Showing posts with label 28 Abibu 6. Show all posts
Showing posts with label 28 Abibu 6. Show all posts

Tuesday, 1 November 2016

KIZAZI CHA MUNGU ALIYETUMA Yoh 9:7

28 abibu, 6
Somo :- KIZAZI CHA MUNGU NI ALIYETUMA YOH9:7

Wakili wa Mungu leo ametangaza rasmi kuwa SILOAMU NI ALIYETUMA SIO TENA ALIYETUMWA.

Amesema kuna ufahamu, hekima,  ufunuo na Neno la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE 1kor15:25-28.

Na kuna ambayo hakusema kupitia waliotumwa ktk vizazi vyote lakini amekuja nayo mwenyewe.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya kusimamisha madhabahu ya kizazi cha Mungu Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Yoh 9:7.

Ambapo kupitia sadaka hii maalumu anguko la kila kizazi limefutwa kwakuwa sio mimi na wewe sio mali tena ya Aliyetumwa Bali ni mali ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Siloamu ni Aliyetumwa:-
Musa alitumwa kizazi cha kwanza kut3:10,  Eliya mtishibi alitumwa kizazi cha pili 1wafalme17:1-, Yesu alitumwa kizazi cha tatu Mdo:10:38,  Eliya Ad2 alitumwa kizazi cha nne yoh 9:7

lakini sasa Mungu amekuja mwenyewe kuongoza Siloamu kizazi cha Mungu 1kor15:25-28 hivyo sasa Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Alifafanua kuwa ilikuwa haiwezekani Mungu kuachilia vitu vizuri wakati Siloamu ilikuwa kwenye kituo cha waliotumwa.

Amesema mahali na kituo leo kanisa lilipohamia hautapigwa tena,  hutakuwa fidia ya waovu tena.

Hivyo basi leo tuna kila kitu kipya yaani familia Mpya, viungo vipya, agano jipya, kizazi kipya, promotion Mpya, utendaji mpya, afya mpya nk.
Alisema alipokomboa kazi zote ni kwa sababu kazi zote ni za Mungu na Mungu alikuwa anafanya maandalizi ya Siloamu kuwa ni ya Aliyetuma wote mwa 1:26-28,                   mwa 3:20
Yoh 9:7.
Kama Siloamu haingekuwa ni ya Aliyetuma sasa wakati wa kizazi cha Mungu Ina maana yafuatayo yangeendelea:-
1⃣Haki ya nafsi ya mtu.
2⃣Tabia ya asili.
3⃣sheria ya dhambi.
4⃣matendo ya mwili.
5⃣mahali pa juu pa kila kitu.
6⃣Anguko
7⃣haki ya mzungu kujiona yuko juu na haki ya mwafrika kujidharau.
Mimi sio mwafrika ni kizazi cha Mungu.

Pia mambo haya ya misingi mibovu isingeweza kuvunjika iwapo:-
⏺babeli yaani mafarakano Ambapo sasa ni umoja wa familia ya Mungu sio mafarakano.
⏺Ibada za mwilini.
⏺wazo la pili yaani kusimama na Neno la madhabahuni hata kama halina logic.
⏺kuibiwa kwa mlima wa Bwana (ufahamu) nafsi ya mtu ilikuwa inaiba.
⏺haki ya nafsi ya mtu.

Hivyo basi kanisa tumetengwa kabisa na mabaya yote yaliyowapata kanisa kizazi cha kwanza hadi cha nne.

Leo kanisa na mwenye haki wamevuka.

Sasa ni wakati wa kujifunza kanuni za Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE na pia tusiwe wakosoaji yaani style ya kuishi ibadilike.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo.