Showing posts with label 18 Tamuzi. Show all posts
Showing posts with label 18 Tamuzi. Show all posts

Saturday, 14 January 2017


KUSIMAMISHA MAJIRA NA NYAKATI YA NGUVU YA KUTOKUMKOSEA MUNGU


.Wakili wa MUNGU amesema baada ya kufuta kila aina ya maumbo ya nyoka, kerubi, shetani, ibirisi, mwili na mwanadamu tumeungana na Nguvu ya MUNGU ya kutoanguka au kutokukosea.
Ameongeza kuwa "tumekatisha pori kubwa mpaka tumefika mahali MUNGU alipo".
MUNGU ni mchungaji halisi zabu:23 baaada ya kuondolewa kwa nyoka,  hila, uchafu n.k MUNGU ndie mchungaji wangu.
Haja ya moyo wako unaondoka nao siku ya leo kwakuungana na nguvu ya kutokukosea ukianza lazima  umalize salama  kama wanafikiri utaanguka wataona unashamiri  hutaanguka.
mwambie MUNGU napokea moyo wako usiotetereka usiozimia unaona mema peke yake  luka:1-5-20 nataka uamini bila kuuliza maswali usiulize maswali MUNGU akikwambia  ndivyo ilivyo.
Toba kwa maswali, mimi kwa MUNGU  sina maswali  MUNGU akupe nguvu ya kuamini    kwa kile wakili anacho kutamkia.
Toba kwa kumbukumbu kwa mahali nilipopitia na kusababisha moyo wa kumuuliza MUNGU maswali
Aidha Wakili ameongoza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya  Baraka kuni over take *zab 28:8-14* (kunifuatilia) na anaezuia MUNGU anakutana nae sadaka hiyo tunaiunganisha na hakika ya NENO lazima litokee.
*mambo yanatosababisha tumkosee MUNGU*
*1. Tabia ya asili* Galatia;2:11-21
Wale wote wenye tabia ya asili ni lazima kumkosea MUNGU tu; wote tunatakiwa kukana tabia ya mwili ili tusimkosee MUNGU.
Watakuja wazungu tutakataa asiwe mkuu wa njia kwa sababu ya tabia ya asili.
Lea nilazima tumwambie MUNGU tunaikana tabia ya asili ambayo inasababisha tumkosee MUNGU bila kutaka, tabia ya asili ni kitu kibaya ni cha kukataa kabisaa
*Sheria ya dhambi* Rumi;7- 15-21
Jinsi ya kuenda mbele za MUNGU ili uondoe sheria ya dhambi zaburi51-1-5 nenda mbele za Mungu kwa kukiri mwambie nimezaliwa hatiani ukusamehe ili uishi bila sheria ya  dhambi
*2. Matendo ya mwili;* Galatia5-19-21
Hata kula na kuvimbiwa  ni matendo ya mwili hata kuona wivu kwa wengine kwakua na kitu zaidi ya ulichonacho ni matendo ya mwili, ni lazima kujitenga na matendo ya mwili.
*3. Kulinganisha kanisa na dini/dhehebu.* Yoh 4:4…
Hili tabia ya kulinganisha anayesimama madhabahuni ni tabia ya dini.
Ukisimama miguu upande maana yake huna kichwa au kiongozi.
Ni lazima ijulikane kuwa saa ya kumwabudu MUNGU katika roho na kweli imefika.
Kutokuamini Neno ni tabia ya dini. Ni lazima ukiri na kuamini kuwa kila MUNGU Anachosema lazima kitokee.
ile tabia ya maswali maswali ni tabia ya dini. Leo MUNGU lazima atutoe katika kwenye kituo hicho.
Tatizo la dini ni mfano wangu, changu chetu. Ukiona unatabia  hiyo ni dini. Leo tupige kabisa hiyo tabia ya dini moja kwa moja.
Dini inatabia yakuweka akiba, nisije nikaangua nikakosa mahali pakuangukia.
*4. Elimu ya dunia* -yoh 12:20-25
Nafahamu kuwa kila mmoja ana ujuzi wake aliopata kutokana na elimu alioipata. Ni lazima upate ujasiri ya kukanyanyaga hiyo elimu ya dunia.
Swala la elimu linasumbua wengi sio kwa aliyesoma tu bali na kwa asiyesoma pia.
Kwanzia leo elimu isije ikasababisha umkosee MUNGU bali uikanyage chini wewe uwe juu.
Darasa lisiwe MUNGU kwako, elimu ya dunia isiwe MUNGU kwako.
Mwambie MUNGU Akusamehe kwa kugeuza elimu ya dunia kuwa MUNGU.
*5. Umri-*Mwanzo 37:9-12
Kujali sana umri, halafu ukakuta na kuhani mwenye umri mdogo hutamsikiliza.
Usipotoka hapo kwenye umri/ MUNGU Atatumia mtoto mdogo kupa ujumbe ukakataa.
MUNGU Atupe neema ya kuondoa mahali pa umri.
Ili hayo yote tuyashinde tufanye je?
Kuomba kwa Nafsi ya MUNGU; 1 Falme 3:11…
Hivi unapomwambia MUNGU mahitaji yako, je una mwambia kwa nafsi yako au kwa Nafsi Yake?
Ni wachache wanaomba kwa Nafsi ya MUNGU na ndicho kinacho sababisha tunanganganiwe na tabia asili, sheria ya dhambi n.k.
Kila kitu tunachofanya tunafanya kwa Nafsi ya MUNGU, MUNGU Akupe neema hiyo.
Mwambie MUNGU kwanzia sasa hivi nakuja kwa Nafsi Yako sio yangu.
Mwambie MUNGU kila kitu nilicho nacho kiwe kwa nafsi yako, uone jinsi MUNGU Atakavyo achilia utajiri wa kutisha.
Ili uweze kuomba kwa Nafsi ya MUNGU, ni lazima:
Kuachana na kukwazika moja kwa moja, ili uweze kuomba kwa Nafsi ya MUNGU.
*Kushinda ubaya kwa wema.*
Kuangalia kusudi la MUNGU peke yake ndani ya kila nafsi.
*usilipe baya jirani  yako* 1thes5:15
Karibu usikilize ibada ya leo UPENDO halisi ilikupokea majira na nyakati za nguvu ya kutokumkosea MUNGU.........