Friday, 4 November 2016

THAMANI NA FAIDA YA MUNGU ALIYETUMA KUSIMAMISHA JUU YA WALIOTUMWQ

3 Zivu, 6

Somo :- THAMANI NA FAIDA YA MUNGU ALIYETUMA WOTE KUSIMAMA JUU YA WALIOTUMWA.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha Sadaka maalum ya Hakuna aliye juu ya Toba ya Mungu Aliyetuma wote vizazi vyote ambayo inafuta kufa na mauti zote.

Aidha katka ibada hiyo Wakili  ametangaza kufutika kabisa ugonjwa wa kufisha uliokaa ndani ya moyo wa mtu uliosumbua waliotumwa ktk vizazi vyote yer 17:9-10.

Sasa moyo hauna ugonjwa wa kufisha tena kwani Aliyetuma wote vizazi vyote anakaa ndani ya moyo akiwa juu ya wote.

Hatahivyo atangaza kurejeshwa Kwa vitu waliotumwa waliondoka navyo na haikuwa rahisi kuvipata mpaka ilibidi aje yeye mwenyewe Aliyetuma wote ili virudishwe na Mungu.

Musa:-
ile nguvu ya kuvuka bahari ya shamu Kwa utayali yaani ile nguvu ya mafuta makubwa ya kuvuka kila eneo Kwa ushindi mkubwa.

Joshua:-
ile nguvu ya uhodari na ushujaa ambapo sasa kila mahali nitakuwa na uhodari na ushujaa wa wivu wa Bwana.

Eliya Mtishibi:-
Ile nguvu ya kushusha moto wa Mungu ambapo sasa Aliyetuma wote ameachilia moto mkubwa wa kuteketeza maadui wa Kanisa.

Elisha II:-
Mji huu sio na njia hii sio yaani sasa kila anayeniwinda atapotea njia yeye mwenyewe.

Yesu:-
Nguvu ya kufuatwa na makutano mkubwa ya watu ambapo sasa makutano mengi na makubwa kuja kwa Aliyetuma wote vizazi vyote.

Petro:-
Nguvu ya kivuli kuponya imerejea sasa kivuli cha mwenye haki kuponya na kuwaleta Kwa Mungu.

Paulo:-
Nguvu ya kuona vitu vyote kama mavi.  Yaani marejesho ya kutokamatwa na kupenda vitu.

Eliya Ad2:-
Utiisho wa Mungu.  Nguvu ya Utiisho wa Mungu imerejea ndani ya Kanisa milele.

Karibu usikilize Kwa upendo uhame vituo vya Ufahamu.

Thursday, 3 November 2016

SIFA ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

2 zivu, 6

Somo:- SIFA ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE.

WAKILI wa Mungu leo amefunua sifa zaidi ya 22 ZA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE na kusema kuwa majira imefika ambapo miungu yote imekwisha angamizwa kwani sasa MUNGU ni moja tu Aliyetuma wote vizazi vyote.

Alianza ibada hiyo Kwa toba ya kina Kwa kuliongoza Kanisa zima ya kufuta roho ya miungu ndani ya Kanisa kutokana na waliokalia kiti cha Mungu Yosh7:1

Lakini awali akijenga msingi wa ibada hiyo alisimamisha Sadaka  maalum ya kupendelewa na Mungu Aliyetuma wote vizazi vyote kwani 1petro 1:10-12 manabii walitafuta kujua haya yatakuwa lini wakafunuliwa si kwao bali kwaajili yetu kizazi cha Mungu.

War 2:11 inasema Mungu hana upendeleo lakini Kwa Wakili wa Mungu na Kwa Kizazi cha Mungu tumependelewa.

Hatahivyo atangaza tarehe rasmi ya kukabidhi jengo la wodi ya kufunulia watoto tuliyojenga ktk jiji la Kristo kigoma zamani kuwa Itakuwa 14 zivu, 6 tuwe tumefika huko.

Nauli ni 100,000/- kwenda na kurudi na vyumba vya kulala ni kuanzia 10, 000/- hadi 20,000/-kwa chumba.

Hata hivyo bado hazina 5 zinahitajika ilikukamilisha milango na madilisha ya jengo hilo hivyo tunatakiwa kuchangia haraka iwezekanavyo ilitufanikishe.

Karibu uhame kituo

Tuesday, 1 November 2016

KIZAZI CHA MUNGU ALIYETUMA Yoh 9:7

28 abibu, 6
Somo :- KIZAZI CHA MUNGU NI ALIYETUMA YOH9:7

Wakili wa Mungu leo ametangaza rasmi kuwa SILOAMU NI ALIYETUMA SIO TENA ALIYETUMWA.

Amesema kuna ufahamu, hekima,  ufunuo na Neno la Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE 1kor15:25-28.

Na kuna ambayo hakusema kupitia waliotumwa ktk vizazi vyote lakini amekuja nayo mwenyewe.

Awali akijenga msingi wa ibada hiyo Wakili wa Mungu amesimamisha sadaka maalumu ya kusimamisha madhabahu ya kizazi cha Mungu Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE Yoh 9:7.

Ambapo kupitia sadaka hii maalumu anguko la kila kizazi limefutwa kwakuwa sio mimi na wewe sio mali tena ya Aliyetumwa Bali ni mali ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Siloamu ni Aliyetumwa:-
Musa alitumwa kizazi cha kwanza kut3:10,  Eliya mtishibi alitumwa kizazi cha pili 1wafalme17:1-, Yesu alitumwa kizazi cha tatu Mdo:10:38,  Eliya Ad2 alitumwa kizazi cha nne yoh 9:7

lakini sasa Mungu amekuja mwenyewe kuongoza Siloamu kizazi cha Mungu 1kor15:25-28 hivyo sasa Siloamu ni ya Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE.

Alifafanua kuwa ilikuwa haiwezekani Mungu kuachilia vitu vizuri wakati Siloamu ilikuwa kwenye kituo cha waliotumwa.

Amesema mahali na kituo leo kanisa lilipohamia hautapigwa tena,  hutakuwa fidia ya waovu tena.

Hivyo basi leo tuna kila kitu kipya yaani familia Mpya, viungo vipya, agano jipya, kizazi kipya, promotion Mpya, utendaji mpya, afya mpya nk.
Alisema alipokomboa kazi zote ni kwa sababu kazi zote ni za Mungu na Mungu alikuwa anafanya maandalizi ya Siloamu kuwa ni ya Aliyetuma wote mwa 1:26-28,                   mwa 3:20
Yoh 9:7.
Kama Siloamu haingekuwa ni ya Aliyetuma sasa wakati wa kizazi cha Mungu Ina maana yafuatayo yangeendelea:-
1⃣Haki ya nafsi ya mtu.
2⃣Tabia ya asili.
3⃣sheria ya dhambi.
4⃣matendo ya mwili.
5⃣mahali pa juu pa kila kitu.
6⃣Anguko
7⃣haki ya mzungu kujiona yuko juu na haki ya mwafrika kujidharau.
Mimi sio mwafrika ni kizazi cha Mungu.

Pia mambo haya ya misingi mibovu isingeweza kuvunjika iwapo:-
⏺babeli yaani mafarakano Ambapo sasa ni umoja wa familia ya Mungu sio mafarakano.
⏺Ibada za mwilini.
⏺wazo la pili yaani kusimama na Neno la madhabahuni hata kama halina logic.
⏺kuibiwa kwa mlima wa Bwana (ufahamu) nafsi ya mtu ilikuwa inaiba.
⏺haki ya nafsi ya mtu.

Hivyo basi kanisa tumetengwa kabisa na mabaya yote yaliyowapata kanisa kizazi cha kwanza hadi cha nne.

Leo kanisa na mwenye haki wamevuka.

Sasa ni wakati wa kujifunza kanuni za Aliyetuma wote VIZAZI VYOTE na pia tusiwe wakosoaji yaani style ya kuishi ibadilike.

Karibu usikilize kwa upendo uhame vituo vya ufahamu na kupona kupitia ibada hii ya leo.