Sunday, 29 January 2017


KUFUNULIWA KWA MAJIRA NA NYAKATI ZA KUPENDEZWA NA KWELI ILYOMO MOYONI ZAB 51:6

Wakili wa MUNGU alipo karibishwa Madhabahuni alianza ibada kwa kusema Shika Nenoooooo!... habari  za siku nyingi? Mnaendeleaje?
Nimekuja kuunganisha KWELI na MOYO maana nimeona wengine wanauliza maswali  kwamba WAKILI alisimamisha KWELI moja  halafu MTENDAJI anaendelea kufundisha MOYO mbona masomo tofauti.
Somo lipo sahihi kabisa kwa sababu hiyo KWELI haikuwepo na iliposimamishwa au ingesimamishwa isingekuwa na mahali pa kukaa maana Moyo haukuwepo ndani yetu ila tulikuwa na mioyo!!
KWELI hukaa ndani ya MOYO, kuna wanaopigana vita kwa sababu hawajui KWELI na hata wangeijua haikuwa na mahali pa kukaa na haikukubaliwa kabisa.
Hivyo wengi waliburuzwa kwa kutoijua hiyo KWELI ya MUNGU. Kuna waliomkataa MUNGU, wakamkosoa na kumdhihaki kwa kutoijua KWELI. Sasa KWELI imepata mahali pa kukaa.
Swali Wakili wa MUNGU aliuliza:- Wangapi walinimiss??  Haah!! Ina maana mlikuwa hamnialiki? …..[tunakualika] sasa kama mnanialika kunimiss kunatoka wapi?  Mnanimisi vipi? 
Ina maana hua hamnialiki kila siku kila wakati mahali ulipo kwenye biashara mlima wa moto ofisini?
Je huwa hamnialiki?
Ujue nimewauliza hivyo makusudi ili nijue maana sitaki mnigeuze kama mchungaji nataka kila wakati mfeel kwamba nipo na ninyi muda wote, kila wakati  kila mahali kwenye biashara , kazi yako, mlima wa moto kwako.
Kwa sababu mimi niliwaambia kwamba nina nguvu nyingi za rohoni. MUNGU alifanya haya ili aone kama huwa mnanialika.
Sasa ukisema umenimisi haya aliyeko karmeli, mlima wa neema kubwa , je aliyeko nchi ya upendo nk?? Atafanyaje? Asemeje sasa yeye?
Na MUNGU aliruhusu  nisije ili ajue kama je mnaelewa au? Maana kila siku nilikuwa natoka nje, dereva anayeniendesha  anakuja kunichukua  lakini MUNGU ananiambia ngoja kidogo….. kwa hiyo nikawa narudi ndani yeye namwambia wasalimie.
Na yeye alivyokuwa mwaminifu  kila siku alikuwa anakuja  kunifuata , lakini MUNGU aliniambia nibaki.. leo ujue kwamba hakuna jambo linalotokea bila sababu.
Sasa muwe mnanialika , mkinialika wala hamtasikia kunimiss  ila mtaniona nikiwa nanyi si nilishawaambia mimi nina nguvu zangu za rohoni.
Wakili wa MUNGU; Amesema kwa kipindi hicho chote alikuwa anatuandalia zawadi ambayo atapewa kila mwenye haki kesho ibadani, japo MTENDAJI ameshawapa hiyo zawadi cha kufanya wewe uje na shilingi 2000 tu maana hata tungekuwa na mashine yetu tungechapisha kwa fedha.
Katika hiyo zawadi kutakuwa na swali juu ya moyo uliochorwa na MTENDAJI ubaoni na katika ile zawadi, utuambie kwa nini umechorwa hivyo na kwa nini upo hivyo una maana gani?
MUNGU ameng’oa ule mwiba ambao ulimchoma Paulo  uliokuwa unaendelea kusumbua kanisani. Mwiba ambao Paulo alipohitaji utolewe MUNGU alimwambia Neema yangu yakutosha leo anauondoa ndani ya Kanisa kwa wenye haki na makuhani.
Kushukuru MUNGU kwa ajili ya kuuondoa huo mwiba uliokuwa unaleta utaabishaji.
Sasa mwiba wa roho ni maneno magumu, matusi utukanwa, kudharauliwa mashitaka hivyo mwenye haki hataonewa tena, hataumizwa tena na kitu chochote tena, sitachomwa na mwiba milele.
Miiba yote MUNGU ameiondoa ndani yangu, unajua kila mmoja hapa nikimwangalia naona ana miiba mingi lakini leo nakuthibitishia MUNGU anaiondoa labda uing’ang’anie wewe mwenyewe.
Kitakachobakia ndani yangu sio miiba tena bali ni ile kweli ambayo imesimama leo.
Wapo wengi ambao hapa kanisani wamechomwa na miiba leo paza sauti yako …. Umshukuru MUNGU kwa sababu miiba imetoka.
Kizazi cha kwanza hadi cha 4 waliotumwa wote walikuwa wakichomwa miiba basi wanakosa amani furaha na haki pia, hivyo wanaowaongoza nao walikuwa wanakosa furaha ile miiba inawapata na kusababisha kizazi nacho kukosa amani.
Leo nashukuru kwa sababu hakuna litakalotokea likanichoma na mwiba.
Majira hii inapoenda kusimamisha kweli yanafutwa mabaya yote na uongo umefutwa milele.
Tumepata moyo wa MUNGU kweli nayo imepata mahali pa kukaa. Tangu majira zilizopita kweli haikuwahi kuwepo ila uongo ndio uliokuwepo.
Kilichokuwa kinaonekana majira zote zilizopita  ni uongo kila sehemu.
Sasa ni kweli moja iliyoko moyoni ndiyo itakayokuwa inaonekana kila sehemu.
Kila atakaeonekana anaongea uongo ataonekana na uumbaji wote kuwa ni kichaa. Sasa kweli iliyoko ndani itatoka nje.
Niliwahi kusoma Uholanzi kuna vitabu vya encyclopedia vinavyoonyesha kuwa muafrica ana mkia hadi ukawa unakatika kidogo kidogo….. kweli jamani muafrica  ana mkia? Si uongo huo.
Wakili;  Ndio maana hata mimi nilinyamaza kimya  … unajua ile katiba ya kanisa iliyoandikwa  walisema hiyo katiba imeandikwa na mmoja tu!
Sasa aliyetakiwa kunitetea na kusema kweli ndiye aliyekuwa wa kwanza kunishitaki.
Alikaa kimya kwa sababu hakuonekana ambaye anaweza kusema kweli, niliyetegemea atasema kweli ndiye aliyedanganya.
Ndio maana nilinyamaza kimya tu!  Maana kweli ya moyo haikupata kibali.
Na kweli ya moyo haikuwahi kusemwa ndio maana wengi  hawakuthubutu kusema  kweli maana hakukuwepo na aliyekuwa tayari kuisikiliza hiyo kweli.
Utasikia wanaosema hili kanisa nalo kwa kuvaa sale sio kuvaa sale kweli inasema vazi jeupe ni kutoka kwenye dhiki kuu ufunuo 7:13
Hivi hujawahi kusikia Rais akisema inawezekana  nikawa sio mwanasiasa mzuri kwa sababu ya kusema kweli.
Wazungu huwa wanasema muafrika ana akili fupi kama zilivyo nywele zake, je sasa hiyo ni kweli?
Kuna dada mmoja alienda America kuwaambia kwamba NABII WA MWISHO ametokea hapa Tanzania, walimuwasha kweli aliporudi akaenda kwa Nabii wa mwisho na kuanza kufoka … kumbe mmenidanganya ….
Na alipotokea MIAKA kuona nani anamfokea Nabii wa mwisho … akamuona huyo dada … ndipo aliposema na wewe MIAKA 1000 ndio muongo mkubwa unaaminika na madhabahuni lkn umesema uongo, ……
Sasa mbona wale wazungu wamesema nina kichaa…. Yote haya yalitokea kwa sababu kweli ilikuwa haijakubalika ndani ya uumbaji wote na haikuwa na mahali pa kukaa lakini leo kwa ibada ya leo kweli imepata pa kukaa na itajulikana kila mahali. Lakini sasa huyo dada yupo mjini huko na penzi nyanya.
Leo kweli imesimama wote watajua kwamba NABII WA MWISHO alitokea hapa, HEAD QUOTER ya MUNGU ni hapa, bustani ya ADEN+EDENI ni hapa, awe muasi, mmarekan, mhindi, muarabu nk wote watakuja hapa. 
There will be a highway from everywhere to here, uwe mzungu, mchina nk ni MTANZANIA.
DANIEL7:22 Kile Daniel alichokiona kwamba alimuona MZEE WA SIKU …. Sasa zile nyayo za MZEE WA SIKU zilionekana hapa.
Miaka 6 iliyopita kuna muisraeli mmoja alikuja ni rafiki mzuri tu wa KUHANI DAMU MOJA, alimwambia kuwa ameambiwa na MUNGU kuwa aje Tanzania maana inaonekana sanduku lipo Ethiopia lakini kilichopo ndani ya hilo sanduku kipo Tanzania.
Lakini hawajui ni wapi….. Damu moja aliponiambia nilimuuliza unafikiri hawajui mahali kilipo? Wanajua vizuri ndio sababu wanagombania mno hili jengo.
Lakini kweli iliyopo ndani ya YOSHUA 1:5 inasema  hakuna asimamae mbele yangu… ukiona bado kuna vinavyokuzuia mbele yako ujue kweli haipo ndani yako.
Marko 7:20-23 ni mpaka uwe na kweli ndani ya moyo wako.
Hawa walishindana wasijue kuwa wanashindana na MUNGU; farao alishindana na Musa, sisera alishindana na Debora, yezebeli alishindana na Eliya mtishibi, wasijue kuwa wanashindana na MUNGU.
Kuna walioshindana na Danieli , pia hamani hakujua kama anashindana na MUNGU.
Ile hali ya kuishiwa ni mwisho kweli imesimama ili wewe mwenye haki usipate shida tena, usigombane na kichwa kanisa ndani ya AGANO.
Waliomsingizia Yusufu na Daniel je walishinda? Hapana. Basi wote wanaokushitaki wanaokuzuia, wanaokuzinga, hawakuwezi  kama walivyoshindwa katika majira zote zilizopita basi wewe ni zaidi.
Wewe ni super maana kweli inayompendeza MUNGU  imesimama ndani yako.
ZABURI 37:25-26 Sijawahi kuona mwenye haki ameachwa, sijawahi kuona mtoto wa mwenye haki akiomba mkate barabarani.
Hata kama umekuja na nauli ya kukopa  tambua leo lazima ushiriki, sio lazima mimi nikupe kwa mkono, je unaamini kuwa leo lazima upokee!!!
Kila jambo baya ulilokuwa umekuja nalo linaishia hapa hapa kwa kuwa kweli moja imesimama.
Aidha Sadaka Maalumu iliyosimamishwa leo ni Kusimamisha kweli kila mahali na kwa sadaka hii majeshi yamesimama, mwenye haki hatakufa milele.
Kutubu kwa kuwa tulikuwa tunaona kinyume na MUNGU.
Niliona kufa tu, nikasema nimetoka mabonde kuinama hivyo siwezi kufanikiwa.
Sasa kufanikiwa ni lazima kwa kuwa  KWELI NI MUNGU na ndio inaniweka huru. Nilikuwa na hofu mashaka wasiwasi leo ni mwisho.
Mioyo hiyo ya hofu mlionayo,  nimeambiwa kuna wengine mlikuwa mnapiga simu ili kujua kama mimi ni mzima je nipo maana hamnioni.
Sadaka ya hakika ya kushinda katika maisha yangu yote ya ushindi, inafuta kuona kuangamizwa, majitu, madhaifu yanaungua, mioyo yote niliyokuwa  nayo zaidi ya moyo wako  yote yapo juu ya sadaka kuunguzwa yote milele.
Kwa sadaka; sifa za leo imenipa uponyaji, imekula maadui wote, imenipa mimi kuvuka moja kwa moja, sifa za leo zimekwisha kumaliza mabaya yote.
Wakili; “Mimi hata siku moja hutakaa uone nachukia milele. Je unajua faida na hasara za kuwa hapo?”
Mafanikio ya wenye haki yapo kwangu ninapochukia kizazi nacho kinaanguka majira hii kizazi hiki HAKITAANGUKA MILELE.
*RAMANI YA KANISA*
EZEKIEL28:16-18 Watu walijaza udhalimu ndani yako,…. moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako,…. umepatia unajisi…..nimetokeza moto…
Haya yote MUNGU alikuwa anamwambia mkamilifu ambaye baadaye alikuja kuasi.
Sasa leo macho yako uyaondoe hata kwa lazima sasa hivi umuone MUNGU anakufundisha ndiye yupo madhabahuni sasa hivi  usimuone MIAKA 1000 wala WAKILI WA MUNGU muone MUNGU sasa hivi ndiye anasema na wewe.
Moyo ulioinuka ndio moto ulitokeza ndani yake hivyo badala ya moyo kutoa chemichemi ya uzima MITHAL 4:23 ISAYA 12:3 moyo ulitoa oili chafu maji machafu badala ya maji masafi.
Badala ya kuwa Baraka ukawa najisi, badala ya uzima ukawa majivu. Je huwa hamuwazi kinyume na mema na MUNGU?
Sasa wengine ndio kabisa  huwa wanawaza kinyume na anayemfundisha alieko madhabahuni. Baada ya kuwaza kinyume utasikia…
Unakuta nikishafundisha hivi kuhani anaenda anadiscus anasema hili nitasema hili sitathubutu kusema wala kufundisha, ni kosa kwa kuhani anaeongoza kituo kujadili somo maaa saa unajadili tu moto unatokeza ndo unaosema hili nitasema hili ni la MIAKA sitasema…….
Leo MUNGU ataongea pasupasu kama ni neema na iwe neema, kwa nini ukubali kutupwa badala ya kutembea pazuri.
Sasa badala ya kumuona WAKILI ubarikiwe ukimuona unalaaniwa,  tubadilike.
Saa unapeleka taarifa za hasara kwa WAKILI kwambabiashara yako umefilisika.
Ni sawa na anayetoa maiti mochwari akampelekea, kuanzia leo hataki kuona wala kusikia anayefilisika anayeishiwa anayepata shida nk anataka kusikia una campuni kubwa viwanda mashamba makubwa
Kataa kituo cha kukaa na MUNGU halafu ukalaaniwa.
Hataki kusikia tena kuna anayeachika ,anayepata hasara KWA AMBAYE YUPO KITUONI KAMA NI KIDOGO AU KIKUBWA.
Badala ya kuwa na akiba njema anakuwa na akiba mbaya;  1SAMWEL 1:14-15  Hana kwa sababu ya kuomba kwa uchungu alionekana ni mlevi.
Ukishaonekana ni mlevi huwezi kujibiwa maombi au shukrani zako.
Pamoja na kwamba umeonewa basi usiweke akiba mbaya ndani ya moyo wako.
Tambua pamoja na wewe kutukanwa hakuna aliyewahi kutukanwa kama MUNGU alivyotukanwa.
sasa sijui utajielezaje mbele yake maana ametukanwa mno MUNGU.
Ujue kuna matusi mengine MUNGU anatukanwa mpaka kwenye magari kwa maandishi kabisa wameandika God is your self, 
Hili ni tusi kabisa, pale ngorongoro kuna wakati nilipita nikakuta watu wapo wengi wanaabudu mti halafu sasa huo mti afadhali hata ungekuwa mkubwa kama mbuyu lakini ni kadogo.
Je kweli akiba mbaya iendelee kukaa ndani ya moyo? Je tunaichukia akiba mbaya au hatuichukii? Tunakumbuka mabaya mno, ndani ya kanisa bado kuna wenye akiba mbaya tena ni wengi.
Je kama ningekuwa nasema kila nachoona nachofanyiwa yanayotokea tungevuka??, tungetoka? Tungeshinda?
Achana na kumbukumbu za uliyofanyiwa mbaya,
Pale ninapoona umevaa suti  halafu unataka kunikosesha ninakuona wewe ni KICHAA. Ili kizazi kisianguke na kizazi hiki hakitaanguka milele.
Sina tabia ya kuuliza mbona umenifanyia hivi, huwa sina livasi hata siku moja, kwa nini unapenda kukumbuka uliyofanyiwa jana juzi mpaka leo unayo leo tuache! Kwa nini unapeleka pua yako CHOONI kunusa????
Principle ya MUNGU kwa anayekukosha muone ni kichaa.
Kuanzia leo umuangalie, umsikilize WAKILI mara zote.
Kuna vitu MUNGU ameruhusu vitokee kabisa. Nataka kuona NENO linathibitika hapa  acha kusikiliza kukumbuka  mwalimu alivyokupiga shule ya msingi, ukoo walivyokutukana wanavyokutukana na walivyokuambia wanakutenga wewe sio ndugu yao.
Leo nataka uje hapa madhabahuni ushike madhabahu  uache kila kumbukumbu iliyokuwa inasumbua ndani yako.
Kila unayekutana yaani mimi nilivyofanyiwa…… Je wewe umekuwa inzi?  Maana inzi ndio ana tabia hiyo ya kufuata kuchukua kupenda kutamani kufurahia uchafu , vitu vibaya tu!!
Jamani muwasamehe vichwa wenu. Akikuambia leo toka mwambie nakupenda, akisema koma mwambie nakupenda, akisema huna kwenu nini mwambie nakupenda, akisema usinifuatefuate jibu lako liwe moja tu NAKUPENDA. Atabadilika tu.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo ya Majira na Nyakati Mtendaji wa Wakili wa MUNGU alifunua kuhusu HISIA ZA MOYO.
Alisema hisia za moyo ni yale tunayoyafanya [unayoyafanya] bila  kukaa chini na kuamua au kupanga mikakati. 
Unafanya pasipo kutegemea unajikuta unacheka, unatabasamu tu, una amani tu, una furaha tu, unaimba tu, unacheza tu.
Au unajikuta unalia mno, unakasirika unanuna tu wewe mwenyewe kumbe ni kutokana na hisia Fulani ulilolikumbuka ulilopitia vile vile inategemea una akiba gani ndani ya moyo yaani hisia yako uliyohisi chanzo chake ni nini inatokana na nini?
Hukupanga kucheka lakini unajikuta umecheka, hata kwenye gari daladala huimbi wakasikia lakini unajikuta unaimba moyo unaimba.
Unapika karamu upo ofisini unahudumia  unakuta unaimba hizi ni hisia za moyo.
Kuna furaha inayokaa ndani yako wewe mwenye haki, kwenye hisia kuna kitu kinaitwa faraha KUTOKA4:14. 
Akimuona tu atafurahi mwenyewe, nae MUNGU atakuwa  pamoja na kinywa cha Haruni na ndani ya kinywa cha Musa hivyo nitasemezana nanyi nanyi mtaelewa.
Kuna jambo kubwa la kutisha linaweza kutokea lakini unajikuta una furaha  au unaweza kupatwa na msiba lakini wewe hata ukijitahidi kulia  unajikuta kulia hakupo ndani yako.
Fuaraha inatoka kwenye moyo wenye akiba njema!!! Ukikutana na mwenye akiba mbaya huwezi kumfurahia hata ukilazimisha kumfurahia kumkumbatia unakuta tu hata moyo ndani unakataa kabisa!! Hisia ni kitu kinachotokea automatic.
Na ukikutana na kitu kibaya  hisia zako unajikuta zinabadilika.
WAKILI WA MUNGU, alipoingia kilichofanyika ni hisia za moyo wako hukupanga kumuona wa  lakini alipotokea tu ulivyomuona tu ukasikia kumfurahia, kumpokea na kumlaki hivyo ukamilifu wa somo kwamba umeelewa ndio huo hukupanga kucheka lakini umecheka umepata burudiko la moyo.
WAFILIPI 4:4-6  Furahini katika BWANA tena nasema furahini…. War 14:17  Maana ufalme wa MUNGU sio kula na kunywa bali ni haki amani na furaha.
Furaha ni hatua kubwa mno kwenye ufalme wa MUNGU.
Ukiwa na akiba ya MUNGU ndani yako unakuwa na furaha wakati wote.
Mahali  pa shida lakini wewe unakuwa na furaha, kuna tukio baya limetokea lakini wewe unakuwa na furaha tu!
Ukitaka ujue kuwa akiba njema imeingia ndani yako ni pale ambapo kuna jambo baya limetokea lakini unajisikia raha tu, ni mahali ambapo unatukanwa lakini unakuwa na furaha, ni wakati ambao  unapita mahali pagumu kwenye matatizo na taabu lakini unakuwa na furaha na huo ndio ufalme wa MUNGU.
Hakuna jambo linalotokea ukasikia kukwazika kukasirika kununa hasira manung’uniko malalamiko tena maana una akiba njema na hisia ya moyo ni njema.
Hatahivyo aliwagiza wenye haki wote kufanya toba ya kina ilikujitenga na kila akiba mbaya kwa kwenda kugusa madhabahu.
Aidha Wakili  wa MUNGU alihitimisha ibada hiyo kwa shukrani maalumu za kusimamisha majira na nyakati hiyo sambamba na kuinua ibada yasiku ya tano kwa vituo vyote vya Kanisa la MUNGU Aliyetuma wote.
Karibu usikilize ibada ya leo iliyobeba majeshi ya Majira na Nyakati iliyosimama leo
kufunuliwa kwa majira   nyakati za kupendezwa na kweli ilyomo moyoni Zab 51:6 ....……..

No comments:

Post a Comment