Saturday, 21 January 2017


MAJIRA NA NYAKATI YA MOYO MMOJA HALISI KWA KILA MWENYE HAKI NDANI YA UUMBAJI WOTE

Wakili wa MUNGU alianza kwa shukrani kwa kuwa moyo wa pili hauta onekana kwa yule atendae kwa haki. Moyo wa kufa, kaburi n.k hautakuwepo tena.
“Nimejifunza kuwa, kusudi la MUNGU halizuiliwi hata kama walikuona hufai n.k
watakutafuta tu.
Hakuna atakae kumbuka jinsi ulivyopakwa mavi n.k au jinsi walivyotukana Siloamu.”
Shukrani kwa MUNGU kwa moyo ninaoondoka nao ni Moyo wa MUNGU.
Aidha Wakili wa MUNGU leo amefundisha kwa kufafanua mistari miwili tu ya NENO ambayo ni Matendo3:19,21 akaifunua kuwa matendo3:19 (mtaji) na 21 (faida).
Kwa moyo moja utakao ondoka nayo leo baada ya toba hata kama ulikuwa tambala la deki hutakuwa hivyo ni lazima watakutafuta.
Maana unaondoka na madhabahu ya moyo mpya na kila kitu kinafunuliwa kwa upya ikiwa ni pamoja na kiungo kimoja kimoja pia kinafunuliwa kwa upya.
Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya madhabahu ya kupokea moyo mpya na kila kitu kufunuliwa kwa upya kutokana na majira na nyakati ya moyo mmoja halisi kwa kila mwenye haki ndani ya uumbaji wote.
Toba kwa ajili ya uliofanyiwa bila kujua katika haya fuatayo:-
#kuwaza,
#kunena,
#kutenda,
#kushitaki
  #na kuomba kinyume.
Toba kwaajili ya uliyofanya wewe mwenyewe bila kujua au kwa kujua;-
#kuwaza
#kunena
#kutenda
#kushtaki
#kuomba.
Yawezekana ulipokuwa tumboni kuna waliokuwazia vibaya vikaingia mpaka kwenye damu na hata leo bado tunaviona, futa kwa Damu ya MUNGU.
Kuna waliokuwazia mabaya tangu tumboni mwa mama yako eg. Atazaa malaya, jambazi hata leo unaonekana hivyo.
Hata ulipokuja Siloamu siku ya kwanza ukaongozwa sara ya toba kuna waliokuwazia vibaya, kuzungukwa zungukwa kwa ayaliyowazwa.
Kuna yaliyonenwa yaliyomabaya unayoyajua na usiyoyajua leo tutubu.
Kila kitu kitakuwa kipya baada ya toba hii.
Like Father
        Like Son.
Kuna uliyotendewa na wengine umejitahidi kusahau lakini bado unakumbuka.
Kuna mambo ulishtakiwa hata pasipo wewe kujua tutubu.
Kuna mengi umeombewa kinyume mengine unajua na mengine hujui tutubu kwa hayo yote.
Kuna uliyowahi kufanya wewe mwenyewe kwa sababu ya uliyofanyiwa, kuwaza kinyume na MUNGU, Kristo, Kanisa, Wakili wa MUNGU, Taifa.
Kuna uliyowaza tofauti na kinyume na MUNGU ukasema wana kijicho leo tutubu.
Kuna niliyoyanena kinyume ukifikiri uko sahihi kumbe haupo sahihi.
MUNGU akupe Neema ya kushinda kujihesabia haki kwa kutubu kwa yale yote tuliyotenda kinyume kwa sababu ya yale niliyonena.
Daniel na Nehemia walitubu kwaajili ya ambayo hawakukosa taifa likapona.
Kuna uliyowahi kushitaki, kujishtaki. Kufuta kwa toba niliyoomba kinyume na wengine.
TUbu kwaajili ya kuendelea kuishi ktk majira ya 1-6 leo MUNGU atusamehe.
Kama ukimaanisha leo unatoka na vitu vizuri ambavyo havijakuonekana kwani haya ndio yalikamatia kizazi cha kwanza hadi cha nne.
Isaya 30:20 MUNGU leo ameyang’oa yote mabaya.
Haya yote yalikuwa yanasababisa kukosa kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha nne, kung’ang’ania majira ya kwanza hadi ya sita.
“haya ndio yaliokuwa yakisabababisha mnifananishe na waliotumwa. Mimi sio nabii, ,mchungaji n.k, nimembeba MUNGU   Aliyetuma wote.
Ukiniona imetosha hata usiponishika mkono”
Kwa sadaka hii kila mmoja akafute kisasi cha ushindi na kishindo cha ushindi.
Moyo wa uzalishaji: Mathayo 12:33
Leo tumepokea moyo wa uzalishaji kila utakacho shika kitapendwa na kile utakacho tamka kita tokea.
Huo ndio moyo wa uzalishaji, utakwenda mahali kuliko kauka kuta badilika saa hiyo hiyo.
Kila mmoja ata tamani uendeshe gari lake ili kiwanda chake kiende juu. Wewe subiri tu magari yanakuja.
Kwa majira ya leo ukienda sehemu ya jangwa ndani ya mwezi mmoja lazima:-
*watajua kupika maandazi.
*watakula matunda.
*watajua kuuza matunda.
*wakifundishwa wanaelewa.
Moyo wa uzalishaji unakupa kujua au kupokea kila kitu kizuri.
Moyo huo unasababisha wengine kufahamu walivyokuwa hawafahamu kwa mwezi mmoja. Wote wenye viwanda watatamani utumie bidhaa zao. 
“Leo umeondoka na moyo wa uzalishaji”
Aidha alihitimisha ibada hiyo kwa kusimamisha moto ulao kwa yeyote aliyekuwa amejipanga kuiba ushindi wa kizazi cha MUNGU wa leo!

Friday, 20 January 2017


THAMANI NA FAIDA YA KUNG’OA KIINI CHA UOVU NDANI YA UUMBAJI WOTE

Wakili wa MUNGU alianza kwa kuunganisha na msingi wa ibada ambapo Mtendaji wa Wakili wa MUNGU leo amefuta viapo alivyowahi kuweka kwa waliotumwa na kuKiweka leo kwa Mungu Aliyetuma wote.
Wakili wa MUNGU alisema kuwa, “ jengo lilisubiri kiapo hiki kwa muda mrefu, sasa tuna hakika ya safari”.
Mtendaji wa Wakili Wa MUNGU alisimamisha Kiapo kuwa: *“Niko Hai na sintakufa;*
*MUNGU hata-aibika*
*Kristo hata-aibika*
*Wakili Wa MUNGU hata-aibika*
*Kanisa halita-aibika*
*Kizazi hakita-aibika*
*Taifa halita-aibika*
Wakili alisema Kiapo hiki kimekata kata mabomba yote machafu.
Aidha Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalum ya Mith 4:23 kwamba Moyo wako hautachakaa maana unalindwa na kiapo, una ulinzi usiokuwa wa kawaida na una uhakika usiokuwa wa kawaida.
Moyo wako hautaingiwa na mshale wowote, kila kitu kita leta faida.
Sadaka hii ina simamisha agano kuwa hutafadhaika tena kwa lolote.
*“Sasa rasmi ufalme wa MUNGU umehama kutoka mashariki ya kati kuja hapa, hakuna siku kama ya leo. Hutafadhaika tena, umbaji umetaharuki.”* aliongeza Wakili katikati ya shukrani.
MUNGU aliwahi kufadhaishwa na *kerubi
   *Adamu
   *mwanamke
   *kizazi cha 1-4
   *waliotumwa
   *kanisa la kizazi 1-4
   *Leo ni mwisho.
"Nasimamisha uhalisi wa kanisa kutofadhaishwa na yeyote"
Je ni ipi thamani na faida ya kungoa kiini cha uovu ndani ya umbaji wote?
Utakaa juu tu, hutashuka hata siku moja. isaya 66:22. MUNGU Hayuko chini, yuko juu tu. Hata akikaa ndani ya moyo Anakaa ndani ya moyo ulio juu.
Sasa hakuna chochote kitakacho kushusha chini tena. Wote waliomwasi MUNGU watakuwa mizoga na watu wote wataokoka.
“ MUNGU Anakaa katikati ya wanadamu yaani juu ya nchi na wote watamabudu na kwa Yule anaemwamini anakuwa kuhani wake na kristo.
MUNGU Anabadilisha mtazamo uliokuwa nao kuhusu YEYE. Ile MUNGU Ameleta mbingu mpya  na nchi mpya.”
Kwa nini Mungu amebadili mtazamo?
Wote waliotumwa walikuwa Mungu, lakini mambo haya kwenda vizuri. Sasa MUNGU Hawezi kuendelea na utaratibu uliopita.
Hekima ya kizazi cha 1-4 Leo umefutwa, utendaji wa kizazi cha 1-4 ni mwisho umefutwa Leo. Isaya66:22 na Ufunuo21:1-3 tazama ya kale yote yamepita sasa yamekuwa mapya.
Hekima ya MUNGU sasa ni ktk viwango vya mstari ulionyooka nyuzi 180, hakuna DOA, hakuna kukosea, hakuna kujitetea, hakuna kujihesabia HAKI yaani ukubali kumilikiwa na MUNGU.
“Alisema kila goti ni lazima lipige mbele zake, jambo hilo ni sasa hivi. MUNGU Akiendelea na utendaji wa zamani, dunia haitatikisika na watu hawatakuja na YEYE Anataka waje.”
Hekima ya MUNGU kuwa ndani ya kila mmoja. Yeremia 31:34
MUNGU kuharibu hekima zilizokuwepo, itabaki hekima ya MUNGU peke yake isiyo na doa. Hekima ya MUNGU ni mstari ulionyooka.
Mlima wa uzalishaji umerudi madhabahuni. Mlima wa uzalishaji ulikuwa bado duniani lakini sasa imerejea kanisani.
Makuhani wa madhabahuni walipotumwa nje walikuwa wakitafuta kuongeza watu sio uzalishaji kwa kuwa mlima wa uzalishaji ulikuwa duniani. Sasa hivi makuhani watafuatilia kwa kila mmoja kuona wanacho zalisha na kukiinua.
Maana tuna nguvu ya uzao, kustawi na kuongezeka.
2 falme 2:19 sasa hivi takataka zote zimerudi kwa waliomwasi MUNGU. Nguvu ya uzao na kuongezeka sasa imerejea,
“MUNGU Amefuta kabisa ule mwanzo  wa uharibifu, Mwanzo Malidadi upo hapa Gosheni (Tanzania). Mwambie kila mmoja hilo.
Sasa shamba la MUNGU limerudi kanisani, waovu walikuwa wamegawana maploti. Leo MUNGU Amekurejeshea ploti kila unachofaya kina tiki.”
“Umeingia mahali pako na mbegu ya kupanda unayo, ukipanda itaota na utavuna. Uta barikiwa na kumiliki mlango wa adui zako. Kichwa wako Amerejea na nguvu za ajabu Ana maploti ya kutisha yenye kila unacho kihitaji.”
Ile bustani ya Eden ilitakiwa kuwa Gosheni sasa imerejea maana waligawana gawana sana, ni lazima waje kuwekeza hapa maana kuna connection ya uzalishaji wa rohoni. Maana mmiliki Amekuja Mwenyewe, Mwenye shamba Amekuja wapangaji wote Amewatoa.
Waliomwasi MUNGU ndio basi tena, na waliokuwa wakiku dharau wata kushang’aa.
“sadaka ya leo ilikuwa inakuanda kuchukua ploti kama utachukua ploti ya  kiwanda  cha uzalishaji au makampuni, masupermarket n.k na ulinzi moja halisi unao.
Nimekupa homework kesho uniambie ni ploti ipi unachukua kwenye shamba hilo.”
Karamu:- sheria ya roho wa uzima, leo inakupa, mlima wa uzalishaji na ikupe ufahamu ya kuchukua ploti yako kwenye shamba la MUNGU.

Thursday, 19 January 2017

BAADA YA KIAPO NI AGANO

Wakili Wa MUNGU alianza  kwa shukrani kwa kusanyiko kubwa lenye Moyo Mmoja Wa MUNGU, MUNGU amepata kusanyiko kubwa sana kizazi hiki lenye Moyo mmoja Wa MUNGU.
Ambapo pia tumepakwa mafuta ya ukamilifu na utimilifu.
Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya kuondoa kabisa kiini cha uovu kilichokuwa kinakuletea shida kwenye familia, Agano lako, biashara, kampuni, mashamba, viwanda, nk ndani ya Moyo wako.
Yer  50:20 Maovu yamefutwa. Dhambi, uovu na uasi utatafutwa wala hautaonekana.
Ebr 8:10-12 Maovu yamefutwa, haya-kumbukwi tena
Isa 30:20-21 Sauti ya MUNGU inasikika ikisema  “NJIA NI HII HAPA”
Huyu ndiye huyu siye.
Kila Maovu, dhambi na uasi kwa Sadaka hiyo aliigeuza kuwa Sadaka ya Shukrani  ili MUNGU kutenda zaidi ya tuliyo-shukuru.
Kuna mwingine amekuwa akijitahidi kuachana na uongo, rushwa, kufyonza n.k leo kiini hicho kinang’oka, Kiini cha kupenda udaku na mambo ya dunia kinang’oka, Kiini cha kusengenya wengine n.k kinang’oka.
Shukrani kwa MUNGU kwa kuwa mwenye Haki  amefika mahali MUNGU anapoishi mahali pa Moyo mmoja Halisi.
Moyo ni chanzo cha kila kitu, sasa tuna-Moyo wa MUNGU.
“Acha Moyo wako ufurahi, furaha yako inapiga maadui. Leo ni siku ya ajabu ufurahi”
Chujio la MUNGU Kristo na Wakili wako Kanisa lipo kazini. Nakusema kiini cha moyo ni level ya juu mno.
MUNGU anaondoa kiini cha wewe kukusudia mema yakatokea mabaya, kuanza vizuri na kumaliza vibaya anang’oa.
Kukusudia kanisa anatokea mwanamke, kukusudia kichwa anatkea mwanaume anang’oa.
MUNGU Kung’oa kiini cha:
Kuanza vizuri kuishia vibaya
Wazo la kwanza na la pili
Utasa, kuachana, mafarakano n.k
Dini na dhehebu, Mti wa ujuzi wa mema na mabaya Ajali, kifo na mauti, wachawi, wanga, wanajimu, washirikina, magonjwa yote MUNGU anang’oa.
Uzee, magonjwa
Nafsi yako kuibiwa
Kulima ukapanda mbegu njema palepale madumadu, tunutu, wakaingia shambani kula mazao leo ni mwisho.
Kiini cha kukuta kaskazini matajiri kusini ni masikini kinafutwa.
Mwanzo wa uharibifu kiini chake kimeng’olewa kimeondolewa.
“Kiapo chochote kina-Agano. Katika kila kiapo ulichoapa kina-agano ndani yake, Kuna viapo ulivyoapa kwa kujua/kutokujua na ndotoni sasa ndani ya kiapo hicho kuna-Agano.
Ili tuweze kukaa na huyu ni lazima tuingie Agano na MUNGU.
Katika Mwa 22:15 MUNGU alimwapia Ibrahimu akatengeneza Agano, Agano ni lazima liwe na Sadaka.
“Wakili Wa MUNGU ameapa na sisi tuna-Agano la kuto-aibika lakini ni kwa Yule atendae kwa haki tu, kwa mwovu haitokei. Wewe umemfuata MUNGU Wa kweli huta-aibika Milele”
Amesema kuna viapo unaweza kuapa bila wewe mwenyewe kujua, pia katika kila kiapo unachofuta unatakiwa ufute na Agano uliloweka.
Aidha amesisitiza kila mmoja kufuta maagano yote ili yasije kuwa mtego kwako mwenye haki.
Leo futa viapo hivyo ili uwe huru na MUNGU awe kuachilia ule utajiri halisi pale ulipo, unapomuapia MUNGU naye anakuapia na wewe.
Leo Kanisa tunamuapia MUNGU kwamba hatutamuacha milele.
Warumi 9:4 MUNGU aliwaapia kwa viapo hivyo na maagano ya MUNGU kuwa nasi.
“Kiapo kimesimama na Agano limesimama usiwe na wasiwasi”

Wednesday, 18 January 2017


MOYO MMOJA HALISI

Wakili wa MUNGU alianza kwa shukrani kwa MUNGU kuwa Siloamu ni Moyo Mmoja Wa MUNGU.  Kwa kila mmoja tunaondoa kila kilichokuwa kikisababisha mioyo mingine.
Kila Mmoja Ndani yake kuna Huduma Mpya kutokana na Moyo Mmoja Wa MUNGU.
Jinsi ya kuondoa vizuizi vya huu Moyo mmoja halisi:-
Kuna mahali uliwahi kujitoa kwa watu kabisa na kinachojitoa ni moyo, sasa tunataka tuuondoe ili tuweze kuwa na Moyo Mmoja Halisi.
Kuna mahali uliwafundisha wengine chochote na wakaelewa na kinachofundisha ni moyo,sasa inatakiwa asikae yoyote pale akazuia usiwe na Moyo Mmoja Halisi.
Kuna uliye-mwapia kuwa hutamwacha kamwe na ni mtu kabisa, kilichomwapia ni moyo, sasa asije akakaa pale na kukuzuia usiwe na Moyo Mmoja Halisi.
Kinachozalisha ni Moyo, sasa kwa kuwa tuna Moyo Mmoja Halisi ni lazima tuongezeke mno.
Kuna mahali/ukoo Fulani ulienda ukapapenda ukaacha moyo wako huko, sasa inatakiwa umkabidhi MUNGU.
Katika ibada hii leo Wakili Wa MUNGU amefuta kiapo alichowahi kuapa kuwa *“Nikiwa Hai Eliya Hatatukanwa!”* na kusema kiapo hicho kilikuwa kikiwaficha waovu kwa kusema tuna-kiapo cha Miaka 1000.
Na ndipo Wakili Wa MUNGU amesimamisha Kiapo kuwa:
*“NAAPA; Kwa kuwa Niko Hai na Sinta-kufa MUNGU Aliyetuma Wote vizazi vyote hata-aibika, Kristo Hata-aibika, Kanisa Halita-aibika, Kizazi cha MUNGU Hakita-aibika, Taifa la MUNGU Halita-aibika”*
Aidha Wakili Wa MUNGU aliongoza Kanisa kutoa Sadaka ya Shukrani kwa MUNGU kwa kuwa Makuhani  sasa Wana-Moyo Mmoja Wa MUNGU ambapo chochote kilichokuwa kinazuia usiwe na Moyo Mmoja Halisi kina-ungua hapo kwenye Sadaka hiyo maalumu.
Kila kiapo ulicho-apa kilichokuwa kinazuia Moyo Mmoja Halisi kina-ungua hapa
“kila nilipokuwa nikiwaita Makuhani waliokuwa wanafaidi ni wengine sio Makuhani kwa kuwa kulikuwa na Moyo wa pili sasa kwa kuwa Makuhani wana-Moyo Mmoja Wa MUNGU, wote waliokuwa wakiiba HAWAJAPATA KITU” alifafanua.
“Tatizo lilikuwa moyo wa pili; wa nje walikuwa wanafaidika kwa sababu ya moyo wa pili na Kanisa lilikuwa haliongezeki kwa sababu ya moyo wa pili
Sasa Tuna-Moyo Mmoja Halisi:-
Wa nje hawapati kitu.
Kanisa sasa linaongezeka.
Taifa hili ndilo Bustani Ya Edeni tulikuwa hatujaliona hilo kwa kuwa tulikuwa na moyo wa pili. Ma-giant wote unaowaona huko nje walitokea hapa.
Utajiri wote unaouona huko nje ulitokea hapa.
=>sasa tumepokea Moyo Mmoja Halisi na Tumeingia Bustani Ya Edeni.
=>Uzalishaji wa kutisha sasa ni lazima.
=>Maongezeko katika kila ufanyalo sasa ni lazima.
=>Sasa MUNGU kapata Kao kwa kila mmoja mahali hapa.
=>Ile kusema hapa ni mahali pa MUNGU kuweka miguu ilikuwa haiwezekani kutokana na moyo wa pili.
=>Sasa kwa kuwa tuna-Moyo Mmoja Wa MUNGU, MUNGU amepata Nafasi/mahali pa kukaa.
Sadaka hii tunaunganuisha na:-
+Wema wako.
+Utukufu wako.
+Uwepo wako
+Majeshi yako
+Moyo Roho Nafsi yako
+ Hakika ya Neno, Safari.
+Ukamilifu wa ushindi.
+Neno lako.
+Ufahamu wako.
+Mamlaka na utisho wako.
+Nguvu, kifua chako.
Sadaka hii ya shukrani tunaiuma kwenye kila kinachoitwa kwa majina yako mwenye haki itakupa hata yale ambayo hatujayaomba.
“Wiki hii ni lazima kila Mmoja Apane"

Tuesday, 17 January 2017


PASAKA YA MUNGU KUGHAIRI MWANZO WA UHARIBIFU NA KUSIMAMISHA MWANZO MALIDADI MILELE

Wakili Wa MUNGU alianza kwa Shukrani kwa MUNGU na kusema Kama umeingia hapa una-huzuni, una-wazia unamdai/anaekudai, aliyekudhurumu una-mioyo sio MOYO.
MUNGU anaangalia Moyo sio Mioyo na Moyo huo uulinde
Hakikisha una-Moyo wa MUNGU, Moyo wa ni kumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli.
Isa 14:13 Moyo wa MUNGU mahali pa Mlima wa Mkutano moyo wa kerubi mahali pa mlima wa Mungu.
Unapo-waza kinyume ina-maana una-moyo wa kerubi na moyo huo unatupwa chini.
Huyu anae-zuia usiwe na Moyo wa MUNGU leo tuna-shungulika nae.
Unapoambiwa Siloamu ni Mbaya wakati umepona na ukakubali huo ni moyo wa pili. Katika mda mfup unafurahi Neno ukitoka linayeyuka yaani una-ghairi Neno huo ni moyo wa pili.
Hiyo roho inayosababisha ughairi: Neno, utakatifu, kutenda mema.
#MUNGU Leo anaghairi Mwanzo wa uharibifu.
# MUNGU anaghairi alivyolighairi kanisa.
# MUNGU anaghairi kumuumba kerubi.
# MUNGU anaghairi kumuweka alama kaini kusema alindwe.
#Mungu anaghairi kuhusu mwenye HAKI kupigwa. Ayubu22:21.
MUNGU anaghairi kutokea kwa *mwanamke.
*nyoka
*anguko
*mioyo miwili.
Aidha Wakili aliongoza wenye HAKI kutoa Sadaka maalumu ya leo ni Kukaa na MOYO wa MUNGU wa kutenda mema Peke yake na mioyo mingine yote kufutwa kabisa.
Kuna namna ambayo unapata Hakika ya Neno halafu ghafla ukimwombea mwingine unasema; isipotokea je?
Hicho ndicho kinaiba Kile kilicho kuwa kimemeza uhalisi  wa kila ulichopewa na MUNGU kinamezwa badala ya kukumeza.
Ile doubt inayokuja baada ya kusikia NENO kinaungulia hapa kwenye sadaka.
Kile kitendo kutoka kanisani kwenda kwa mganga leo ni mwisho. Kila kinachotoka madhabahuni lazima kitimie.
Kutoka 24:12-, kutoka 32:7-8
Kizazi cha kwanza, hata kama umekwenda juu kiasi gani ama una moyo wa MUNGU kiasi gani ilikuwa  lazima ushuke chini.
Leo ni mwisho  na yote yaliokuwa ya kisababisha kushuka moyo leo MUNGU Anaondoka.
Leo moyo unapokuwa juu tu, ukijua kuwa MUNGU Anakuwazia mema tu.
Yeyote akikuletea taarifa mbaya mwambie ina muhusu kerubi
Yeremia 1:4-11 MUNGU hukuweka juu sana lakini unaona uko chini. Leo MUNGU Anakupeleka juu, usishuke tena. Usianagalie hali ulionayo tena.
Uibiwe usiibiwe, ona mema tu.
Leo MUNGU Anapokupeleka juu ,utashuka tena?
MUNGU Anapoachilia Moyo wake Mwenyewe hatarajii kuona ukiangalia mazingira tena.
-yohana 21:3-10 MUNGU Yuko hapa Anakupa vitu vizuri alafu unamwacha, je utapata kitu?
Kunawalioko hapa ambao wakiona msukosuko wanasema ng’oja nikae kwanza  nyumbani hadi hali hii iishe.
*Mahali  penye msukosuko kuna MUNGU,  kusipokuwa na msukosuko ina maana unatenda anayotaka kerubi.*
Wewe unapewa  na MUNGU vitu vikubwa alafu unakutana na msukosuko, unadondosha  chini?
Kwa sababu yeyote nisikute
Nafsi yako imeinama. "upokee furaha ya milele na kicheko cha milele".
"Nikikuona umeinama nafsi sitakusalimia na hata ukinisalimia sitaitikia" alisema Wakili wa MUNGU.
*Leo ni Pasaka ya MUNGU anaghairi mwanzo wa uharibifu milele na kusimamamisha Mwanzo Malidadi.*

Monday, 16 January 2017


KUFUNULIWA KWA KANISA LENYE MOYO MMOJA TU WA MUNGU

Wakili wa MUNGU Alianza ibada kwa uongoza wenye haki kutoa SADAKA YA: Kufuta agano la kutanguliwa kwa wenye HAKI Kila wanapotaka kushinda.
Ni sadaka ya kuishi ADEN na EDEN bila kutoka *kufika nimefika na kutoka sitoki*
Ni kusimamisha ukamilifu wa ushindi.
Kuingia EDEN na kukaa hapo hapo, baada ya kuondoa umbo la nyoka. Sasa tumefika kwenye ukamilifu wa ushindi.
Kuondoa agano la kutanguliwa kwa mwenye haki kila anapotaka kushinda. Katika kila eneo natangaza  ukamilifu wa ushindi kwa kuondoa agano la kutanguliwa.
Kanisa sio kwamba lilikuwa halija shinda, ukamilifu wa ushindi ulikuwa bado. Kila utakacho tamka ni lazima kitokee.
Leo tumepata ukamilifu wa ushindi, kazi ndio imeanza kwa mwenye haki kujiwekea ulinzi waovu wasikuvulie uchafu wao tena bali waokoke.
Mwa3:1-6, 3:1-3, moyo unaomwelekea MUNGU kwa kuongea sawa na Alichosema.
Mwa 3:4-6, moyo unaomwelekea kerubi kwa sababu ya kuamini uongo.
Hii ni mioyo miwili ndani ya mtu mmoja au ndani ya mwenye haki mmoja. Kuna kipindi unaongea kama MUNGU Alichosema, na kuna kipindi unaongea kama ndugu n.k nakuamini hata kama ni uongo.
SWALI: Ni kitu gani kilitokea hadi kerubi/ nyoka akafanikiwa kumdanganya mke wa Adam?
Mwa3:4-6, aliamini kuwa MUNGU nimbaya hataki tufanane naye.
Mkakati Katika Mwa3:4-6  nyoka alifanikiwa kuonyesha kwa mke wa Adam yaani kanisa kuwa MUNGU hampendi Adam, ila yeye kwa kuwa amewaibia  siri ndio mzuri.
MUNGU kuonekana mbaya, kerubi kuonekana mzuri.
Yale ambayo MUNGU Alikusudia kumpa Adam na mkewe hakupewa tena; Hiyo ndio hasara kwa kanisa. Hata vile alivyopewa Adam vilienda kwa kerubi.
Ndio maana mwenye haki kila anapofanya kizuri anaonekana kuwa anajipendekeza. Kila anachofanya mwenye haki kuonekana ni kibaya na mwovu kizuri.
MUNGU leo Anang’oa  kabisa huo moyo mwingine maana MUNGU Anataka moyo usio na mawazo wala makunyanzi.
Sasa moyo wa pili haupo tena na hauna nafasi tena ndani yako, ndani yako kuna moyo mmoja tu.
Moyo unaotokana na mataifa ulioenda, jamii, n.k haupo tena.
Sasa maongezeko yatakuwa makubwa maana kila kinacho toka hapa kinazaa matunda. Tumerudi katikati ya bustani ya EDEN hatutoki tena.
Ni wakati wa uzalishaji wa kumaanisha maana tumeingia CENTRE. Kile ambacho MUNGU Atakiachilia kwetu kitakaa hakitaibiwa tena. Kuna tabia ya kujihukumu kwa mwenye haki sasa tuache.
Nataka sasa umwambie MUNGU nitukanwe/ nisitukanwe kwenye kiini sitoki.
Yeyote akija kukuambia kinyume, mwambie kamwambie kerubi. Mimi sitoki.
+ufunuo 12:1-3 imefutwa kwa uhalisi.
+mwa1:2 Giza ukiwa na utupu mwisho.
+mwa2:8 mti wa ujuzi wa mema na mabaya umefutwa.
#kanisa tunakabidhiwa Mwa2:15 bustani kuilima na kuitunza.
Sasa MUNGU Anatuunganisha Na jeshi la:-
*kuwa na hakika ya safari kutimia.
*kuwa na hakika ya NENO kubarikiwa.
*kuwa na hakika ya kuinuliwa.
*kusudi la MUNGU kutokuzuiliwa na yeyote milele.
*aliyonena MUNGU yote yanatimia.
Ezekiel 36:26 MUNGU ametupa
#moyo MPYA.
#Roho mpya.
#Nafsi mpya.
Wakili amesema SILOAMU ambayo MUNGU alimpa Eliya Ad2 ndio imeanza Jana baada ya kufuta mioyo na tukabaki na Moyo.
Karibu usikilize ibada ya Leo upokee Moyo mmoja tu wa MUNGU.........

Sunday, 15 January 2017


KUOMBA AU KUSHUKURU KWA NAFSI YA MUNGU

WAKILI WA MUNGU alianza kwa kusema kila Neno litokalo Madhahuni ni lazima litokee. Neno la Madhabahuni ni lazima lithibitike.
1YOH 5:8 Umoja wa MUNGU, KRISTO NA KANISA = kila anae-kuona unaomba/unashukuru aone unashukuru kwa Nafsi ya MUNGU, Wote wajue kuwa sisi na MUNGU ni KITU KIMOJA.
Zab 27:4 kutafuta UZURI WA BWANA.
JE; unatafuta gari, nyumba n.k kwa ajili ya Nani? Kwa ajili yako ajisifie kwa wengine au kwa ajili ya utukufu wa MUNGU?
Kila mmoja leo ajipime hapa madhabahuni kama unataka kutubu/utubu kama kushukuru/ushukuru. Mdo 13:22-23 kwa kuwa unaomba kwa Nafsi ya MUNGU basi unampendeza MUNGU.
Unapo-nyoa leo hivi/kesho hivi ni kwa Nafsi ya Nani? =unapo-suka leo hivi/kesho hivi ni kwa Nafsi ya Nani? Unapo = weka hivi mara ukate hivi mara hivi ni kwa Nafsi ya Nani?
Wengi hatuna Moyo bali tuna-Mioyo na MUNGU anataka tuwe na Moyo Mmoja tu wa kwake Mwenyewe. MUNGU anataka sasa uombe kwa Nafsi yake sio yako.
*1samweli 11:1- ili hanna  apate mtoto ilibidi aombe kwa Nafsi ya MUNGU Waamuzi 14:1-3 Zab 50:12
MUNGU anataka Nafsi zetu tuziunganishe na yeye moja kwa moja, sio kwamba ana-shida. MUNGU anataka kila mahali ulipo aonekane lakini uwe na Moyo wake uombe kwa Nafsi yake.
Swali: nina Moyo wa kerubi ua wa MUNGU? Mwa 3:1-3
Ukiona unashindwa kuomba kwa Nafsi ya MUNGU ujue una- mioyo sio Moyo wa MUNGU.
Uwe na Moyo wa MUNGU mwenyewe ili ushukuru/uombe kwa  Nafsi ya MUNGU.
Tukubali kuanzia leo, tuwe na Moyo Mmoja Wa MUNGU ili tuombe kwa Nafsi ya MUNGU.
1 FALM E 3:5-13 kuomba kwa Nafsi ya MUNGU ni Chochote unachotaka kwa ajili ya utukufu wa MUNGU pokea sasa hivi. Unataka kibali, kutetewa  na uumbaji kwa ajili ya utukufu wa MUNGU pokea sasa hivi.
Je;unataka nini kwa ajili ya utukufu wa MUNGU? Pokea sasa hivi kila unachotaka
“kama unataka chochote kwa ajili ya  MUNGU apate heshima,utukufu,sifa; MUNGU ni lazima akupe”
Awali akijnga msingi wa ibada hiyo Wakili wa MUNGU alisema Zab 98:4- kila mmoja kumsifu BWANA -Furaha yako ni lazima ijulikane
“kila ambacho MUNGU amenitamkia ni lazima kitimie.
Ndani ya Moyo wa MUNGU cha kwanza ni sifa na sisi tunamsifu MUNGU, MUNGU hakuwahi kusifiwa”.
Ni lazima tumshukuru MUNGU kwa  kuwa tumependelewa mno, tumepewa Neema Kubwa.  Nataka nione furaha yako unapomwambia  MUNGU ASANTE.
Eze 34:1-23(a) MUNGU mwenyewe kuwaachisha kazi wachungaji wa kondoo na kutaka kondoo zake. MUNGU sasa anachunga kondoo  zake mwenyewe”. MUNGU kuweka Mchungaji Mmoja ambae ni YEYE MWENYEWE.
MUNGU amekuja mwenyewe maana anataka usiishiwe tena, usipungukiwe tena, usionewe tena, usilale njaa tena n.k.
MUNGU yuko na wewe hapo ulipo wewe utendae kwa HAKI, Hapohapo unapoanzia MUNGU anakuwa pamoja na wewe.
MUNGU ni Halisi kwetu formula zote za waovu kuangusha kanisa/Mwenye Haki zimefeli na hazipo tena. Adamu aliibiwa Nafsi Hai yenye Pumzi Hai na ndicho kinacho tafutwa na waovu kwa mwenye Haki.
Sasa MUNGU amekuja mwenyewe kuishi nasi hatoki wachafue /wasichafue hatoki.
SEMA;
Nidanganywe/nisidanganywe, nibezwe/nisibezwe/, nitukanwe/nisitukanwe n.k  EDENI NIMEINGIA SITOKI. Kama unajijua wewe ni Mwenye Haki basi yeyote anae kuja kushindana na wewe hashindani na wewe bali anashindana na MUNGU na huwezi kushindwa, tambua kila kitu chako kiko salama.
Aidha leo wenye haki wametoa Sadaka maalumu ya: “Kurejesha wema na ufahamu wa MUNGU mahali pake”
Kila aliyetenda Wema akiwa mwenye Haki, MUNGU alikuwa hatukuzwi na wewe mwenye Haki upewi hata asante. Kwa anzia sasa hivi, asifiwe na kutukuzwa MUNGU  kwa kila wema utendao.
Wema, Sifa, Utukufu  umerudi kwa mwenyewe na ijulikane kuwa Mfadhili  ni MUNGU sio yeyote.
Ukipanda Mema utavuna Mema, utatenda mema na kulipwa mema. mwovu hataweza kuchukuwa mema badala yako.
Toba kwa waliokuwa wanachukuwa wema,sifa, utukufu wa MUNGU.