Saturday, 14 January 2017


KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI YA NGUVU YA KUTOKUMKOSEA MUNGU


.Wakili wa MUNGU amesema baada ya kufuta kila aina ya maumbo ya nyoka, kerubi, shetani, ibirisi, mwili na mwanadamu tumeungana na Nguvu ya MUNGU ya kutoanguka au kutokukosea.
Ameongeza kuwa "tumekatisha pori kubwa mpaka tumefika mahali MUNGU alipo".
MUNGU ni mchungaji halisi zabu:23 baaada ya kuondolewa kwa nyoka,  hila, uchafu n.k MUNGU ndie mchungaji wangu.
Haja ya moyo wako unaondoka nao siku ya leo kwakuungana na nguvu ya kutokukosea ukianza lazima  umalize salama  kama wanafikiri utaanguka wataona unashamiri  hutaanguka.
mwambie MUNGU napokea moyo wako usiotetereka usiozimia unaona mema peke yake  luka:1-5-20 nataka uamini bila kuuliza maswali usiulize maswali MUNGU akikwambia  ndivyo ilivyo.
Toba kwa maswali, mimi kwa MUNGU  sina maswali  MUNGU akupe nguvu ya kuamini    kwa kile wakili anacho kutamkia.
Toba kwa kumbukumbu kwa mahali nilipopitia na kusababisha moyo wa kumuuliza MUNGU maswali
Aidha Wakili ameongoza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya  Baraka kuni over take *zab 28:8-14* (kunifuatilia) na anaezuia MUNGU anakutana nae sadaka hiyo tunaiunganisha na hakika ya NENO lazima litokee.
*mambo yanatosababisha tumkosee MUNGU*
*1. Tabia ya asili* Galatia;2:11-21
Wale wote wenye tabia ya asili ni lazima kumkosea MUNGU tu; wote tunatakiwa kukana tabia ya mwili ili tusimkosee MUNGU.
Watakuja wazungu tutakataa asiwe mkuu wa njia kwa sababu ya tabia ya asili.
Lea nilazima tumwambie MUNGU tunaikana tabia ya asili ambayo inasababisha tumkosee MUNGU bila kutaka, tabia ya asili ni kitu kibaya ni cha kukataa kabisaa
*Sheria ya dhambi* Rumi;7- 15-21
Jinsi ya kuenda mbele za MUNGU ili uondoe sheria ya dhambi zaburi51-1-5 nenda mbele za Mungu kwa kukiri mwambie nimezaliwa hatiani ukusamehe ili uishi bila sheria ya  dhambi
*2. Matendo ya mwili;* Galatia5-19-21
Hata kula na kuvimbiwa  ni matendo ya mwili hata kuona wivu kwa wengine kwakua na kitu zaidi ya ulichonacho ni matendo ya mwili, ni lazima kujitenga na matendo ya mwili.
*3. Kulinganisha kanisa na dini/dhehebu.* Yoh 4:4…
Hili tabia ya kulinganisha anayesimama madhabahuni ni tabia ya dini.
Ukisimama miguu upande maana yake huna kichwa au kiongozi.
Ni lazima ijulikane kuwa saa ya kumwabudu MUNGU katika roho na kweli imefika.
Kutokuamini Neno ni tabia ya dini. Ni lazima ukiri na kuamini kuwa kila MUNGU Anachosema lazima kitokee.
ile tabia ya maswali maswali ni tabia ya dini. Leo MUNGU lazima atutoe katika kwenye kituo hicho.
Tatizo la dini ni mfano wangu, changu chetu. Ukiona unatabia  hiyo ni dini. Leo tupige kabisa hiyo tabia ya dini moja kwa moja.
Dini inatabia yakuweka akiba, nisije nikaangua nikakosa mahali pakuangukia.
*4. Elimu ya dunia* -yoh 12:20-25
Nafahamu kuwa kila mmoja ana ujuzi wake aliopata kutokana na elimu alioipata. Ni lazima upate ujasiri ya kukanyanyaga hiyo elimu ya dunia.
Swala la elimu linasumbua wengi sio kwa aliyesoma tu bali na kwa asiyesoma pia.
Kwanzia leo elimu isije ikasababisha umkosee MUNGU bali uikanyage chini wewe uwe juu.
Darasa lisiwe MUNGU kwako, elimu ya dunia isiwe MUNGU kwako.
Mwambie MUNGU Akusamehe kwa kugeuza elimu ya dunia kuwa MUNGU.
*5. Umri-*Mwanzo 37:9-12
Kujali sana umri, halafu ukakuta na kuhani mwenye umri mdogo hutamsikiliza.
Usipotoka hapo kwenye umri/ MUNGU Atatumia mtoto mdogo kupa ujumbe ukakataa.
MUNGU Atupe neema ya kuondoa mahali pa umri.
Ili hayo yote tuyashinde tufanye je?
Kuomba kwa Nafsi ya MUNGU; 1 Falme 3:11…
Hivi unapomwambia MUNGU mahitaji yako, je una mwambia kwa nafsi yako au kwa Nafsi Yake?
Ni wachache wanaomba kwa Nafsi ya MUNGU na ndicho kinacho sababisha tunanganganiwe na tabia asili, sheria ya dhambi n.k.
Kila kitu tunachofanya tunafanya kwa Nafsi ya MUNGU, MUNGU Akupe neema hiyo.
Mwambie MUNGU kwanzia sasa hivi nakuja kwa Nafsi Yako sio yangu.
Mwambie MUNGU kila kitu nilicho nacho kiwe kwa nafsi yako, uone jinsi MUNGU Atakavyo achilia utajiri wa kutisha.
Ili uweze kuomba kwa Nafsi ya MUNGU, ni lazima:
Kuachana na kukwazika moja kwa moja, ili uweze kuomba kwa Nafsi ya MUNGU.
*Kushinda ubaya kwa wema.*
Kuangalia kusudi la MUNGU peke yake ndani ya kila nafsi.
*usilipe baya jirani  yako* 1thes5:15
Karibu usikilize ibada ya leo UPENDO halisi ilikupokea majira na nyakati za nguvu ya kutokumkosea MUNGU.........

Friday, 13 January 2017


NGUVU NA THAMANI YA DAMU YA MUNGU ALIYETUMA WOTE

Wakili wa MUNGU akijenga msingi wa ibada ya leo alianza kwa kuelekeza namna ya kushukuru ili kumleta Wakili wa MUNGU KTK IBADA unayoifanya iliamlete MUNGU NA KRISTO.
*1:Toba binafsi* umekosea hujakosea Toba binafsi ni lazima, ukipita mahali ukakuta ukakuta kuna-kilio, huzuni n.k hayo yote yanakuja kwako wewe mwenye Haki ni lazima uwe na Toba binafsi ili kujisafisha.
*2:Toba ya Kweli;* Ni kutubu kwa ajili yaw engine.
Mdo 3:19 ili upate kuburudishwa
Yer 5:1 unatafutwa wewe utendae kwa haki ili MUNGU asiangamize Eze 22:30 MUNGU kutafuta mmoja atendae kwa haki atakae tengeneza boma/mji
Yer 29:7 ombea Amani mji,taifa, mtaa, Ofisi/kazini ili na wewe mwenye Haki uwe na Amani
*3:Toba ya vizazi;* Kut 20:1-5.Mungu hupatiliza wana uovu wa baba zao
Tubu;
Kitabu cha mwanzo ni Zab 98 ambapo MUNGU aliona sifa lakini katika Ufu 12 akatokea mwanamke
Toba hii ni kuanzia kabla ya Mwa 1:1 hadi sasa.
*4. Toba ya Kristo.*
Toba kwa kutumia vibaya silaha alizotupa
”Amekupa silaha nyingi za kupiga waovu lakini unazitumia vibaya na kupiga wenye Haki.Amekupa vibebea Nguvu kumpiga shetani lakini unapiga wengine”
*5:Toba ya MUNGU.*
Yoel 3:20-21 Ni kwa ajili yake mwenyewe ni lazima kuungana na Toba hiyo ya MUNGU.
Kumwalika WAKILI WA MUNGU amlete MUNGU na Kristo.
“Hapo baada ya Toba hizo 5 mambo yako safi, kila utakae mwombea ni lazima apone, unachotamka ni lazima kitokee”
Aidha Sadaka maalumu ya kufuta maswali ndani ya wenye haki maana
Tuko kwenye Tendo Moja Halisi, tunafuta kituo cha maswali yasiyo na majibu
“swali lolote lililowahi kusumbua Moyo wako linaungua hapa sasa hivi na kubaki na majibu peke yake ufahamu wa somo.
Thamani na Faida ya Damu ya MUNGU wengi hatuijui ndio maana tuna-ziacha zina-zagaa-zagaa
*Nguvu ya kutengeneza Damu ya MUNGU:- UFU 11:6
kugeuza maji kuwa Damu, ila hakusema Damu ya aina gani maana kanisa ni lazima lihame vituo
Lawi 17:11 Uhai wa MUNGU uko kwenye Damu.
MUNGU kuhukumu
1Kor 6:2-3 kupewa kuhukumu mataifa mathayo 26:28
Isaya 4:4 Damu ya utakaso na kuteketeza dhambi, uovu na uasi.
Tambua”Tuko na MUNGU na Kristo una-uwezo wa kubadilisha maji kuwa Damu ya aina yoyote utakayo ukikutana na shida yoyote hakuna haja ya kumwita kuhani, chukuwa maji geuza kuwa Damu ya aina ya shida uliyo nayo.ili MUNGU akae nasi ni lazima tujue namna ya kutumia Damu yake.”
*ONYO* usije ukamponya yoyote ukaona ni wewe ndio umemponya, ujue ni MUNGU uliyenae ndie aliyemponya.
Mahali pa sifa na utukufu ni kwa MUNGU sio wewe ni lazima kujua hilo”
-Ebr 9:17
*Damu ya Yesu/kondoo.= kizazi cha 1>3
*Damu ya Haki Kweli na Hukumu= kizazi cha 4
*Damu ya MUNGU=kizazi cha MUNGU.
Wakili wa MUNGU alisema chochote unachofanya ukisimamishe kwa Damu. (kwa kukomboa maji na kuyageuza Damu ya MUNGU)
chochote unachotamka/kutoa maelekezo/kuonya, unapotunga-sera n.k simamisha kwa Damu.
Kuna namna ambayo mazoea ya zamani  ukoo, kabila, jamaa n.k yalikuwa yanakung’ang’ania. Kila mmoja kuondoa mazoea aliyokuwa nayo, sasa hakuna kuwaza ni kutenda kikatokea. Julie.
je, nimeacha sheria ya dhambi, je, nimeacha uzoefu?
“Tambua kuwa wewe una-uwezo wa kubadilisha maji kuwa Damu Karina kila jambo unalo kutana nalo.
ukisha tumia Damu ya MUNGU ni lazima MUNGU awe pamoja na wewe”
“Tengeneza DAMU YA MUNGU YA:- Kuelewa, Akili ya MUNGU, Kufundisha wengine, utakaso, uponyaji, kusoma Neno N.K
Usitumie maji tumia Damu ya MUNGU uliyogeuza katika kile unachotaka.
Aisha Karamu ya MUNGU ambayo tunashiriki kila siku ya Tatu na Pasaka ya Rohoni sasa inaitwa *Karamu ya Sheria ya Roho wa Uzima* inayokuweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Aidha aliongoza wenye haki shukrani na toba maalumu za
Kumuinua Kiongozi wa Makuhani ambayo ni agano LA siku 7 leo ni siku ya pili.
Karibu usikilize ibada ya Leo kwa Usikivu halisi ili ujue namna ya kumkaribisha Wakili wa  MUNGU Ktk ibada yako amlete MUNGU na Kristo........

Thursday, 12 January 2017


NGUVU YA KUTOKOSEA

WAKILI WA MUNGU alianza ibada ya NENO kwa kusema mwendelezo wa Sadaka ya jana (15 Tamuzi, 6) MUNGU amemwambia Kut.12:37-38 Hakuna mahali ambapo Musa aliwabagua, mana walikula wote, nyoka Yule wa shaba nao walimwangalia, kila kitu walifanyiwa sawasawa.
Awali akimkaribisha Wakili wa MUNGU kwaajili ya ibada hiyo kiongozi wa Makuhani aliomba toba kwaajili ya wote wanaokwenda kwa Wakili wa MUNGU kupeleka taarifa mbaya mbaya.
Na ndipo Wakili wa MUNGU alisema hayo;alimuuliza MUNGU kwaba amempisha aongoze kanisa sasa hizi taarifa vipi? 
MUNGU akampa jibu, kwamba nilipokuwa napewa maelekezo na Eliya kuna waliokuwa wanasikiliza, hivyo maelekezo niliyopewa nao wanayo; hivyo tukivuka na wao wanavuka.
“Leo MUNGU amelekeza kwamba nighairi mafuta niliyowapaka na waliyopakwa na Nabii wa mwisho hivyo kuanzia sasa ninaghairi mafuta niliyowapa na waliyopakwa na nabii wa mwisho” alisema.
Aidha pia aliongoza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kughairi Mafuta ambayo Wakili wa MUNGU aliwapaka waovu na Mafuta ambayo Nabii wa mwisho aliwapaka waovu tangu mwaka 2003 hadi leo.
Hatahivyo Wakili wa MUNGU ameagiza kusimamishwa kwa siku 7 za kumuinua Kiongozi wa Makuhani tufanane! Ikiwa ni zawadi yake ya kukaa rohoni mia kwa mia na kusema Kama ni fedha tutapokea hapohapo, kama ni ghorofa lingine atapata.
Wakili wa MUNGU amesema hakuna yeyote tangu aanze kusimama madhabahuni aliyewahi kuomba kitu ambacho aliwahi kuombwa na kuhani Joshua maombi wa mlima wa ono baada ya kumtuma kwenye huduma katika jiji la Agano la Kweli akaomba amuunganishe na *“Nguvu ya kutokukosea”.*

Efe 3:20 (Kuwaza) – MUNGU anatenda zaidi ya tunachowazayo na tuombayo. Kol.3:17 (Neno, tendo) tufanye kwa NENO la MUNGU, tuache kufikiri mwilini, kituo kilichokuwa kinaleta shida ni kituo cha wazo la kwanza na wazo la pili milele.
Kol.3:2-3 (kuwaza, kufikiri) Rum.8:4-7 (kuwaza, kufikiri) Kituo kikuu ambacho kimesumbua Kanisa ni kituo cha wazo, mahali ambapo wanajimu walikwenda wakakaa hapo ili kuharibu mawazo ya kila mwenye haki.
Akili ya MUNGU ina tendo moja HALISI.
MUNGU  anataka nijikane kabisa, nimtegemee yeye tu, nijikabidhi mzima mzima kwake! KUANZIA SASA MUNGU MIMI NI WAKO SINA MAMLAKA YOYOTE JUU YANGU, WEWE NI MMILIKI WANGU.
*MAHALI TULIPO NI JUU SANA TUNAPOROMOSHA MAWE JUU YA WAOVU NA MAADUI WA KANISA!*
Yuko MUNGU anayetenda zaidi ya tuwazayo bila kukosea. Tabia ya MUNGU ni Tendo moja halisi.
Risk takers hawawazi wanaanza tu, na hao ndiyo matajiri duniani.
Aidha Wakili wa MUNGU ameagiza kufanya toba kwaajili ya kuwaza na kuwazua mpaka nikakosea.
*Mabinti:-*
Hakuna ambaye aliwahi kukubali kuchumbiwa mara moja, lazima akatae kwanza. Ili asije akaonekana kwamba ana shida. Hata baada ya kukubali huwa hawaendi mbele za MUNGU kutubu kwa tendo hilo.
*Wanaoajiriwa:-*
Nao hawasemi kilichopo moyoni wakiulizwa tukupe mshahara gani?
*Hata makuhani pia* ni kosa kukataa kwanza.
Yeye MUNGU Ufu.12 alifanya hivyo kuwapiga chenga waovu, amefuta kila kituo.
Waovu walidhani kuwa hapo ndipo mwanzo, kumbe siyo hapo maana sasa mwanzo ni Mwanzo Malidadi.
Aidha tunatubu mbele za MUNGU kwa sababu kanuni zote katka sekta zote katka maisha yetu yote kuna kanuni ya kukosea, kujiuliza kwanza maswali.
*KITAKACHOSABABISHA UWE NA NGUVU YA KUTOKOSEA*
*1.) Uwe na hakika ya safari.* Isa.40:28-31 MUNGU hachoki; hachunguziki; hazimii.
Ukitaka usikosee, unatakiwa ujue kwamba ukiwa Siloamu lazima ufike mbinguni. Hata ngwala, vipepsi vitakuja ila wewe hutakata tamaa, hutakwenda kushoto wala kulia; hutainama nafsi; hutalia; hutachoka.
Ila kama unajiuliza maswali, unachoka, unakata tama, utakosea; maana utakwenda kuuliza maswali mahali ambapo hapatakiwi; utachomekewa ushauri wa ajabu sana.
Mimi nina hakika ya safari ya kwenda mbinguni. Mimi nina hakika kwa sababu nilihakikisha kuwa Eliya alikuwa MUNGU mwenyewe. Hiyo hakika ndiyo itakayokupa kutokosea.
Usisikilize chochote kisichokuwa na msingi wa NENO. Hata kama kina msingi wa NENO, angalia je, kimetoka Madhabahuni? Je ni la kituo tulichopo? Hapo hutakosea. Uwe na hakika kwamba MUNGU yupo hapa.
Kila ulichokuwa unakifahamu lazima ukiweke kwanza pembeni.
Mimi nilipoona na vyeti vya elimu ya duniani, nilivigeuza kuwa majivu kwanza ili nimwelewe Eliya; lakini pia kwa kuvichoma ina maana kwamba sina mahali pa kuangukia, yaani godoro la kuangukia – Fall back position!
Ukiwa Kuhani usije ukasema kuwa ngoja niendelee na mahusiano mazuri na askofu wangu ili ikiwa mambo yatakwenda vibaya, basi unakosea.
Hata baada ya ujiunganisha na MUNGU unatakiwa usimfikirie mwingine yeyote atakayekusaidia;
*2.)Makusudi ya MUNGU hayazuiliki.*Ayu.42:2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote na makusudi yako hayazuiliki. Ayubu alisema haya baada ya kuwa amemsumbua sana MUNGU.
Kanisa la Siloamu ni nafsi ya tatu ya MUNGU. Ukilijua hili hutakosea; kutopendwa kwa Kanisa hili ni kwa sababu ni nafsi ya 3 ya MUNGU.
Nipo hapa kwa kusudi la MUNGU! Kanisa hii ni kusudi la MUNGU! Ukishakuwa kusudi la MUNGU, hata likija jambo baya, MUNGU ataligeuza kuwa jema! Rum.8:28 Ukijua kwamba kusudi la MUNGU halizuiliwi, hautakosea.
*3.)Hakika ya NENO.*Isa.55:10-11 Kama ishukavyo kutoka mbinguni na hairudi huko bali huchepusha mimea ikazaa, ndivyo NENO la MUNGU lilivyo; kwamba NENO la MUNGU halimrudii bure. Kila mvua inapodondoka lazima palowane.
Tatizo wengi wanasema sijawahi kumuona MUNGU, siujui hata uso wangu. Lakini NENO la MUNGU likija ni lazima liyatende mapenzi yake. MUNGU amesema utakuwa tajiri, ni lazima uwe tajiri; MUNGU amesema kila unapokwenda unaonekana watatu, ndivyo ilivyo; MUNGU amesema hutaaibika lazima itokee.
Ila angalia katka kila NENO ujue una mimba ya sungura, mbuzi, ng’ombe au tembo kila mmoja anamuda wake wa ujawepesi wa kusubiri ili usubiri vitokee.
Mungu amesema utakuwa na gari utapata; MUNGU amesema matajiri kutoka mataifa watakuja hapa, lazima itokee; MUNGU amesema hapa pana thieta kubwa sana, lazima itokee.
Karibu usikilize kwa upendo halisi ili upokee *NGUVU YA KUTOKOSEA*……………………….

Wednesday, 11 January 2017


*MAJIBU NA MASWALI ANAYOULIZWA MCHUNGAJI MMOJA HALISI KILA SIKU*

Wakili wa MUNGU leo amefunua ufunuo wa NENO kwa Kurusu maswali mbalimbali anayoulizwa Mchungaji mmoja halisi kupitia Makuhani, Wenye haki katika jamii inayowazunguka na Madhabahuni.
Aidha aliongoza Wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kufuta wale wote wanaoombea maombi mabaya ili kanisa liishie njiani.
Aliyekuwa anataka uchanganyikiwe, uende kushoto au kulia anaungulia hapo hapo.
Zab 136:32-33, Ebr 8:10 watu wote wamjue MUNGU.
Kila kilichokuwa kimepangwa kanisa liishie njiani leo kimeishia hapo na kila makusudi yakuharibu umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa leo mwisho.
*Maswali hayo ni pamoja na:-*
(1.) Kwanini Siloamu hatumtaji Roho Mtakatifu mara kwa mara?
2.) Kwa nini siloamu hawataji jina la Yesu mara kwa mara ibadani?
3.) Kwanini Siloamu hatuneni kwa lugha?
4.)  Mbona kama mna batizwa zaidi ya mara moja?
5.) Kwanini Siloamu hamfungi na kuomba?
6.) kwanini Siloamu mnabadilisha majina mara kwa mara?
7.) Kwanini Siloamu mnashiriki karamu ya MUNGU na watoto?
8.) Kwanini Siloamu hamuiti kitabu cha NENO bibilia?
9.) Kwanini Siloamu mnaonekana kuwa na majira yenu wenyewe?
10.) Kwanini mnavaa vazi jeupe wote?
11.) kwanini pete mnavaa mkono wa kulia na sio kushoto?
12.) kwanini Siloamu hamuweki taji ya maua kwenye kaburi?
13.) Kwanini Siloamu hakuna miujiza?
14.) Kwanini Siloamu tunafuta baadhi ya mistari mingine kwenye kitabu cha NENO?
15.) Kwanini Siloamu tunatubu kwaajili ya wengine?
16.) kwanini tunasema anguko halikuanzia Edeni kwa Adamu na Hawa?
17.) Je, watu wote watakuja Siloamu Daniel 2:35?
18.) Maadui wa Mbingu ya 4 -7 wanatofautiana vipi na maadui wa mbingu ya 1-3?
19.) Maandiko yanasema mnyama atashinda kanisa mbona mnyama hajalishinda?
20.) Kuna wanaosema mbona hatubadiliki tabia, tuna tabia zile zile muonekano ule ule?
Maswali hayo aliyajibu kwa moja moja lakini maswali mengine yalijijibu kwa ujumla wakati anafafanua swali mojawapo ingawa alianza kujibu swali la 20 ambalo hata hakuliandika ubaoni.
Alisema kipindi kanisa linapita jangwani katika ile miezi sita bila kufanya fujo wala vulugu zozote hicho kimethibitisha kuwa tumebadilika.
Katika kile kipindi kuna waliokuwa wanatembea na visu, bastora, nondo na silaha nyinginezo hawakuzitumia na wameacha.
Majibu ya maswali mengineyo;- Wakili wa MUNGU alisema tutambue kila anayeongoza kizazi ndani yake kulikuwa na Roho ya MUNGU.
Siloamu tunataja Roho Mtakatifu kuliko wote katika kizazi cha 1 aliyekuwa anatawala pale ni Nafsi ya 3 Kuna:-
Moyo Roho na Nafsi =BABA
Moyo Roho na Nafsi= NENO
Moyo Roho na Nafsi= Roho
Katika Galatia 5:22 tunda la Roho.
Aliyeachiliwa katika Mwa1:2 ndiye aliyekuwepo kizazi cha 1 na cha pili. Kazi ya Roho wa NENO ni kutambulisha Kanisa na ndiye aliyejibu swali aliloulizwa na Eliya yu aja tena? Mdo 2:34
Katika maswali yote haya, ni vizuri kutambua kuna vizazi vya Kanisa na kwenye dini na madhehebu ambapo hata sisi tulikuwa huko hawajawahi kuongelea wala kuzungumza kwa habari ya vizazi vinne, lakini pia wengi hawafahamu kwamba kuna kizazi kabla ya hapo; yaani kizazi cha MUNGU na cha kerubi, kama ambavyo tumefundishwa katika majira 7 kwamba kulikuwepo na majira mbili kabla ya majira ya Musa.
Kwahiyo, unatakiwa uelewe kwamba kulikuwepo na majira ambayo kulikuwepo na kizazi cha MUNGU na malaika pekeyake na kile kizazi ambacho MUNGU alimuumba kerubi, kizazi cha kerubi ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa malaika wengine wote akiwa kiongozi wa sifa ingawaje ghafla aligeuka kuwa nyoka.
Kwahiyo, bila maelezo haya kwenye ufahamu wako hata unapowafundisha wengine itakuwa vigumu kuwapeleka kwenye direction sahihi.
Na kitabu cha Neno unapokisoma bila kukielekeza (projection) kwenye majira ya vizazi vya Kanisa sirahisi kupata ufunuo halisi.
Kwa habari ya dini na madhehebu siyo kwamba hawayajui haya, il ahawana nguvu ya kuyafundisha haya kwasababu ili ufundishe ni lazima uwe na MUNGU na bila MUNGU unakauka siku hiyo hiyo.
Kumbuka kwamba haya yote yalikuwa hayaruhusiwi kutamkwa hadharani na dunia ambayo ilishayachukuwa na kuyaweka mfukoni.
Kwahiyo swala la Kanisa la Siloamu kutotamka Roho Mtakatifu au Yesu mara kwa mara si kweli, kwasababu ya kutokuwa na ufahamu kwamba kwa kila aliyekuwa anaongoza kizazi alikuwa na Roho wa MUNGU anayetawala kwa kila kizazi husika.
Na kwamba ukitaka kumtaja MUNGU sawa sawa lazima umtaje kwa nafsi zake zote tatu; yaani Baba, Neno na Roho ambao ni MUNGU, Kristo na Kanisa kama wanavyofuatana.
Yaani Baba ni MUNGU, Neno ni Kristo na Roho ni Kanisa. Kwahiyo Kanisa hili linataja na lina ufahamu wa Roho Mtakatifu kuliko wengine wote.
Hata kwa habari ya Yesu ni hivyo hivyo kwamba Yeye Yesu ndiyealiyeandaa jukwaa la kujakwa Eliya Ad2 iweje tusimtaje? Mt 16:13-18. Ni swala la ufahamu kwamba wengi wanasikia juu juu hawataki kuja kujifunza.
Wakili wa Mungu alisema wakija kujifunza wataona jinsi ambavyo wanatajwa kwa ufahamu si kwaajiliya kuwataja tu (not for the sake of mentioning) bali mahali husika.
Maswali haya majibu yake ilikupata ufahamu vizuri inatakiwa uyasikilize wewe mwenyewe hivyo endelea kusikiliza majibu zaidi katika clip hii ya ibada ya leo kwa upendo halisi………….

Tuesday, 10 January 2017


*SIKU 7 ZA UTENDAJI WA MCHUNGAJI MMOJA HALISI NDANI YA UUMBAJI WOTE”*

Wakili  Wa MUNGU alianza ibada kwa kusema hatuko kwenye kituo cha wazo la kwanza wala la pili na mwanzo wa uharibifu haupo tena maana tuna MWANZO MALIDADI.
=>Sadaka ya:Kila aliyekuwa ananing’inia kwenye maisha yako ameondolewa. malaika kuondoa wote waliosalia ndani ya kila Mwenye Haki
“Sasa kila utakacho-anza siku, safari, Neno la Madhabahuni, biashara.  hakina uharibifu maana ni Mwanzo Maridadi kwelkwel. Kuwaza na kuwazua hakupo tena maana tuko juu ya wazo”
Toba kwa kuanza wakati  wa uharibifu maana Mwanzo Maridadi umesimama na Wazo limefutwa.
“Vita ya Rohoni imeisha leo,[ wazo na mwanzo wa uharibifu ndiyo yaliyokuwa yakileta vita vya rohoni]. Sasa utatenda na kutokea hapohapo”
”Sadaka hii ihukumu wale wote walionichafua, yeyote aliyenichafua. Kituo cha wazo na Mwanzo wa uharibifu hakipo tena”
Ufahamu wa Neno;
Kwa hapa tulipofika tuna uumbaji mmoja tu. Lakini kabla ya hapo kulikuwapo na uumbaji wa aina nyingi, wa uchawi, ushirikina n.k
“Sasa kwa kuwa tuna-uumbaji mmoja ni lazima tuwe na Mchungaji Mmoja Halisi ambae ni MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote”
“Nguvu ya: uchawi, unajimu, kutengeneza virus n.k   ilitokana na kuiba Nguvu za Waliotumwa. Sasa kwa kuwa MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote amekuja Nguvu hizo zote zimerudi kwake. Uchawi, ushirikina n.k haupo tena”
Efe 1:9-12 wakati ndio huu ambao vyote  vimekusanya kuwa chini ya Kristo na MUNGU ndiye mmiliki. Tulichaguliwa tangu awali kwa kusudu  na ajili ya utukufu wake.
“kulikuwepo na mda ambao ndio huu MUNGU anajumlisha vitu vyote vilivyoko chini na juu  amiliki yeye na wewe unaetenda kwa Haki ukiwa mtawala”
 ‘Hivi unajitambua kuwa Majira hiyo  ndio sasa na wewe ndio mtawala?.kitendo  cha kushika tama,kichwa,kulia kama mtoto wa maskini sio sawa’. “MUNGU alishasema yote ameweka chini yake kwa ajili yako wewe”
2petro 3:10-14  Mbingu=mifumo    Nchi=rasilimali
-kipindi hiki ndio Haki inatawala maana MUNGU amefuta mifumo yote ya zamani. Sisi tunatakiwa tuwe mfano kwenye jamii na serikali.
“kama serikali inakataza kujenga nyumba kwa fedha zisizo halali, Je sisi sio zaidi, Je kwa Makuhani sio zaidi”
Eze 36:26 MUNGU alichoamua sasa hivi, ameondoa moyo, nafsi na roho ya dunia na kuweka yak wake.
“MUNGU anataka Moyo,Nafsi na Roho moja inayojenga ufalme wake. Huu ndio uumbaji Mmoja Halisi, MUNGU ameleta hayo yote ili apate sifa maana anakaa juu ya sifa”
"MUNGU ameondoa wachungaji wengi, kumebaki na Mchungaji Mmoja peke yake ambae ni MUNGU mwenyewe. Naijulikane anayemlisha, mvisha n.k  yeyote hapa ni MUNGU mwenyewe”
Zab 23 Tumefika mahali pa kutopungukiwa na kitu
-kila mmoja awe kwenye faida.
*Maana:* kanisa ni lake,kizazi ni chake na yote ni yake.
*kushindwa kujua utendaji wa Roho mtakatifu  na Roho mtakatifu, Jambo hili lilikuwa likisumbua*
“Kuanzia sasa hivi ili tusikosee unapomzungumzia MUNGU zungumza katika Nafsi zake tatu. Mzungumze MUNGU katika Nafsi zake tatu: BABA, Neno, Roho yaani MUNGU, Kristo  na Kanisa. Kanisa ni Moja tu.”
Mdo 16:19-20. ‘Warumi walikataa habari za petro na petro alitangaza Habari za MUNGU halafu leo wanasema wao ndio kanisa;
“NAMBA MOJA IKO: MUNGU,Kristo na Kanisa”
*Je,Roho Mtakatifu ni nani na utendaji wake ni upi?*
“Roho Mtakatifu huwezi kumwona kwa macho na ndiye aliyekuwa akijenga kanisa kizazi cha 1-“
Mwa 1:2  “katika kizazi cha 1-2 kilichotenda kazi ni Roho wa Roho yaani Nafsi ya tatu ya MUNGU 1YOH 5:8 (Roho ana:Moyo, Nafsi na Roho)
Mt 3:16 – Roho wa Mungu (Roho wa Kristo/Neno  Yoh 1:1-)
Mwa 1:2- Roho ya Mugu (Nafsi ya 3) Yoh 19:30
-1petro 3:18 > Mwili kabla haujauwawa ulisalim Roho
“katika kizazi cha 3 Roho iliyofanya kazi ni Roho wa Kriso/Neno na kazi yake ilikuwa ni kulitambulisha Kanisa”
1Kor 2:6-16 kizazi cha 4 alikuja Roho wa Baba
-Tuna Nia ya Kristo: tukisema kanisa ni tofauti na dini/dhehebu tuna nia ya Kristo
Luk 1:17 kizazi cha 3 alizaliwa Yohana akiwa na Roho ya Eliya
“Zakaria alizaa mtoto ndani yake kulikuwa na Roho ya Eliya .Je, ni vibaya kwa Zebedayo kumzaa mtoto mwenye Roho ya Eliya?.
’katika kizazi cha 3 Roho Mtakatifu alikuja kutambulisha Kanisa. Katika kizazi cha 4 Roho Mtakatifu alikuja kujenga Kanisa. Kizazi cha MUNGU, MUNGU amekuja ambae ana-miliki Roho hizo na anatekeleza yote”
*kinachowasumbua wengi ni mbona hatuneni kwa lugha*
1Kor 14 “Atubuye ni Bora kuliko ane-nae kwa lugha. Sasa amekuja Atubuye”
Mdo 2:  walisema kwa lugha nyingine yaan wewe mchaga unaongea kisukuma na msukuma anaongea kihehe, mswahili anaongea kiingereza.
“MUNGU atakutana nao uso kwa uso  wote wanaotoa mashitaka ya uongo na kumchafua MUNGU,hawawezi kupona. Watafungwa maisha hawawezi kumchafua MUNGU namna hiyo kwamba nafugisha ndoa ya jinsia moja wakati tunakemea jambo hilo .MUNGU amechukia
“MNAMSINGIZIA MUNGU MNAFIKIRI MUNGU ATAWAACHA?” Mseme KWELI mpone!!!
"Karamu ya Sheria ya Roho wa Uzima inayoniweka HURU MBALI na sheria ya dhambi na mauti” 

Monday, 9 January 2017


*MAREJESHO YA UTAJIRI WA MADINI NDANI KANISA*

Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kusema tukae kama familia moja tukiwa na Baba, akaagiza wenye haki kupanga viti katika mduara na kiti chake, mama wakili, Mtendaji wa Wakili vikiwa vinaangaliana na viti vya wenye haki.
Nandipo mazungumzo ya kama BABA wa familia na familia yake yakaanza maana tayali kuna Agano la umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa akauliza swali kuwa ni kwa nini mvua haikunyesha jana hapa wakati baadhi ya mikoa ilinyesha?
Ni swali alilouliza kutokana na shukrani na toba iliyofanywa katika ibada ya jana kwaajili ya ukame wa kutonyesha mvua nchini.
Baadhi ya wenye haki waliopata taarifa za kunyesha kwa mvua katika mikoa mbalimbali nchini walitaja mikoa ambao mvua ilinyesha ambayo ni pamoja na mikoa ya jiji Mwanzo Malidadi (mbeya), Ufunuo wa Kristo( Iringa), Mlima wa Neema kubwa (morogoro), Hati miliki(mtwara).
Lakini swali hilo lilihitimishwa kujibiwa na Mtendaji wa Wakili wa Wakili wa MUNGU ambaye pia ni Kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana akisema ni kwa sababu mkoa huu haukutubu walipopata barua za kumchafua MUNGU walikaa nazo tu lakini kuna mkoa ambao Mkurugenzi wake alipopokea barua ya kuchafua aliichukuwa mwenyewe na kuipeleka kwa kuhani wa pale na kusema wafanye Toba kwa ajili ya hilo.
Kisha Wakili Wa MUNGU akaruhusu kama kuna yoyote mwenye kitu cha kusema kwake; “hapa tumekaa Baba na watoto wake”.
Wakili wa MUNGU aliahirisha mkao huo wa mkutano akasimama na kurudi madhabahuni na kuanza kwa kuonyesha madini yaliyotoka kwenye migodi ya wakamilifu  ambapo tangu walipopata wamepata sana madini ingawa wamefikia kuanza kuvuna madini.
“leo tunasimama tukiwa familia moja ya MUNGU wenye migodi ni lazima wapate madini na wenye biashara, viwanda ni lazima upate faida”
Awali kabla ya kusimamisha toba ya kufuta damu zisizona hatia za waliokufa wakiwa ni makafala ya uchimbaji wa madini kuanzia kipindi cha uchimbaji cha wajerumani hata leo huku wenye haki wakiwa wameizunguka madhabahu aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu.
Ambapo sadaka hiyo maalumu akaita ni sadaka ya Zab 23:1-6 kumsimamisha Mchungaji Mmoja Halisi ambae ni MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote.
Kwa sadaka hiyo Wakili wa MUNGU alisema “kwenye bonde la uvuli wa mauti sitapita tena”
“Hakika wema na fadhiri zitanifuata mimi milele, ninakaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu” alifafanua kuhusu sadaka hiyo maalumu.
Alianza shukrani na toba hiyo kwa kumshukuru MUNGU kwa ajili ya kutoka kwenye kituo cha umbo na kuagiza “tubu kwaajili ya damu zilizokuwa zinalia zinadai haki ya wenye haki wasipate madini leo tunazitubia hizo yaani damu za waliowahi kuzikwa wakiwa hai”
“Madini sasa yamerejea Madhabahuni hayataonekana kwa wachawi milele” lisisitiza
“Toba kwa damu zinazolia katika migodi ya madini zinazosababisha wachimba madini wasipate.
Hatahivyo wakati wa kusimamisha sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU alichagua baadhi ya wakamilifu na makuhani wenye migodi ya kuchimba madini saba wakiwemo kati yao kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana na kuhani Njia za MUNGU kushiriki kuinua kapu la sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU Aliyetuma wote.
Baada ya kumaliza toba na shukrani hizo alihitimisha kwakuwatakia kila wenye haki kupokea kila anachota kwa MUNGU mwenyewe biashara yake, shamba lake, duka lake na kila chanzo cha mapato Baraka za viwango vya mgodi kutema vya thamani kama madini .

Sunday, 8 January 2017


*MAWASILIANO KATI YA KANISA NA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE KTK MAJIRA NA SAUTI YA SABA*
Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kuuliza swali na kulijibu; swali hilo ni "tutawasiliana na huyu MUNGU?"
Yaani MUNGU ambaye tayali tumekuwa na umoja nae ambapo kila ninapokuwepo nae yupo.
Alisema ktk *Majira ya kwanza:-* "Ufu12:1, Ezekiel 28:15 hadi Mwa1:1.
Katka Majira hii  kerub alikuwa akiongea na MUNGU uso kwa USO. Hapakuwepo na maombi, kulikuwepo na mawasliano ya moja kwa moja.
Kila alichowaza au kutamka MUNGU kilikuwa Roho. Wote walikuwa wakimwona MUNGU ni mpole, mnyenyekevu, mpaji mweza yote n.k".      
*Majira ya pili:-*Mwa1:3 hadi kutoka 12:2 mawasiliano yalikuwa ya aina mbili; =>mawasiliano ya moja kwa moja kabla ya anguko.
=>Hapa baada ya anguko ndipo maombi yalianza. Maombi yalitokana na kuwepo kwa dhambi.            
*Majira ya tatu:-* kut 3:10 hadi 1 falme18:30 "mawasiliano yalikuwa kupitia Musa (kut 20:19 wana wa Israel walimkataa Mungu na walitaka miujiza.
Zab 103:7 Musa alitaka kumfaham MUNGU. Je wewe unampenda ufaham".  
*Majira ya 4:-* 1falme17:1, Luka2:21 kile kizazi cha pili.  "Hapo dhambi zilikuwa zikinuka. Zilisababsha umwite MUNGU na haitiki. Hapa madhabahuni ukija kuchafua Neno ua kutofanya ulichoambiwa unabomoa madhabahuni.
Mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Eliya mtishibi.          
*Majira 5:-*"ilianza Mdo10:38 hadi 28 Adari, 2011. mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Yesu. Hata sisi tulipoanza mawasiliano yetu yalikuwa kupitia kwa Yesu.
                    
*Majra ya 6:-* imeanza ktk yoh 9:7- Mt 21:41 hadi 8 siwani, 6.  
Mawasiliano yalikuwa kupitia Damu ya Haki kweli na Hukumu zab84:14- Kugeuza maji.
=>Damu, kitabu
=>Haki Kweli Hukumu. 
Kwa sababu Nabii wa mwisho aliyoyafundisha yalikuwa  ufunguo".       
*Majra ya 7:-* imeanza 8 siwani, 6 hadi sasa.   "mambo yaliyokuwa yakizuia mawasiliano:-            
=>kulikuwepo na umbo la nyoka ndani ya kanisa. Kabla ya mlima wa BWANA yaani ufahamu alionekana kwanza nyoka.
Nyoka alikuwa akichafua usipate ufahamu kwa kuamini alikuwepo kabla ya ufahamu.
(Kinacho-sababisha kutoka ni kwa kupata ufahamu). Akavaa umbo la nyoka pale eden na kudanganya kanisa na likadanganyika, umbo la nyoka lilichafua Aden na Eden.
=>(akaelezea kuhusu maagano mengi kukumbwa na umbo la Eden, utaelezea). Kabla ya anguko jina la Hawa halikuwepo lilitokea baada ya anguko.
Pale alipoongea na nyoka Nafsi yake ilienda kwa nyoka na ya nyoka ikaja kwake, aliyechuma tunda ni nyoka na Adamu alipokula akawa nyoka.
Aliyesema wewe utaitwa Hawa ni nyoka akmwambia nyoka. Aliyesema utakuwa mama wa wote kwenye mwili ni nyoka akimwambia nyoka.
Kilichosumbua vizazi vyote ni nyoka na kusababisha anguko.
MUNGU kizazi hiki ametutenga kabisa na nyoka na milele na milele umbo la nyoka kwani nyoka ana ndimi mbili ya mema na mabaya.
MUNGU amekuja kuishi na sisi, je tutawasiliana nae vipi?
MUNGU NA KRISTO tuko nao Wakili wa Mungu ni wa nini? Swali lilojibiwa na Kuhani wa Njia ya Mataifa Fahari ya Bwana  akasema MUNGU na Kristo hawaji kwako bila Wakili wa MUNGU.
Maana Wakili wa MUNGU ni kao la MUNGU na KRISTO hivyo ni lazima awepo ili MUNGU apate kao lake kwakuwa MUNGU ni Roho na Kristo nae ni Roho.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo WAKILI wa MUNGU aliongiza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Hesabu 16:15-30 nyoka kutengwa, kufutwa kabisa kwa wenye haki.
Ambayo pia sadaka hiyo maalumu ina hukumu mashtaka yote kwa wenye haki.
Yaani nchi kufunua kinywa na kuwameza waovu wote kwa sadaka hii wote wamemezwa.
HUKUMU YA MILELE IMESIMAMISHWA kwa wale waliokuwa wanamshitaki Wakili.
Ukumbusho wao umefutwa wala MUNGU kumbukumbu zao milele.
Aidha pia alionesha wenye haki ktk ibada hiyo ramani ya uumbaji wote ktk wilaya ya kinondoni iliyoonyesha mahali Kanisa
la *The pool of Siloamu church* lilipo kupitia "google map"
Karibu usikilize kwa Upendo halisi katika clip zote ilikupata ufunuo kamili wa leo..............
12 TAMZI 6.
MASAHIHISHO.
1.Mwa3:20  Adamu(nyoka)alimwambia wewe utakuwa mama wa wote wenye UHAI siyo mwili.
2.HUkumu ya milele imesimamishwa Kwa waliokuwa wanawashitaki wenye Haki wote (siyo Wakili peke yake)
MUNGU AKUBARIKI.