Sunday, 29 January 2017


KUFUNULIWA KWA MAJIRA NA NYAKATI ZA KUPENDEZWA NA KWELI ILYOMO MOYONI ZAB 51:6

Wakili wa MUNGU alipo karibishwa Madhabahuni alianza ibada kwa kusema Shika Nenoooooo!... habari  za siku nyingi? Mnaendeleaje?
Nimekuja kuunganisha KWELI na MOYO maana nimeona wengine wanauliza maswali  kwamba WAKILI alisimamisha KWELI moja  halafu MTENDAJI anaendelea kufundisha MOYO mbona masomo tofauti.
Somo lipo sahihi kabisa kwa sababu hiyo KWELI haikuwepo na iliposimamishwa au ingesimamishwa isingekuwa na mahali pa kukaa maana Moyo haukuwepo ndani yetu ila tulikuwa na mioyo!!
KWELI hukaa ndani ya MOYO, kuna wanaopigana vita kwa sababu hawajui KWELI na hata wangeijua haikuwa na mahali pa kukaa na haikukubaliwa kabisa.
Hivyo wengi waliburuzwa kwa kutoijua hiyo KWELI ya MUNGU. Kuna waliomkataa MUNGU, wakamkosoa na kumdhihaki kwa kutoijua KWELI. Sasa KWELI imepata mahali pa kukaa.
Swali Wakili wa MUNGU aliuliza:- Wangapi walinimiss??  Haah!! Ina maana mlikuwa hamnialiki? …..[tunakualika] sasa kama mnanialika kunimiss kunatoka wapi?  Mnanimisi vipi? 
Ina maana hua hamnialiki kila siku kila wakati mahali ulipo kwenye biashara mlima wa moto ofisini?
Je huwa hamnialiki?
Ujue nimewauliza hivyo makusudi ili nijue maana sitaki mnigeuze kama mchungaji nataka kila wakati mfeel kwamba nipo na ninyi muda wote, kila wakati  kila mahali kwenye biashara , kazi yako, mlima wa moto kwako.
Kwa sababu mimi niliwaambia kwamba nina nguvu nyingi za rohoni. MUNGU alifanya haya ili aone kama huwa mnanialika.
Sasa ukisema umenimisi haya aliyeko karmeli, mlima wa neema kubwa , je aliyeko nchi ya upendo nk?? Atafanyaje? Asemeje sasa yeye?
Na MUNGU aliruhusu  nisije ili ajue kama je mnaelewa au? Maana kila siku nilikuwa natoka nje, dereva anayeniendesha  anakuja kunichukua  lakini MUNGU ananiambia ngoja kidogo….. kwa hiyo nikawa narudi ndani yeye namwambia wasalimie.
Na yeye alivyokuwa mwaminifu  kila siku alikuwa anakuja  kunifuata , lakini MUNGU aliniambia nibaki.. leo ujue kwamba hakuna jambo linalotokea bila sababu.
Sasa muwe mnanialika , mkinialika wala hamtasikia kunimiss  ila mtaniona nikiwa nanyi si nilishawaambia mimi nina nguvu zangu za rohoni.
Wakili wa MUNGU; Amesema kwa kipindi hicho chote alikuwa anatuandalia zawadi ambayo atapewa kila mwenye haki kesho ibadani, japo MTENDAJI ameshawapa hiyo zawadi cha kufanya wewe uje na shilingi 2000 tu maana hata tungekuwa na mashine yetu tungechapisha kwa fedha.
Katika hiyo zawadi kutakuwa na swali juu ya moyo uliochorwa na MTENDAJI ubaoni na katika ile zawadi, utuambie kwa nini umechorwa hivyo na kwa nini upo hivyo una maana gani?
MUNGU ameng’oa ule mwiba ambao ulimchoma Paulo  uliokuwa unaendelea kusumbua kanisani. Mwiba ambao Paulo alipohitaji utolewe MUNGU alimwambia Neema yangu yakutosha leo anauondoa ndani ya Kanisa kwa wenye haki na makuhani.
Kushukuru MUNGU kwa ajili ya kuuondoa huo mwiba uliokuwa unaleta utaabishaji.
Sasa mwiba wa roho ni maneno magumu, matusi utukanwa, kudharauliwa mashitaka hivyo mwenye haki hataonewa tena, hataumizwa tena na kitu chochote tena, sitachomwa na mwiba milele.
Miiba yote MUNGU ameiondoa ndani yangu, unajua kila mmoja hapa nikimwangalia naona ana miiba mingi lakini leo nakuthibitishia MUNGU anaiondoa labda uing’ang’anie wewe mwenyewe.
Kitakachobakia ndani yangu sio miiba tena bali ni ile kweli ambayo imesimama leo.
Wapo wengi ambao hapa kanisani wamechomwa na miiba leo paza sauti yako …. Umshukuru MUNGU kwa sababu miiba imetoka.
Kizazi cha kwanza hadi cha 4 waliotumwa wote walikuwa wakichomwa miiba basi wanakosa amani furaha na haki pia, hivyo wanaowaongoza nao walikuwa wanakosa furaha ile miiba inawapata na kusababisha kizazi nacho kukosa amani.
Leo nashukuru kwa sababu hakuna litakalotokea likanichoma na mwiba.
Majira hii inapoenda kusimamisha kweli yanafutwa mabaya yote na uongo umefutwa milele.
Tumepata moyo wa MUNGU kweli nayo imepata mahali pa kukaa. Tangu majira zilizopita kweli haikuwahi kuwepo ila uongo ndio uliokuwepo.
Kilichokuwa kinaonekana majira zote zilizopita  ni uongo kila sehemu.
Sasa ni kweli moja iliyoko moyoni ndiyo itakayokuwa inaonekana kila sehemu.
Kila atakaeonekana anaongea uongo ataonekana na uumbaji wote kuwa ni kichaa. Sasa kweli iliyoko ndani itatoka nje.
Niliwahi kusoma Uholanzi kuna vitabu vya encyclopedia vinavyoonyesha kuwa muafrica ana mkia hadi ukawa unakatika kidogo kidogo….. kweli jamani muafrica  ana mkia? Si uongo huo.
Wakili;  Ndio maana hata mimi nilinyamaza kimya  … unajua ile katiba ya kanisa iliyoandikwa  walisema hiyo katiba imeandikwa na mmoja tu!
Sasa aliyetakiwa kunitetea na kusema kweli ndiye aliyekuwa wa kwanza kunishitaki.
Alikaa kimya kwa sababu hakuonekana ambaye anaweza kusema kweli, niliyetegemea atasema kweli ndiye aliyedanganya.
Ndio maana nilinyamaza kimya tu!  Maana kweli ya moyo haikupata kibali.
Na kweli ya moyo haikuwahi kusemwa ndio maana wengi  hawakuthubutu kusema  kweli maana hakukuwepo na aliyekuwa tayari kuisikiliza hiyo kweli.
Utasikia wanaosema hili kanisa nalo kwa kuvaa sale sio kuvaa sale kweli inasema vazi jeupe ni kutoka kwenye dhiki kuu ufunuo 7:13
Hivi hujawahi kusikia Rais akisema inawezekana  nikawa sio mwanasiasa mzuri kwa sababu ya kusema kweli.
Wazungu huwa wanasema muafrika ana akili fupi kama zilivyo nywele zake, je sasa hiyo ni kweli?
Kuna dada mmoja alienda America kuwaambia kwamba NABII WA MWISHO ametokea hapa Tanzania, walimuwasha kweli aliporudi akaenda kwa Nabii wa mwisho na kuanza kufoka … kumbe mmenidanganya ….
Na alipotokea MIAKA kuona nani anamfokea Nabii wa mwisho … akamuona huyo dada … ndipo aliposema na wewe MIAKA 1000 ndio muongo mkubwa unaaminika na madhabahuni lkn umesema uongo, ……
Sasa mbona wale wazungu wamesema nina kichaa…. Yote haya yalitokea kwa sababu kweli ilikuwa haijakubalika ndani ya uumbaji wote na haikuwa na mahali pa kukaa lakini leo kwa ibada ya leo kweli imepata pa kukaa na itajulikana kila mahali. Lakini sasa huyo dada yupo mjini huko na penzi nyanya.
Leo kweli imesimama wote watajua kwamba NABII WA MWISHO alitokea hapa, HEAD QUOTER ya MUNGU ni hapa, bustani ya ADEN+EDENI ni hapa, awe muasi, mmarekan, mhindi, muarabu nk wote watakuja hapa. 
There will be a highway from everywhere to here, uwe mzungu, mchina nk ni MTANZANIA.
DANIEL7:22 Kile Daniel alichokiona kwamba alimuona MZEE WA SIKU …. Sasa zile nyayo za MZEE WA SIKU zilionekana hapa.
Miaka 6 iliyopita kuna muisraeli mmoja alikuja ni rafiki mzuri tu wa KUHANI DAMU MOJA, alimwambia kuwa ameambiwa na MUNGU kuwa aje Tanzania maana inaonekana sanduku lipo Ethiopia lakini kilichopo ndani ya hilo sanduku kipo Tanzania.
Lakini hawajui ni wapi….. Damu moja aliponiambia nilimuuliza unafikiri hawajui mahali kilipo? Wanajua vizuri ndio sababu wanagombania mno hili jengo.
Lakini kweli iliyopo ndani ya YOSHUA 1:5 inasema  hakuna asimamae mbele yangu… ukiona bado kuna vinavyokuzuia mbele yako ujue kweli haipo ndani yako.
Marko 7:20-23 ni mpaka uwe na kweli ndani ya moyo wako.
Hawa walishindana wasijue kuwa wanashindana na MUNGU; farao alishindana na Musa, sisera alishindana na Debora, yezebeli alishindana na Eliya mtishibi, wasijue kuwa wanashindana na MUNGU.
Kuna walioshindana na Danieli , pia hamani hakujua kama anashindana na MUNGU.
Ile hali ya kuishiwa ni mwisho kweli imesimama ili wewe mwenye haki usipate shida tena, usigombane na kichwa kanisa ndani ya AGANO.
Waliomsingizia Yusufu na Daniel je walishinda? Hapana. Basi wote wanaokushitaki wanaokuzuia, wanaokuzinga, hawakuwezi  kama walivyoshindwa katika majira zote zilizopita basi wewe ni zaidi.
Wewe ni super maana kweli inayompendeza MUNGU  imesimama ndani yako.
ZABURI 37:25-26 Sijawahi kuona mwenye haki ameachwa, sijawahi kuona mtoto wa mwenye haki akiomba mkate barabarani.
Hata kama umekuja na nauli ya kukopa  tambua leo lazima ushiriki, sio lazima mimi nikupe kwa mkono, je unaamini kuwa leo lazima upokee!!!
Kila jambo baya ulilokuwa umekuja nalo linaishia hapa hapa kwa kuwa kweli moja imesimama.
Aidha Sadaka Maalumu iliyosimamishwa leo ni Kusimamisha kweli kila mahali na kwa sadaka hii majeshi yamesimama, mwenye haki hatakufa milele.
Kutubu kwa kuwa tulikuwa tunaona kinyume na MUNGU.
Niliona kufa tu, nikasema nimetoka mabonde kuinama hivyo siwezi kufanikiwa.
Sasa kufanikiwa ni lazima kwa kuwa  KWELI NI MUNGU na ndio inaniweka huru. Nilikuwa na hofu mashaka wasiwasi leo ni mwisho.
Mioyo hiyo ya hofu mlionayo,  nimeambiwa kuna wengine mlikuwa mnapiga simu ili kujua kama mimi ni mzima je nipo maana hamnioni.
Sadaka ya hakika ya kushinda katika maisha yangu yote ya ushindi, inafuta kuona kuangamizwa, majitu, madhaifu yanaungua, mioyo yote niliyokuwa  nayo zaidi ya moyo wako  yote yapo juu ya sadaka kuunguzwa yote milele.
Kwa sadaka; sifa za leo imenipa uponyaji, imekula maadui wote, imenipa mimi kuvuka moja kwa moja, sifa za leo zimekwisha kumaliza mabaya yote.
Wakili; “Mimi hata siku moja hutakaa uone nachukia milele. Je unajua faida na hasara za kuwa hapo?”
Mafanikio ya wenye haki yapo kwangu ninapochukia kizazi nacho kinaanguka majira hii kizazi hiki HAKITAANGUKA MILELE.
*RAMANI YA KANISA*
EZEKIEL28:16-18 Watu walijaza udhalimu ndani yako,…. moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako,…. umepatia unajisi…..nimetokeza moto…
Haya yote MUNGU alikuwa anamwambia mkamilifu ambaye baadaye alikuja kuasi.
Sasa leo macho yako uyaondoe hata kwa lazima sasa hivi umuone MUNGU anakufundisha ndiye yupo madhabahuni sasa hivi  usimuone MIAKA 1000 wala WAKILI WA MUNGU muone MUNGU sasa hivi ndiye anasema na wewe.
Moyo ulioinuka ndio moto ulitokeza ndani yake hivyo badala ya moyo kutoa chemichemi ya uzima MITHAL 4:23 ISAYA 12:3 moyo ulitoa oili chafu maji machafu badala ya maji masafi.
Badala ya kuwa Baraka ukawa najisi, badala ya uzima ukawa majivu. Je huwa hamuwazi kinyume na mema na MUNGU?
Sasa wengine ndio kabisa  huwa wanawaza kinyume na anayemfundisha alieko madhabahuni. Baada ya kuwaza kinyume utasikia…
Unakuta nikishafundisha hivi kuhani anaenda anadiscus anasema hili nitasema hili sitathubutu kusema wala kufundisha, ni kosa kwa kuhani anaeongoza kituo kujadili somo maaa saa unajadili tu moto unatokeza ndo unaosema hili nitasema hili ni la MIAKA sitasema…….
Leo MUNGU ataongea pasupasu kama ni neema na iwe neema, kwa nini ukubali kutupwa badala ya kutembea pazuri.
Sasa badala ya kumuona WAKILI ubarikiwe ukimuona unalaaniwa,  tubadilike.
Saa unapeleka taarifa za hasara kwa WAKILI kwambabiashara yako umefilisika.
Ni sawa na anayetoa maiti mochwari akampelekea, kuanzia leo hataki kuona wala kusikia anayefilisika anayeishiwa anayepata shida nk anataka kusikia una campuni kubwa viwanda mashamba makubwa
Kataa kituo cha kukaa na MUNGU halafu ukalaaniwa.
Hataki kusikia tena kuna anayeachika ,anayepata hasara KWA AMBAYE YUPO KITUONI KAMA NI KIDOGO AU KIKUBWA.
Badala ya kuwa na akiba njema anakuwa na akiba mbaya;  1SAMWEL 1:14-15  Hana kwa sababu ya kuomba kwa uchungu alionekana ni mlevi.
Ukishaonekana ni mlevi huwezi kujibiwa maombi au shukrani zako.
Pamoja na kwamba umeonewa basi usiweke akiba mbaya ndani ya moyo wako.
Tambua pamoja na wewe kutukanwa hakuna aliyewahi kutukanwa kama MUNGU alivyotukanwa.
sasa sijui utajielezaje mbele yake maana ametukanwa mno MUNGU.
Ujue kuna matusi mengine MUNGU anatukanwa mpaka kwenye magari kwa maandishi kabisa wameandika God is your self, 
Hili ni tusi kabisa, pale ngorongoro kuna wakati nilipita nikakuta watu wapo wengi wanaabudu mti halafu sasa huo mti afadhali hata ungekuwa mkubwa kama mbuyu lakini ni kadogo.
Je kweli akiba mbaya iendelee kukaa ndani ya moyo? Je tunaichukia akiba mbaya au hatuichukii? Tunakumbuka mabaya mno, ndani ya kanisa bado kuna wenye akiba mbaya tena ni wengi.
Je kama ningekuwa nasema kila nachoona nachofanyiwa yanayotokea tungevuka??, tungetoka? Tungeshinda?
Achana na kumbukumbu za uliyofanyiwa mbaya,
Pale ninapoona umevaa suti  halafu unataka kunikosesha ninakuona wewe ni KICHAA. Ili kizazi kisianguke na kizazi hiki hakitaanguka milele.
Sina tabia ya kuuliza mbona umenifanyia hivi, huwa sina livasi hata siku moja, kwa nini unapenda kukumbuka uliyofanyiwa jana juzi mpaka leo unayo leo tuache! Kwa nini unapeleka pua yako CHOONI kunusa????
Principle ya MUNGU kwa anayekukosha muone ni kichaa.
Kuanzia leo umuangalie, umsikilize WAKILI mara zote.
Kuna vitu MUNGU ameruhusu vitokee kabisa. Nataka kuona NENO linathibitika hapa  acha kusikiliza kukumbuka  mwalimu alivyokupiga shule ya msingi, ukoo walivyokutukana wanavyokutukana na walivyokuambia wanakutenga wewe sio ndugu yao.
Leo nataka uje hapa madhabahuni ushike madhabahu  uache kila kumbukumbu iliyokuwa inasumbua ndani yako.
Kila unayekutana yaani mimi nilivyofanyiwa…… Je wewe umekuwa inzi?  Maana inzi ndio ana tabia hiyo ya kufuata kuchukua kupenda kutamani kufurahia uchafu , vitu vibaya tu!!
Jamani muwasamehe vichwa wenu. Akikuambia leo toka mwambie nakupenda, akisema koma mwambie nakupenda, akisema huna kwenu nini mwambie nakupenda, akisema usinifuatefuate jibu lako liwe moja tu NAKUPENDA. Atabadilika tu.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo ya Majira na Nyakati Mtendaji wa Wakili wa MUNGU alifunua kuhusu HISIA ZA MOYO.
Alisema hisia za moyo ni yale tunayoyafanya [unayoyafanya] bila  kukaa chini na kuamua au kupanga mikakati. 
Unafanya pasipo kutegemea unajikuta unacheka, unatabasamu tu, una amani tu, una furaha tu, unaimba tu, unacheza tu.
Au unajikuta unalia mno, unakasirika unanuna tu wewe mwenyewe kumbe ni kutokana na hisia Fulani ulilolikumbuka ulilopitia vile vile inategemea una akiba gani ndani ya moyo yaani hisia yako uliyohisi chanzo chake ni nini inatokana na nini?
Hukupanga kucheka lakini unajikuta umecheka, hata kwenye gari daladala huimbi wakasikia lakini unajikuta unaimba moyo unaimba.
Unapika karamu upo ofisini unahudumia  unakuta unaimba hizi ni hisia za moyo.
Kuna furaha inayokaa ndani yako wewe mwenye haki, kwenye hisia kuna kitu kinaitwa faraha KUTOKA4:14. 
Akimuona tu atafurahi mwenyewe, nae MUNGU atakuwa  pamoja na kinywa cha Haruni na ndani ya kinywa cha Musa hivyo nitasemezana nanyi nanyi mtaelewa.
Kuna jambo kubwa la kutisha linaweza kutokea lakini unajikuta una furaha  au unaweza kupatwa na msiba lakini wewe hata ukijitahidi kulia  unajikuta kulia hakupo ndani yako.
Fuaraha inatoka kwenye moyo wenye akiba njema!!! Ukikutana na mwenye akiba mbaya huwezi kumfurahia hata ukilazimisha kumfurahia kumkumbatia unakuta tu hata moyo ndani unakataa kabisa!! Hisia ni kitu kinachotokea automatic.
Na ukikutana na kitu kibaya  hisia zako unajikuta zinabadilika.
WAKILI WA MUNGU, alipoingia kilichofanyika ni hisia za moyo wako hukupanga kumuona wa  lakini alipotokea tu ulivyomuona tu ukasikia kumfurahia, kumpokea na kumlaki hivyo ukamilifu wa somo kwamba umeelewa ndio huo hukupanga kucheka lakini umecheka umepata burudiko la moyo.
WAFILIPI 4:4-6  Furahini katika BWANA tena nasema furahini…. War 14:17  Maana ufalme wa MUNGU sio kula na kunywa bali ni haki amani na furaha.
Furaha ni hatua kubwa mno kwenye ufalme wa MUNGU.
Ukiwa na akiba ya MUNGU ndani yako unakuwa na furaha wakati wote.
Mahali  pa shida lakini wewe unakuwa na furaha, kuna tukio baya limetokea lakini wewe unakuwa na furaha tu!
Ukitaka ujue kuwa akiba njema imeingia ndani yako ni pale ambapo kuna jambo baya limetokea lakini unajisikia raha tu, ni mahali ambapo unatukanwa lakini unakuwa na furaha, ni wakati ambao  unapita mahali pagumu kwenye matatizo na taabu lakini unakuwa na furaha na huo ndio ufalme wa MUNGU.
Hakuna jambo linalotokea ukasikia kukwazika kukasirika kununa hasira manung’uniko malalamiko tena maana una akiba njema na hisia ya moyo ni njema.
Hatahivyo aliwagiza wenye haki wote kufanya toba ya kina ilikujitenga na kila akiba mbaya kwa kwenda kugusa madhabahu.
Aidha Wakili  wa MUNGU alihitimisha ibada hiyo kwa shukrani maalumu za kusimamisha majira na nyakati hiyo sambamba na kuinua ibada yasiku ya tano kwa vituo vyote vya Kanisa la MUNGU Aliyetuma wote.
Karibu usikilize ibada ya leo iliyobeba majeshi ya Majira na Nyakati iliyosimama leo
kufunuliwa kwa majira   nyakati za kupendezwa na kweli ilyomo moyoni Zab 51:6 ....……..

Friday, 27 January 2017


THAMANI NA FAIDA YA KUWA NA MOYO WENYE AKIBA NJEMA

MITHAL  4:23 linda sana moyo wako. ISAYA 57:15 MUNGU anakaa kwenye moyo uliotubu na kunyenyekea. Yer 29:11 Mawazo ya MUNGU ni mema kwetu siku zote.
Tunatakiwa tuwaze yaliyo mema kama MUNGU KRISTO na WAKILI wa MUNGU WALIVYO. ISAY14:13 Mawazo ya shetani kerubi ni mabaya siku zote.
EZEKIEL 28:17 Ukiwa na mawazo mabaya unakuwa na akiba mbaya ya moyo wako.
Moyo ndio unateketea  na vitu vyako moto unaotoka ndani yako ndio unaua kila unachokifanya.
Mt 7:20-23 Kilichoko ndani ya moyo wako ndicho kinachokupa kuonekana ulivyo, moyo wako ukiwa na akiba mbaya huwezi kuona umuhimu wa mwingine wala huwezi  kusifia au kukubali kazi ya mwingine.
LUKA 6:45 Mtu mwema katika akiba yake hutoa matunda mema na mwenye akiba mbaya hutoa matunda mabaya.
Leo tunamwambia MUNGU kama kuna chochote kibaya kinachotoka ndani  yangu kinachotokana na akiba mbaya ya moyo wangu ukiondoe.
Aidha leo tumetoa Sadaka Maalum ya kufuta akiba mbaya ndani ya Moyo wako, kwa wenye haki, na kwa kanisa.
Sadaka hii inasimamisha akiba njema ndani ya moyo wa kanisa na kwa mwenye haki mmoja mmoja.
Akiba mbaya ni hatari mno katika maisha yangu. Akiba mbaya ndani ya moyo ndio husababisha moto utoke ndani yako na kuangamiza maisha yako au familia yako au kazi zako.
Lakini pia Sadaka hii maalum inafuta kabisa akiba mbaya ndani ya wenye haki kwa kusimamisha nuru zaidi ya Isaya 45:7 ambapo MUNGU kwa uhalisi kabisa anaumba nuru na ana huluku kabisa giza ndani yetu.
*AKIBA MBAYA NI UCHAWI ULIOKO NDANI YAKO MWENYEWE.*

Unatakiwa usimwangalie mwenzio kuwa ni mchawi, mganga,  msengenyaji, ana tabia mbaya.
Yesu alisema usiangalie banzi lililopo ndani ya jicho la mwenzako wakati kwako kuna boriti, toa kwanza boroti ndani ya jicho lako ndipo ukalitoe banzi ndani ya jicho la mwenzako.
Moyo wenye akili mbili, Leo tunaenda kuona akili mbili ndani ya moyo. Akili zinakaa kwenye moyo, akili zipo zinazotokana na moyo wenye akiba njema.
Kuna akili zinazotokana akiba mbaya, na kuna akili zinazotokana na akiba njema ndani ya moyo.
Sasa kumbe akili zinatofautiana, kuna yale uliyosikia na uliyoyaona wewe mwenyewe  hayo hutengeneza store, hifadhi na akiba ndani ya moyo wako.
Unapowaza unawaza kile kilichopo ndani ya moyo wako na kilichoingizwa ndani ya akili yako.
KUMB 8:5 Nawe fikiri moyoni mwako, kufahamu una akiba gani ndani ya moyo wako/wake/wangu.
KUMB 8:2 Nawe utaikumbuka njia yako ambayo BWANA MUNGU wako alikupitisha ili ajue kilichoujaza moyo wako.
MUNGU alikuacha uone njaa, kiu, shida, taabu, aibu ikupate akuone umejaza nini ndani ya moyo wako.
MUNGU anakupima kwa kipimo chake kimoja cha moyo (tester).
Anakuacha ulale na njaa, kuna wakati unawasha mpaka shukrani unaikataa njaa na unasema njaa imefutwa kwa wenye haki kumbe MUNGU ndiye aliyeweka hiyo njaa ndani yako.
Anafanya hayo yote aone kama utaendelea kushika njia zake au utaacha.
MUNGU hawezi kukuacha huru mpaka akupime kwanza aone kama unaendelea kumpenda au umepata wengine wa kuwapenda.
Kumbe kuna majira ambayo MUNGU anakutest moyo wako. Kuna  testa ya akiba njema na akiba mbaya.
Anakutesti kwa njaa au kwa namna yoyote apendavyo MUNGU.
MUNGU anajaribu moyo sababu yeye siku zote huangalia moyo.
MUNGU anakutweza kwa njia yoyote ile ili aone moyo wako.
KUTOKA 14:1- MUNGU aliwajaribu wana wa Israel hata wakae miaka 40.
Hata kipindi cha miezi 6 wapo waliolaumu kwa kuwa MUNGU alikuwa anatupitisha kwa kututweza ili aone, Je unampenda au ndani ya mioyo yetu kuna akiba njema?
Israeli walijaribiwa na MUNGU  kidogo tu pasipo kujua kwa ni MUNGU anawajaribu maneno yaliwatoka, malalamiko, manung’uniko, mpaka wakakumbuka nyama, wali,  pilau na vituguu saumu vya kwa farao.
Kuna saa MUNGU anaruhusu jambo lolote likupate ili aone, Je moyoni mwako kuna nini kimeujaza moyo wako? kwa kuwa kila mmoja huyanena yaujazayo moyo wake.
Walimlaumu Musa mpaka wakasema Yupo nje ya reli  nini mbona tunaona mambo yamezidi, mafunuo yamezidi “as if” utafikiri wao wanaijua hiyo njia.
Maswali ya malaumu kibao wengine wakasema kapotea, mbona tunaomba MUNGU hajibu kumbe wapo kwenye examination na wamekutwa na akiba mbaya ndani ya moyo.
Unamuwazia jambo baya mwingine hata hayupo ila sababu moyo wako umekaa kujihesabia haki tu huoni kama unakosea leo tutubu na tuache.
Leo MUNGU unaona amekuja kuondoa akiba mbaya ujue kwamba  ina maana kwamba kanisa tumeshavuka tayari.
Je unapoona unatoka Madhabahuni au kazini ukakuta vyombo vyote vimetolewa nje na mwenye nyumba kashaweka kufuli lake huku anasema sifungui bila hela yangu  ule wimbo wa naona memaa… unakuja kweli au kitu kipi kinatokea?
Kanisa unakuta kichwa wako yuko na kahaba na hashituki anaendelea tu na mabusu hivi unakuja ule wimbo wa naona memaa….
Leo tujifunze kwa Wakili wa MUNGU;  7abibu 6 alikujaa na gitaa akasema leo ni siku ya kuimba kucheza kuruka maana wengi walisema siku hiyo ni Judgementday wakiimba na kucheza……
Yoh 21:13 Habari za kutwezwa zilimpata Petro akaamua kurudi kuvua samaki. Petro alifanya hivyo kwakuwa alikuwa na akiba ya kuvua samaki.
Ilibidi aondoe akiba yote ndani yake abaki na akiba ya MUNGU tu!!
ISAYA 49:15 MUNGU amesema mwanamke hawezi kumsahau mwanae, Lakini  MUNGU hata akikutweza hawezi kukusahau.
Kwa hiyo ramani ya kanisa MUNGU aliijua tangu zamani kuwa siku ya leo tutafika hapa kwa kuwa  alituchora kwenye vitanga vya mikono yake.
MUNGU alijua leo utavaa vazi ulilovaa leo, utawaza unayoyawaza, utakaa ulipokaa leo na utaelewa somo kwa viwango ulivyoelewa kutokana na akiba ya ndani ya moyo wako ikoje ni ipi.
Unapokanyagwa ni makusudi ili tuone moyo uliokuwa nao yaani MUNGU karuhusu kabisa!!!
Leo ukipata mtihani unatakiwa umshukuru MUNGU.
MUNGU kuna wengine aliwafanya wawe akina farao ili tuwe imara katika imani.
Kwa hiyo  kizazi hiki hatuna majaribu bali tuna mtihani.
[A] Uwe na msamaha kila wakati. Usikumbuke yaliyopita, uwe mwepesi wa kuachilia na kusahau haraka.
Usiamke nalo na ukafika nalo wajibu ukashinda nalo ukarudi nalo huo sio moyo wa MUNGU.
Katika moyo wa MUNGU ni kuwa  na msamaha 1Sam 1:12 Unatakiwa kusamehe kuachilia na kusahau yote.
*UKIWA NA AKIBA MBAYA WATU HAWAKUONI VILE UNAVYOJIONA KWENYE KIOO.*
Hana alikuwa akiomba lakini akiwa hajasamehe wala kuachilia hivyo mbele za MUNGU alionekana ni mlevi wa kutisha.
Ukiwa na akiba mbaya ndani ya moyo wako kila unachokifanya  chochote kinakufa pia unaonekana kitu kisichofaa.
Utakuta mwalimu ametoa swali 1+1 na umeweka jibu 2 lakini akisahihisha akaweka kosa sio kwamba kakosea yeye kaona 4 kutokana na akiba ya moyo wako. Leo tubadilike MUNGU ametuvumilia mno.
Kuna mahali unatembea unajiona binti mrembo mzuri kumbe wote unaokutana nao unaoonana nao wanakuona wewe ni kijana au babu au bibi nk. Sura yako imerejea leo.
Moyo ndio huwa unapika, kichwa wako anaposema chakula ulichopika ni kibaya ni kwa sababu ya moyo wako ulioubeba.
Kila siku anakuambia upike kama Fulani ni moyo wala sio kwamba huyo Fulani ni hawala wake hapana, leo badilika.
Unapika huku unaongea sana karamu huwa mbaya,  pika karamu kwa toba shukrani na imba na kucheza uone kama hajafurahia karamu yako.
Ukimpa shamba mwenye akiba mbaya mazao yote yanaoza, ukiuza dukani duka lote linafilisika na hajaiba na mahesabu yapo vizuri, ukimpa kitu wote wanakufa na wengine anawala yeye mwenyewe kituo hakiongezeki.
Moyo wenye akiba mbaya ni moyo usiozaa, ukiomba nao mito ya shukrani inakufa, ukimpa mwenye haki amlee anamuua, ukifanya nae biashara inakufa, hata ukimpa bilioni tilioni zote zinaisha zote bila kufanya chochote cha maana.
[B] Kibali, kiwango cha kibali unachokuwanacho kinatokana akiba ya moyo wako. Kiwango cha akiba njema ilioko ndani yako Zab 119:1-
[C] Kumcha BWANA  ukiwa na akiba njema moyoni mwako ndipo unaweza kumcha BWANA.
[D] Nguvu ya kutamka jambo likatokea, Kung’oka kwa mlima mbele yako kunatokana na akiba iliyoujaza moyo wako MARKO 11:23
[E]  Hakika ya NENO, War 10:9-10 Kwa kadri ulivyokuwa na hakika iliyojaa ndani ya moyo wako  hukiri na kupokea yale uliyokusudia kupokea. 
Isaya 55:11 MUNGU anasema kuwa kama mvua isivyorudi juu mawinguni ndivyo NENO analolituma kwangu lilivyo kwamba lazima litimizwe sawa na kusudi lake, halirudi bure.
Aidha tumeshiriki Karamu ya Akiba njema ambayo ni Sheria ya Roho wa Uzima.
MWAMBIE MCHUNGAJI MWEMA AKUPE AKILI YAKE ISIYOKUWA NA PANDE MBILI !!!!!

AKIBA NJEMA NI IPI NA AKIBA MBAYA NI IPI?? MITHALI 4:23

Kusimamisha akiba njema ya moyo inayofuta akiba mbaya zote ndani yaa moyo. Moyo una pande mbili.
Kuna chumba kinachohifadhi akiba njema na kingine kinahifadhi akiba mbaya. Tumepewa Moyo halisi ingawa haya yako kwenye Moyo mmoja.
Chemichemi ya uzima inatoka  kwenye moyo wenye akiba njema. Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo.
Moyo ni store na ni hifadhi ya wanyama wadudu na ndege, majoka pundamilia.
Huu moyo unahifadhi mabaya na mazuri kwa wakati mmoja na ninao moyo mmoja.
LUKA2:18-19  wote waliyasikia maneno hayo lkn mariamu aliyahifadhi moyoni mwake maneno yale.
LUKA 6:45 Mtu mwema katika hazina ya moyo wake hutoa yalio mema ktk moyo wake.
Kadhalika mtu mwenye hazina mbaya katika  moyo wake hutoa mabaya katika moyo wake.
Yote haya yanatokana na kiwango chako cha yale uliyo yasikia na kuyaona.
Maana kila uliyoyasikia yanakaa katika moyo.
Kuna mambo ambayo uliyakokota tangu ukiwa tumboni mwa mama yako tokea siku uliyotungwa mimba kuna uliyoyakuta na yakaendelea kuwepo hapo yakiongezeka kila siku mpaka siku unazaliwa.
Ukiwa tumboni mwa mama yako  kuna ambayo ulikuwa unayasikia yalemama yako anatendewa hata ukayaweka ndani ya moyo wako kwa kuwa moyo ndio hifadhi ya kila ulichosikia na kukiona.
Hii ndio sababu ukizaliwa tu lazima ulie kutokana na yale unayoyajua kuwa yapo ndani ya mji unaouendea.
Kila anachopatwa mama na wewe unapatwa hukohuko tumboni ; mfano, mama akiumwa na wewe unaumwa, akiongea mabaya, akitukana akisengenya, akipigwa, malalamiko, manung’uniko.
Kuna mwingine tokea mimba alichukiwa akakataliwa na baba ukiuliza kwa nini anakuambia ilikuwa si majira niliyokuwa nimepanga kupata mtoto, amenivurugia mipango yangu.
Hivyo mpaka siku akizaliwa mtoto anajua kuwa baba hanipendi  wala hawezi kupatana au mama hanipendi, mama hata kunyonyesha ananyonyesha tu huku akisema sina jinsi ndio hivyo kashazaliwa.
Kuna mjomba, shangazi, babu, bibi walimchukia mama akiwa amebeba mimba au ujawepesi angu hivyo hata nikizaliwa siwezi kupatana nao automatically pasipo hata kuambiwa yaliyowahi tokea nyuma,
Hata wakijifanya kukupenda taa nyekundu inawaka ikisema hawakupendi hawa tokea ukiwa tumboni mwa mama yako.
Pia kuna wanaozaliwa na uchungu na kukataliwa huu ni msingi uliokutana nao ukiwa tumboni uliotangulia.
ZABURI 11:3  Kama msingi ukiharibika mwenye haki atafanya nini? Kwa kuwa tangu zamani ukiwa tumboni mwa mama yako ndiko msingi wako ulianzia halafu ukaharibika, Je ukikua utafanya nini?
Je chumba cha moyo wako kinahifadhi gani? Kuna wenye chumba cha mataarifa ya kusikia, mataarifa ya namfahamu huyu vizuri hadi kwao na tabia zao.
Wengine wengi nafsi zao zimekuwa kama gari la taka, mavi linavuta mitaro.
Kiwango unacholinda moyo wako usiingiwe na mambo mabaya ndicho kiwango cha akiba njema kilichoko ndani yako.
Nafsi ya mtu haili itakula jeuri yake. MITHALI 13:2- Kila mtu atakula matunda ya kinywa chake, kwa kuwa kinywa hunena yaujazayo moyo wake.
MARKO 7:20-23 Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi, maana midomo ya mtu hutoa unajisi matusi ujinga na upumbavu lugha mbaya tu!
EZEKIEL 28:17-18 Nimetokeza moto ndani yako nao umekuteketeza umekuwa majivu najisi kitu kisichofaa.
Moto uliokula biashara yako, kazi, agano lako, nk ni moto ulioko ndani yako wewe wenyewe.
Moto ulioko ndani yako ulioutengeneza kwa chuki  jeuri nk ndio unaosababisha ukwazike, unaovuruga agano lako, unakufarakanisha na kichwa wako, ndio uliokufikisha hapo ulipo wewe katika kila eneo.
Moto uliotokeza ni ile akiba ya ndani ya moyo wako, kile ulichokijaza kwenye moyo  kama kinatokana na maneno au NENO.
Kama una akiba njema  basi utakuwa na mema tu!! Kama ilikuwa akiba mbaya ndani ya moyo basi utakuwa na mabaya tu.
Store ya mambo mabaya akiba mbaya ni moyo wako wewe mwenyewe hiyo ndio imekuteketeza hata huwezi kuwaachilia wengine huwezi kuwatoa ndani ya moyo wako huwezi kuwasamehe na kusahau;
Ndio imekufanya kuwa majivu najisi na kitu kisichofaa, kitu kibaya, ukifanya kazi unajiona house girl, maswali maswali ya kwa nini mimi tu?
Akiba mbaya ndio inakufanya uone unanyanyaswa na kichwa wako, hata kama unaambiwa kweli unaona unadharauliwa, huheshimiwi, kumbe limoyo lako wewe mwenyewe, unasema kila siku unanikwaza kitu kidogo tu hasira umefurai yanakutoka kama umemeza betri leo hama kituo hicho.
Kazi ya akiba mbaya ni kutoboa madirisha kwenye moyo wako ili aje akuibie:-  
+nguvu,
+Uweza,
+Baraka,
+hekima,
+heshima,
+utukufu na                                                               +utajiri.
Akiba mbaya analeta ukimwi kisukari ili ujue kama ni akiba mbaya utasikia doctor anasema usiwaze sana, usipaniki, usikasirike kasirike, usikwazike, manung’iniko yote haya husababishwa na akiba myaya ndani ya moyo.
Kwa hiyo ujue akiba ya MOYO wako ndio inayokupa maisha ya kuishi. Akiba mbaya hufungua milango ya mabaya na kukuletea mauti.
Huleta magonjwa, ukiwa na vidonda vya tumbo ujue una akiba mbaya ya moyo wako. *DALILI ZA AKIBA MBAYA;*
#Magoti kulegea,
#mabega kuchoka,
#mgongo kuuma, 
#kiuno kuuma,
#miguu kuwaka,
#kujisikia kununa saa zote,
#vidonda vya tumbo,
#kukosa hamu ya kula kitu chochote,
#kutokuwa na amani wakati wote,
#macho kupungua nguvu ya kuona,
#kukosa usingizi au kusinzia sana,
#kutembea huku unaongea peke yako mwenyewe mpaka unaamua mwenyewe,
#kupenda kujieleza sana .
#Kutojiamini ,
#hisia mbaya kila anayeongea anakusema wewe,
#kukosa furaha saa zote,
#hata ukivaa hupendezi, #hakuna hata siku moja ambayo unambiwa umependeza, #unafilisika tu huongezeki, #unaharibu mahusiano yako na MUNGU na unakufarakanisha na kuoa kuolewa fedha, kazi,
Inakula mifupa ,
#ndio unaokuchafua, unaokutaabisha, unamuangamiza, unakushusha chini, unakufedhehesha, unakukosesha na kazi nzuri,
#kila unachoongea ni kibaya.
Je hujawahi kuona mwenye diploma anapata kazi nzuri lakini mwenye digrii mfagiaji tena anapewa kufagia nje? Sababu ni moyo.
Badala yakuwa na moyo wenye kutoa chemichemi ya mambo mazuri unakuwa ya kutoa mabaya.
Dalili hizo ni pamoja na; uso wake hukunjamana ,kuwa na hasira saa zote, ana maswali yasiyo na majibu, kuwa na hofo, woga hata kupanda pikipiki tu utakikia anaogopa kufa, kuota ndoto za kufukuzwa na wanyama, kutomwamini mwingine.
Kutokuwa na moyo wa shukrani, kutokuwa na furaha hata ufanyiwe nini,huoni mema kwa wenzako yote ni mabaya tu, hata uimbe vipi naona mema aa naona mazuri tu ….. akiba mbaya anakuzomea maana anajua unadanganya kupritent!
Hupati tenda kwa sababu ya moyo wako… unapoandika application sio yale maandishi yanayokua kazi tenda tena bosi anaposoma hasomi lile karatasi bali anasoma moyo wako ndio sababu hupati unachotaka.
Unapaka cream ili uonekane mzuri, kuwa na machunusi usoni, ngozi inakubabuka, umeoauka  midomo inakauka na kupasuka.
Ni mkali cku zote kitu kidogo tu anashikilia bango, akitembea utasema ni mnyenyekevu kumbe amejaa akiba mbaya tu!
Kila unachofanya ili kipate kibali au kikose kibali ni kutokana na akiba uliyonayo.
Kuna moto unaotoka ndani  ya kila mmoja unasababisha uwe kitu kisichofaa mbele za MUNGU na mbele za wengine.
Leo kila tabia uliokuwa nayo au moyo uliokuwa nao wenye akiba mbaya unatolewa.
MAMBO YANAYOSABABISHA AKIBA MBAYA;
*Kufukuzwa kazi kwa kuonewa kwa ghafla,
*kuna jambo ulilolitarajia likachelewa kutokea,
*kuna majibu mazuri uliyoyategemea yakajibiwa vibaya,
*kuna matokeo mazuri uliyategemea yakaja kinyume visivyo,
*kuna uliyemtegemea akakuacha kwa ghafla,
*uliyemuamini sana akakuasi,
*akakugeuka, akakusaliti,
*akakutenda ubaya,
*ulitenda mema ukalipwa mabaya,
*kufiwa ghafla na uliyempenda,
*aliyekupenda,
*uliyemwamini,
*ukamwamini,
*Tendo au matendo uliyowahi kufanyiwa ukatili,
*kubakwa kulazimishwa kufanya mabaya,
*kuugua kwa muda mrefu,
*kuuguza kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa halafu asipone akafa,
*kupita mahali pagumu kukosa fedha,
*kusalitiwa na uliowaamini,
*waliokuwa karibu na wewe.
*na mambo mengine hayo yote yanayoleta kuwa na akiba mbaya ndani ya moyo  wako.
*Aidha kuna madeni yasiyolipika ,
*kudaiwa kwa vurugu mfululizo.
*Kesi za kusingiziwa,
*kusingiziwa umezini,
*unaiba na uchawi hizi ndizo kesi ambazo huleta shida mara nyingi pia huleta akiba mbaya.
*Na wengine huchukua uamuzi mbaya mno, hatua mbaya.
Tunatakiwa tuwe na moyo wenye akiba njema pekee.
Homework ; kila mmoja kuanzia leo akutane na mwenzake au kuhani ili ufunguliwe ili kuondoa akiba mbaya zote ndani ya moyo kwa siku saba. Pia katika wiki hii hutakiwi kukosa ibada za majibu.
CHUNGAJI MMOJA LEO AMETUKUTA NA AKIBA MBAYA KILA MMOJA AONDOE ILI APATE  PA KUKAA.
POINT: EZEKIEL 28:18{b}

Wednesday, 25 January 2017


SIKU 7 ZA KUKABIDHI MOYO MMOJA HALISI KWA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE

Kushukuru MUNGU kwa ajili ya mwezi tammuzi uliotupa moyo mmoja halisi. 
Moyo  ambao umetupa Kweli Halisi inayotupa kuishi na MUNGU na inatupa kuchungwa na Mchungaji mmoja Halisi.
SADAKA; Kufuta chochote chochote kilichokuwa kimekaa  kwenye moyo wangu na kuondolewa ngani yangu, Kanisa kwa wenye haki na kila kinachoitwa kwa jina langu.
ZABURI27:4 Sadaka hii inanipa mimi kukaa kwenye Neno sawa na ninavyofundishwa kwa uzuri wa MUNGU, Nifurahie na kutafakari  ambayo MUNGU ametenda kwetu Kanisa.
Mwezi wa tammuzi tumepewa Moyo mmoja Halisi, MUNGU anachoangalia ni Moyo wake ndani yangu, Moyo ambao ndani yake hakikai wala hakai yeyote zaidi ya MUNGU peke yake.
Ukiweka kilimo ndani ya Moyo, siku ya kupanda  unasema napanda kwangu kwanza kwa MUNGU baadae.
Huu sio moyo mmoja unatakiwa kumuweka MUNGU kuwa namba moja   kwako.
Hakikisha hufanyi chochote kilicho chako kabla kufanya kwa MUNGU.
Na sasa unatakiwa ujenge tabia ya kujenga au kupanda kwanza kwa MUNGU kabla yako.
Ifike mahali  pa kusema MUNGU kwanza vitu vingine baadae.
Unatakiwa uwe na Moyo mmoja Halisi sio mioyo mingi, mioyo ya vitu vingine ndani yako.
Matendo13:22 WAKILI WA MUNGU siku zote anatenda anafanya yaliyo mapenzi ya MUNGU peke yake.
Tunaona hata kizazi cha pili Daudi aliyatenda mapenzi ya MUNGU.
Leo mimi mwenye haki ndiye ninayetakiwa kuyatenda mapenzi ya MUNGU ndani ya kizazi chake.
ZABURI 89:1- Ni Daudi peke yake ambaye MUNGU amesema kuwa kiti chake kitakuwa cha MUNGU kwa kuwa aliyatenda mapenzi ya MUNGU kwa sababu ya Moyo mmoja ndani yake.
Kiti kuthibitika, Moyo wa MUNGU unakupa kushinda  kama WAKILI wa MUNGU alivyoshinda na zaidi ya kushinda.
KUMB5:29 Laiti wangekuwa na Moyo kama huu siku zote wa kunicha wangefanikiwa wao na watoto wao yaani [uzao] MUNGU anasema ukiwa na Moyo wake ndani yako utafanikiwa.
Kinachozaa ni Moyo kwa hiyo usipokuwa na Moyo wa MUNGU unazaa mambo ya Moyo ulionao sawa na ulivyopanda  utavuna hivyo hivyo.
Math12:33-35 ili uzae lazima uwe na Moyo wa MUNGU unaozaa vitu vizuri.
Hata ukisema tasa ni Moyo wako ndio tasa lakini kizazi chako ni kizuri ila kwa sababu Moyo ni chanzo cha vitu vizuri kama haupo vizuri huwezi kupata mtoto.
Madoctor utakuta wanahangaika na pracenter akijua ndio tatizo lilipo kumbe tatizo lipo kwenye moyo wake mwenyewe maana kinachozaa ni moyo sio pracenter.
VITU VINAVYOKAA KWENYE MOYO:- Moyo umebeba yafuatayo;-
#Nguvu ya udhihirisho,
#Nyota ya mambo mazuri [MAFANIKIO].
#Moyo ni mtawala wa vitu vyote.
#Ndani ya huu moyo wenye vitu vizuri anahitajika akae  MUNGU peke  yake.
Katika NYOTA KUNA;-
*nguvu,
*hekima,
*Baraka,
*utukufu,
*heshima,
*uweza,
*utajiri.
Moyo ukiibiwa ujue vitu vyote hivyo utavipoteza.
Pia jua kwamba akija mwingine kukaa ndani ya moyo vitu vyote vinakimbia hata ulivyokuwa umeahidiwa hupewi tena.
Ndio sababu MUNGU anasema linda sana moyo wako kuliko vitu vyote uvilindavyo Mith 4:23.
ZABURI32:1- Neno linasema heri aliyesitiriwa dhambi zake yaani heri anayesamehewa dhambi, Daudi alieleza moyo wake jinsi usivyomficha MUNGU. 
Wenye haki hatutakiwi kuruhusu moyo kubeba uchafu ndani yetu, siku zote tutafakari ukuu wa MUNGU.
1nyakat29: Daudi alikuwa ni mtoaji kwa viwango visivyo vya kawaida, sadaka alizokuwa anatoa zilikuwa zinaonyesha moyo wa MUNGU ndani  yake.

MUNGU anataka kila mmoja awe na huo moyo wa MUNGU ndani yake.
Kila kitu unachofanya ufanye kwa ajili ya MUNGU kama WAKILI WA MUNGU anavyofanya. Tujifunze kwa mtini .
WAKILI wa MUNGU hakuwahi kumtolea MUNGU kitu kinyonge, je sisi tunatoa wapi?
Tunatoa vitu vingine hata sisi wenyewe tukipewa haturidhiki na hata tukipata wengine tunavitupa au kugawa kwa wengine, leo tubadilike.
Leo unatakiwa uondoe chochote kinachosababisha usimuabudu MUNGU kwa Roho na Kweli.
Unapoona Kichwa,  Kanisa, watoto, biashara, shamba, nyumba  anasababisha usije hata ibada za majibu usimtolee  MUNGU ujue vipo ndani ya moyo wako leo uwaondoe na uviondoe ukatae kabisa.
Jikague kuna mahali unajikuta unaongea maneno mengi badala ya NENO ujue kuwa ni kwa sababu ya walioko ndani ya moyo wako .
Kuna ambao mko hapa lakini kuna jambo ndani ya mioyo ambalo halitoki ili MUNGU akae leo kubali wewe mwenyewe likatae na uyakatae yote uliyowahi kufanyiwa  ambayo mpaka leo ukilikumbuka hata MUNGU Kristo Wakili wa MUNGU unawaambia wakae pembeni kwanza leo kubali kulitoa ili MUNGU akae ndani yako.
MUNGU anaangalia moyo kitu gani ukiguswa unalalamika unanung’unika unakwazika unanuna unakasirika unafura?
je ni fedha, mahali pa juu pa cheo kazi umri fedha kichwa kanisa watoto.
Hivyo kwa sababu wote tumekubali tumekiri kuwa kuna kitu tukiguswa ndani yetu tunashindwa kuvumilia basi yatupasa kutubu.
Leo tunatakiwa tutoe kila kitu kilichokuwa kimebaki ndani yangu/ yako / yetu badala ya Moyo mmoja wa MUNGU.
*MCHUNGAJI MMOJA ANAKAA KWENYE MOYO WENYE AKIBA NJEMA*

Tuesday, 24 January 2017


*KWELI IMESIMAMA    KWA UHALISI*

Tunashukuru MUNGU kwa sababu sasa Kweli imesimama kwa uhalisi. Kweli ilipotoshwa tangu UF12:1 alipo wa na Kanisa akatokea mwanamke [photocopy].
Tangu mlimani na vizazi vyote vinne kweli ilikataliwa kulikuwa na uongo na alifutwa jana. Mbinu za uovu zilizokuwa zinasumbua wenye haki  zimefutwa.
Tangu siku ya kwanza MUNGU alipoumba mbingu na nchi na kisha kuwakabidhi shamba wakulima kweli haikukubaliwa ilikataliwa.
YOHANA 19:1-20 PILATO alikubali kwa sababu kweli haikuwepo. Damu ya kweli kufuta uongo na ukweli.
Shinikizo limesababisha wengine watoke mahali pao.
Kuna waliofukuzwa kwenye agano lao, leo kiapo kimesimama; kuvunjwa kwa agano la kwa uongo.
Yeyote aliyekuwa anachukua nafsi za wenye haki na kuzitumia kinyume leo ndio mwisho wake.
*MBINU 3 WANAZOTUMIA MASHETANI*
Kwa nini mwenye haki anaadhibiwa?
1.)Muovu kuingia ndani ya nafsi ya mwenye haki na kutenda dhambi.
V Unajikuta unafanya kitu cha ajabu mpaka wewe mwenyewe unajishitukia unajishangaa kwa yale unayoyafanya.
Kuna wakati unajikuta unajiuliza maswali kwamba hivi ni mimi ninayefanya haya yote kumbe ni kutokana na Yule muovu aliyeingia kwenye nafsi yako.
Hali hii ya muovu kuingia ndani ya mwenye haki na kutenda mabaya kinyume na MUNGU kinyume  na Neno ni mwisho.
2.)Muovu kuingia ndani ya bosi wako , mzazi, mlezi, mwanao nk ili kuharibu uhusiano mzuri uliokuwepo kati yenu leo ni mwisho.
Unakuta bosi wako kwa ghafla kabadilika mpaka anatamani akufukuze kazi na wakati mwingine unajikuta unatamani usaini kuacha kazi kumbe ni adui leo ni mwisho.
Mlima wa moto unakutana na watoto ukiwaambia msifanye msiangalie tivi kabla ya kupika unakuta wameangalia mpaka wameunguza karamu.
Kijana, binti unajikuta mzazi wako kila ukipika anakuambia karamu gani hii umepika mbaya namna hii na amekula amemaliza kushiriki leo njia zote za adui kuharibu uhusiano mzuri na madhabahu yake imefutwa milele.
3.)Kuvalishwa mavazi mabaya ya waliokufa, uchawi, uganga, uloz, unajimu, hasara, kudharauliwa, leo yamefutwa.
Haya mavazi yalisababisha hata ukisema kweli ikataliwe leo ni mwisho.
Leo ukisema  kweli na kuonekana kuwa ni mchawi ni mwisho.
Wakili wa MUNGU anapokupa vazi lake ujue kwanza umepokea mafuta yake.
Hii nguvu wachawi walichukua na kuligeuza wenye haki kuonekana wachawi waovu leo mwisho. YOHANA 8:1-
Tabia ya kutafuta kumuua WAKILI WA MUNGU kila siku ni kwa sababu  NENO LA MUNGU halikuwepo halipo ndani yao.
Utasikia sisi ni wa Ibrahimu, Eliya mtishibi, Yesu, Eiya Ad2 lakini wanayofanya hayafanani nao ambao wanawasema ndio sababu Yesu mwasema ninyi ni wa baba yenu Ibrahimu;
Mbona mnayotenda hayafanani na huyo Ibrahimu, Eliya Ad2 maana hata wao wangekuwepo wasingefanya hayo mnayoyafanya leo kwa Wakili wa MUNGU.
Hata wakati wanaongoza vizazi hawakuwahi kumshitaki yeyote, hawakumtukana yeyote, hawakumkosoa MUNGU milele. Nyie mmetoa wapi?
Aliye wa MUNGU husikia na kuyajua yaliyo ya MUNGU na kuyelewa sasa mbona WAKILI WA MUNGU anasema yaliyo ya MUNGU lakini hamuelewi, mnamshitaki  MUNGU.
Ukisoma haya mazungumzo yaliyopo yohana 8 utajua kuwa kweli ilikataliwa siku zote hizo.
Hawataki kweli utasikia wanasema WAKILI tunampenda lakini mafundisho yake hatuyataki tunayataka yale ya baba yetu Ibrahimu,
Eliya Ad2, kizazi cha tatu walikataa mafundisho ya Yesu wakataka ya Ibrahimu yaani mafundisho ya kabla hata ya majira ya 3 ya kizazi cha 1.
YOHANA 19:1-20 Pilato naye hakuijua kweli japo alitamani alipenda kumtetea YESU ktk majira ile lakini haikuwezekana kutokana na kutoikubali kweli.
Kanisa tuna haja ya kumuomba MUNGU kweli kweli ili Pilato ajue kweli na aikubali. Leo tunaipeleka kweli kwa pilato.
Mpaka sasa serikali haina shida na kanisa na WAKILI WA MUNGU shida ipo kwa wale wanaopeleka taarifa za uongo, barua za masingizio, mashitaka ya uongo, michoro ya mabaya, ramani mbaya  leo tutubu.
Leo kwa sababu kweli imesimama mashitaka yote yamefutwa kwetu milele.
Mashitaka ambayo MUNGU, Kristo Wakili wa MUNGU Kanisa na Taifa wameshitakiwa leo yamefutwa milele.
Nira zote kamba zote zilizokuwa zimetufunga leo zimefutwa milele. Kizazi hiki pilato lazima aijue kweli ili mashitaka yote yaondolewe kwa YESU.
Maagano ya kichwa kanisa yaliyo haribiwa na kahaba leo yamerejea kwenye kusudi kwa sababu kweli imesimama leo.
Kesi za masingizio zimefutwa ila kama ulikuwa na machungwa ya watu kweli nenda ukaseme kweli kwa kuwa kweli imesimama yenye kukuweka huru. Vifungo vyote vimeng’olewa milele.
Roho za masingizio zimefutwa, kuanzia leo utaaminiwa kila akuonae ataona wema wako ulioutenda, uadilifu wako utaonekana, ukifanya kazi utalipwa kwa haki maana kwa kuwa sasa kila utakapofanya kazi utakapoonekana utakuwa KEKI kwenye wajibu wako mlima wa moto, biashara zako.
Kila kazi unayofanya ulikuwa unadharauliwa kuanzia leo utathaminiwa.
Sasa kama ulifanya biashara lakini ikakataliwa leo kaianzishe tena utafanikiwa itakubalika itapendwa itakimbiliwa utaitwa kwenye tenda mbalimbali.
SADAKA maalumu ya leo ni kufutwa kwa mavazi ya mambo mabaya yote, kutokuwa na thamani katika kila kitu unachofanya.
Kusimamisha Kweli ili kuunguza mavazi ya maneno mabaya yote kwa sadaka hiyo.
Pia Sadaka hiyo maalumu inafuta usingiziaji kwa maneno yote ya uongo na mavazi ya usingiziaji kwa wenye haki. 
Kufuta laana zisizo na sababu, kituo cha kufanya kazi kubwa bila malipo.
Mashitaka yaliyokuwa yamepelekwa kwa pilato yamefutwa.
Uongo uliokuwa umeenezwa kwa ajili ya Kanisa umefutwa kwa sadaka. Pilato + kaisari wataijua kweli kwa sadaka hii.
Mavazi aliyokuwa amevalishwa pilato asiijue kweli leo yameuungua yamefutwa kwa sadaka sasa ataijua kweli moja halisi.
*MCHUNGAJI MMOJA MWEMA NA AKUKUTE KWENYE KWELI SASA ILI APATE KUKUCHUNGA.*

Monday, 23 January 2017


KWELI MOJA TU IMESIMAMA NDANI YA KANISA NA UUMBAJI WOTE.


Wakili wa MUNGU leo amesimaisha Kweli moja tu ndani ya kanisa na uumbaji wote na kusema “Maisha yangu yote kuanzia sasa hivi yatakuwa na Moyo mmoja, hivyo Moyo mmoja umekuwa ni sehemu ya maisha yangu yote milele.”
Sasa baada ya Moyo mmoja tunasimamisha kweli moja halisi. LEO KWELI INASIMAMA NA UKWELI NA UONGO UNAFUTWA.
Kulikuwa hakuna namna ya kuwa na kweli kutokana na mioyo mingi iliyokuwepo tukajikuta hata ukiambiwa uongo unaona ni kweli lakini leo ndio mwisho kweli itajulikana kuwa kweli na uongo utajulikana kuwa ni uongo.
Kwa sababu kweli imesimama sasa hatutasingiziwa tena, hatutazushiwa tena. Mashitaka ya uongo kwa wenye haki leo yameungua.
Maisha ya mateso kwa wenye haki, masingizio kwenye familia, kuchukiwa kwenye familia yako kutengwa kwenye familia yako, kuonekana hufai kumefutwa hutaona tena maana kweli imesimama.
Sasa utaonekana ni mwenye haki kwenye familia nk.
ZEKARIA8:1 na YOHANA8:31-. Kweli pekee ndio inayokuweka huru kila mahali. Tangu zamani kweli haikuwahi kusimama.
Hata wakati wa YESU kila aliposema kweli waliokota mawe wakitaka kumpiga nayo na wakati huo hata wao wanajiita ni wa MUNGU.
Leo tambua hata wale wote WANAOMKATAA wanaomtukana WAKILI WA MUNGU hao sio wa MUNGU japo wanajiita ni wa MUNGU.
*Kweli ilikuwa haikuwahi kukubaliwa popote.*
Kuanzia leo TUMEAGIZWA kusema kweli tu! Kwa kuwa hakuna wa kuokota mawe hakuna wa kukupiga jiwe milele.
KUANZIA LEO TAMBUA KWAMBA MUNGU AMEKUBALIWA NDANI YA UUMBAJI WOTE KWA SABABU KWELI IMESIMAMA.

ZEKARIA8:1- Sasa kanisa ni mji wa kweli ya MUNGU  na MLIMA MTAKATIFU .
Sasa MUNGU atakuwa ni MUNGU wetu katika Kweli na katika Haki.
Adui alikuwa ni moyo wa pili kwa sababu hiyo  MUNGU aliacha tupigane power chafu lakini leo MUNGU hataacha wakusumbue wakupige power chafu kwa sababu tayari Kweli imesimama.
Mwanzoni tulionekana ni laana lakini sasa hatutaonekana laana tena. Wakati wa natuwasha tulionekana kama vile hatuna MUNGU lakini  sasa MUNGU amesimsmisha kweli yake hakuna wa KUNIGUSA.
Kila mmoja na aseme kweli  na jirani yake. Kila mmoja asimame kwa haki asiape kwa uongo.
Huu ndio mwisho wa kerubi , ibilisi, shetani, nyoka mwamamke, mwanaume, kahaba mkuu, mnyama asiyejulikana sasa KANISA LA MUNGU litajulikana.
Kila mmoja na aseme kweli na ndugu yake . mashtaka yaliyokuwa yamepelekwa popote ya uongo yamefutwa.
Aidha wakili ameongoza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Kusimamisha kweli. Kufuta  uongo ukweli. Kufuta mashitaka ya uongo juu ya wenye haki.
Sasa kweli imesimama wengi waliofungwa gerezani wataachiliwa huru kwa sababu wengi walihukumiwa mpaka kufungwa kwa sababu ya mashitaka ya uongo leo mwisho. Mataifa yaliyokuwa yanatumia nguvu ya taifa hili sasa utaona wengi wakiishiwa  wataanguka kwa kuwa kila kitu kinarejea mahali pake.
Sasa hivi ni majira halisi ya KUJULIKANA NA KUTAMBUA kwamba nani alikuwa anamsaidia mwingine /mwenzake. Hii majira ilikuwa inasubiri leo.
Ibada ya jana ilikuwa si ya kawaida ndio iliyotuletea ibada ya leo.  Sasa wewe ambae umeoa  umeolewa badala ya mwingine hapo ndio sijui tumuachie MUNGU mwenyewe.
Wengine tunawaona wamepararaizi lakini kumbe ni mzima ila kuna mmoja anayetumia  upande huo mmoja leo mwisho.
Kuna tuliowaona ni zezeta kumbe ndio wana akili nzuri. Kila aliyekuwa anasoma kwa ajili ya wengine wakaenda juu leo wanafukuzwa vyuoni.
Kila aliyeshitakiwa kwa uongo leo anaachiwa huru. Kweli imesimama kila mmoja atasimama kwa NAFSI yake.

Wengine hapa hawana afya zao sura zao leo zinarejea. 
Haya yote yanatokea kwa kuwa kweli imesimama.
Na ijulikane wale akina mama wenye macho mekundu kule SHINYANGA  kama ni wachawi au laa.
Dini na dhehebu wanasema kuwa SILOAMU ni freemason leo kweli imesimama na ijulikane kama SILOAMU au ni wao dini na dhehebu ndio freemason.
Baada ya kweli kusimama sasa mchawi na asimchawi atajulikana.
Kila mmoja anapokea shea yake kwa MUNGU iliyokusudiwa tangu mwanzo.
Sasa anayesema kweli atajulikana na anayesema uongo atajulikana. Ambae ni mwizi atajulikana na asiye mwizi atajulikana.
SHUKRANI: Kuna kiapo kimesimama *NI MWISHO WA MUNGU, KRISTO WAKO, WAKILI WAKO, KANISA LAKO, TAIFA LAKO NA KIZAZI CHAKO KUSHITAKIWA.*
Tumeinua mnara wa kweli  ambao unasababisha kila mmoja  kuona kuwa SILOAMU ndio wanaosema kweli pekee. Mnara wa uongo uzushi  adui umefutwa.
Hakuna atakae gombana na jirani ndugu yake milele. Mafaili ya kila aina ya uongo yamefutwa.
Leo ni cku ya kukumbukwa mno kwetu. Maana kila nafsi inarudi mahali pake. Kila shilingi dola rasilimali heshima vyote vilivyokuwa vimeibiwa vimerejea mahali pake.
Kila ulichowahi kuibiwa jua leo kimerejea. Mambo ni matamu. MUNGU awabariki awape kila mnachohitaji. 
KWELI NDIO INAYOKUPA KUCHUNGWA NA MUNGU AMBAYE  NDIYE  MCHUNGAJI MMOJA HALISI.

Sunday, 22 January 2017


MOYO MALIDADI KWA UHALISIA NDANI YA KILA MWENYE HAKI.


MUNGU leo ametupa Moyo Toba na unyenyekevu ambao ndio unaotupa kuwa na Moyo Malidadi.
Wakili wa MUNGU akasema pasipo huo unyenyekevu huwezi kupokea huo Moyo Malidadi.
Aidha kabla ya fundisho la leo MUNGU alikuja na ushuhuda wa ushindi wa MUNGU, KRISTO NA KANISA , ushuhuda wa kutisha wa Farasi wa Moto unaoitwa THE POOL OF SILOAM CHURCH.
MUNGU amesema sasa kanisa halipo kwenye yai tena bali hadharani. Akasema mambo haya yanatambulikana kwa jinsi ya Rohoni zaidi.
Kushukuru MUNGU kwa ushuhuda huu ina maana kila mmoja leo alichokuwa anataka amepokea.
Aliyekuwa anataka gorofa, kiwanja, nyumba, gari, kampuni, afya , ufahamu hekima maarifa nk leo umepokea.
Akasema siku ya leo kwa ushuhuda huu chochote ulichowahi kukihitaji leo UMESHAPATA.
Aidha akaonesha kitabu kipya ambacho kina majibu tu ya maswali mbalimbali anayoulizwa MUNGU Aliyetuma wote akasema “KUMBUKA kitabu hiki hakina maswali bali kina majibu tu!
Hivyo hata wewe mwenye haki huna maswali una majibu tu!
Leo hama kituo cha itakuwaje kwa habari ya ada za watoto, kwa habari ya kichwa wangu, kanisa wangu biashara yangu, wajibu wa moto. leo ondoka ukijua una majibu peke yake”.
“Anayetembelea Reli ya rohoni leo anaondoka na majibu peke yake anaondoka na vitu vizuri peke yake” aliongeza Wakili wa MUNGU.
Aidha MUNGU alifurahia uimbaji wa leo akasema HAKUMBUKI SIKU TULIOWAHI KUIMBA VIZURI KAMA LEO!
YOELI 3:16-19; Sasa magonjwa utasa kuzomewa mateso hayataonekana kwa wenye haki tena kwangu kwako milele.
Bonde la shitimu yaani jangwa ukame kukaukiwa kuishiwa kumefutwa kwa wenye haki wala hutaona tena.
Kwa ibada ya leo utakuta account yako imejaa, mlima wa moto utakuta friji limejaa karamu.
leo kila mmoja atapokea zawadi, kila mmoja ataondoka na zawadi yake.
Misri itakuwa ukiwa giza utupu upofu hasara wenye kupatwa na mabaya unyonge utumwa mgumu mahangaiko nk Aliyetamba kwa dhuluma atakuwa ukiwa. Mfuko uliokuwa hauna kitu leo unaondoka umejaa.
Tumefika ile majira ya ukifikiri tu umepokea, kutozaa kwa tabu, huzuni na kuugu vimekimbia kwangu  kwa uhalisi.
MUNGU akasema tuache mshangao muda wa ibada, TAMBUA walishaapa kuwa mwenye haki hatavuka.
*“LEO NAAPA KWAMBA MWENYE HAKI AMEVUKA!!!!”* aliapa Wakili wa MUNGU.
Kulikuwa na madhabahu ya siri iliyokuwa inasababisha kila kitu unachotamkiwa wewe mwenye haki  kizuri kugeuzwa kuwa kibaya , yaani hata utamkiwe NENO tamu vipi unaona kuwa haiwezekani , unaangalia mazingira ulivyolala na njaa jana ulivyopigwa na kutaabishwa na kichwa wako kila siku LEO MUNGU AMEIFUTA HIYO MADHABAHU KWA UHALISI.
Sasa hata hii Madhabahu mahali nilipo ni round sio pembe nne tena , maana huu ni MLIMA WA BWANA hakuna pembe 4. Ni majira ya ISAYA2;2 MATAIFA WANAKUJA hawawezi kufikia kwenye madhabahu ya pembe nne.
LEO, mwambie MUNGU akupe kituo cha kushinda maswali maswali. Unayotamkiwa unaona hayawezekani je hata MUNGU  huna? Je kwa nini sasa usione kwamba umepokea?
Changamka maana kila ulichokuwa unahitaji umepata mtaji umepata. Sema hapa nilipo sina jangwa, sipungukiwi, sifilisiki, sioni majitu, sikati tamaa…. hakuna maskini wote tupo kwenye bustani ya Edeni mpya kabisa.
Aidha Wakili wa MUNGU aliagiza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kuhukumu mtaabishaji wa Kizazi cha MUNGU.
Yeyote aliyekuwa anavaa vazi la kumtaabisha MUNGU Kristo Wakili wa MUNGU Kanisa taifa kizazi cha MUNGU amehukumiwa kwa sadaka hii.
Nataka ufurahie Vazi Jeupe ambalo maana yake ni kutoka kwenye dhiki kuu.
Leo kila mmoja anashuhuda aliyekuwa anazuia amehukumiwa na MUNGU. Kushukuru MUNGU kwa kuwa mtaabishaji wa kizazi cha  MUNGU amehukumiwa tayari.
Maana ilikuwa ukitamkiwa Baraka anasema laana , ukitamkiwa uponyaji anasema magonjwa, fedha-makaratasi, utajiri-umaskini, uzima-mauti leo amehukumiwa.
Sasa umefika wakati wa kwenda mikumi unakutana na simba wala hana haja na wewe, hii itatokea mtaanza kusikia kwenye vyombo vya habari.
Akizungumzia Moyo Malidadi Wakili wa MUNGU alisema Malidadi ni mpya haujawahi kuwepo ,
leo kanisa tunaondoka na Moyo Malidadi mpya. Malidadi ni zaidi ya malidhawa.
Leo MUNGU amefuta mioyo mingi ndani yetu ili tuweze kupata huo moyo Malidadi lazima tuwe na moyo wa toba na unyenyekevu.
TUNAPATA FAIDA GANI; 1SAMWELI 15:10- Unyenyekevu ni nini na faida yake ni nini? Leo tuondoe moyo wa kujihesabia haki kujitetea. Tunaona bado tuna tabia ya kumdanganya MUNGU.
SAULI alikuwa akiambiwa jambo na MUNGU anakubali vizuri anaitikia vyema kabisa lakini akimpa kisogo tu anaenda kufanya kinyume huu ni ukaidi . 
Bado akikutana na nabii wa BWANA akiulizwa na ametoka kufanya kinyume tunaona sauli alisema kuwa amefanya kama MUNGU alivyomuagiza wakati hajawaangamiza waamaleki wala mfalme wao huu ni ukaidi leo tuhame vituo makuhani wa MUNGU NA KRISTO WAKE.
Tunatobolewa macho kwa kukosa kutenda sawa na tunayoagizwa tunatoka ibadani kwa MUNGU WA KWELI tunarudi kwenye dini na dhehebu, mila na desturi, dhambi uovu uasi na yale tuliokuwa tumeyaacha kwenye mataputapu nk leo tambua GARI LA MUNGU HALINA LIVASI.
Unakosoa mafundisho,husikilizi ibada wewe ni wa siku ya tano hadi ya tano, huji ibada ya majibu huu ni UKAIDI na ujue unaibiwa vitu vyako vizuri.
Kilichosababisha sauli kuwa hivyo ni 1SAMWEL 10:17 MOYO ulikuwa na takataka. 
Hamsikilizi masomo nyie mnataka kuniambia hamna laki 1 ,2 za kununua simu nzuri za kusikiliza masomo?  Je, mnashindwa kumwomba SHOHAMU akuunganishe na GROUP uwe unapata masomo ?
MWANZO 3:1- Adamu alikosa moyo wa toba na unyenyekevu. Kutokukubali kosa .
kujihesabia haki . kujitetea hivyo hata ambavyo MUNGU alimuahidi  alivyokuwa amekuahidia HUPATI MILELE kwa kukosa unyenyekevu na toba.
Vilevile MUNGU anakutupa kwa kukosa unyenyekevu na toba na akikutupa amekutupa. 
Acheni uongo, usiseme ni Fulani kanifanyia hivi hivi kanikosesha … kaa kwenye toba tubu kwa yote.
ISAYA 61:1, Mwenye moyo wa unyenyekevu ndie anayepewa habari njema.
WAKILI WA MUNGU; moyo wa toba na unyenyekevu ndio uliosababisha kila siku kupewa ufunuo mpya , miezi 6 hiyo ilikuwa  sio mchezo. 
YOHANA 21:15 YESU alikuwa anataka kumuondolea ule moyo wa kumkana YESU mara3.

1SAMWEL3: NENA BWANA KWA KUWA MTUMISHI WAKO ANASIKIA, huu ni moyo wa unyenyekevu. Unakupa kuisikia sauti ya MUNGU pia kuijua hiyo sauti ya MCHUNGAJI MMOJA.
Mlango wa kupokea huo moyo; Ni kukubali kufundishika usifikiri MUNGU atashuka na suti na miwani.
Siri ya uzuri kwa mabinti ni kuwa na moyo wa unyenyekevu na toba, na akili nzuri unaipata kwa unyenyekevu na toba. RAIS amesema kwa kila jambo mtangulize kwanza MUNGU huu ni unyenyekevu.
Usitake kuchangia pointi kila unachokisikia , acha kusukumia wengine makosa . Wakili amesema; “am talking my life”.
Hata kama kichwa wako hakupendi ondoka na moyo wa unyenyekevu leo lazima atakuambia anakupenda. Majira hii unapokwama muite WAKILI WA MUNGUUUU!!!! Aibu yako itafutika mara moja.
MUNGU HAKOSEI, WAKILI HAKOSEI alichokubali WAKILI na MUNGU amekikubali. Alichokikataa WAKILI na MUNGU amekikataa, aliyekubaliwa na WAKILI na MUNGU amemkubali.
KILA MMOJA ATAMBUE KUWA MOYO WA UNYENYEKEVU NI WEWE UKUBALI KUCHUNGWA NA MCHUNGAJI MMOJA PEKEE zaburi23.