Yoh 9:7.

Ambapo kupitia sadaka hii maalumu anguko la kila kizazi limefutwa kwakuwa sio mimi na wewe sio mali tena ya Aliyetumwa Bali ni mali ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Siloamu ni Aliyetumwa:-
Musa alitumwa kizazi cha kwanza kut3:10,  Eliya mtishibi alitumwa kizazi cha pili 1wafalme17:1-, Yesu alitumwa kizazi cha tatu Mdo:10:38,  Eliya Ad2 alitumwa kizazi cha nne yoh 9:7

lakini sasa Mungu amekuja mwenyewe kuongoza Siloamu kizazi cha Mungu 1kor15:25-28 hivyo sasa Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Alifafanua kuwa ilikuwa haiwezekani Mungu kuachilia vitu vizuri wakati Siloamu ilikuwa kwenye kituo cha waliotumwa.

Amesema mahali na kituo leo kanisa lilipohamia hautapigwa tena,  hutakuwa fidia ya waovu tena.

Hivyo basi leo tuna kila kitu kipya yaani familia Mpya, viungo vipya, agano jipya, kizazi kipya, promotion Mpya, utendaji mpya, afya mpya nk.
Alisema alipokomboa kazi zote ni kwa sababu kazi zote ni za Mungu na Mungu alikuwa anafanya maandalizi ya Siloamu kuwa ni ya Aliyetuma wote mwa 1:26-28,                   mwa 3:20
Yoh 9:7.
Kama Siloamu haingekuwa ni ya Aliyetuma sasa wakati wa kizazi cha Mungu Ina maana yafuatayo yangeendelea:-
1⃣Haki ya nafsi ya mtu.
2⃣Tabia ya asili.
3⃣sheria ya dhambi.
4⃣matendo ya mwili.
5⃣mahali pa juu pa kila kitu.
6⃣Anguko
7⃣haki ya mzungu kujiona yuko juu na haki ya mwafrika kujidharau.
Mimi sio mwafrika ni kizazi cha Mungu.

Pia mambo haya ya misingi mibovu isingeweza kuvunjika iwapo:-
⏺babeli yaani mafarakano Ambapo sasa ni umoja wa familia ya Mungu sio mafarakano.
⏺Ibada za mwilini.
⏺wazo la pili yaani kusimama na Neno la madhabahuni hata kama halina logic.
⏺kuibiwa kwa mlima wa Bwana (ufahamu) nafsi ya mtu ilikuwa inaiba.
⏺haki ya nafsi ya mtu.

Hivyo basi kanisa tumetengwa kabisa na mabaya yote yaliyowapata kanisa kizazi cha kwanza hadi cha nne.

Leo kanisa na mwenye haki wamevuka.

Sasa ni wakati wa kujifunza kanuni za Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE na pia tusiwe wakosoaji yaani style ya kuishi ibadilike.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo.