Wednesday, 11 January 2017


*MAJIBU NA MASWALI ANAYOULIZWA MCHUNGAJI MMOJA HALISI KILA SIKU*

Wakili wa MUNGU leo amefunua ufunuo wa NENO kwa Kurusu maswali mbalimbali anayoulizwa Mchungaji mmoja halisi kupitia Makuhani, Wenye haki katika jamii inayowazunguka na Madhabahuni.
Aidha aliongoza Wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kufuta wale wote wanaoombea maombi mabaya ili kanisa liishie njiani.
Aliyekuwa anataka uchanganyikiwe, uende kushoto au kulia anaungulia hapo hapo.
Zab 136:32-33, Ebr 8:10 watu wote wamjue MUNGU.
Kila kilichokuwa kimepangwa kanisa liishie njiani leo kimeishia hapo na kila makusudi yakuharibu umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa leo mwisho.
*Maswali hayo ni pamoja na:-*
(1.) Kwanini Siloamu hatumtaji Roho Mtakatifu mara kwa mara?
2.) Kwa nini siloamu hawataji jina la Yesu mara kwa mara ibadani?
3.) Kwanini Siloamu hatuneni kwa lugha?
4.)  Mbona kama mna batizwa zaidi ya mara moja?
5.) Kwanini Siloamu hamfungi na kuomba?
6.) kwanini Siloamu mnabadilisha majina mara kwa mara?
7.) Kwanini Siloamu mnashiriki karamu ya MUNGU na watoto?
8.) Kwanini Siloamu hamuiti kitabu cha NENO bibilia?
9.) Kwanini Siloamu mnaonekana kuwa na majira yenu wenyewe?
10.) Kwanini mnavaa vazi jeupe wote?
11.) kwanini pete mnavaa mkono wa kulia na sio kushoto?
12.) kwanini Siloamu hamuweki taji ya maua kwenye kaburi?
13.) Kwanini Siloamu hakuna miujiza?
14.) Kwanini Siloamu tunafuta baadhi ya mistari mingine kwenye kitabu cha NENO?
15.) Kwanini Siloamu tunatubu kwaajili ya wengine?
16.) kwanini tunasema anguko halikuanzia Edeni kwa Adamu na Hawa?
17.) Je, watu wote watakuja Siloamu Daniel 2:35?
18.) Maadui wa Mbingu ya 4 -7 wanatofautiana vipi na maadui wa mbingu ya 1-3?
19.) Maandiko yanasema mnyama atashinda kanisa mbona mnyama hajalishinda?
20.) Kuna wanaosema mbona hatubadiliki tabia, tuna tabia zile zile muonekano ule ule?
Maswali hayo aliyajibu kwa moja moja lakini maswali mengine yalijijibu kwa ujumla wakati anafafanua swali mojawapo ingawa alianza kujibu swali la 20 ambalo hata hakuliandika ubaoni.
Alisema kipindi kanisa linapita jangwani katika ile miezi sita bila kufanya fujo wala vulugu zozote hicho kimethibitisha kuwa tumebadilika.
Katika kile kipindi kuna waliokuwa wanatembea na visu, bastora, nondo na silaha nyinginezo hawakuzitumia na wameacha.
Majibu ya maswali mengineyo;- Wakili wa MUNGU alisema tutambue kila anayeongoza kizazi ndani yake kulikuwa na Roho ya MUNGU.
Siloamu tunataja Roho Mtakatifu kuliko wote katika kizazi cha 1 aliyekuwa anatawala pale ni Nafsi ya 3 Kuna:-
Moyo Roho na Nafsi =BABA
Moyo Roho na Nafsi= NENO
Moyo Roho na Nafsi= Roho
Katika Galatia 5:22 tunda la Roho.
Aliyeachiliwa katika Mwa1:2 ndiye aliyekuwepo kizazi cha 1 na cha pili. Kazi ya Roho wa NENO ni kutambulisha Kanisa na ndiye aliyejibu swali aliloulizwa na Eliya yu aja tena? Mdo 2:34
Katika maswali yote haya, ni vizuri kutambua kuna vizazi vya Kanisa na kwenye dini na madhehebu ambapo hata sisi tulikuwa huko hawajawahi kuongelea wala kuzungumza kwa habari ya vizazi vinne, lakini pia wengi hawafahamu kwamba kuna kizazi kabla ya hapo; yaani kizazi cha MUNGU na cha kerubi, kama ambavyo tumefundishwa katika majira 7 kwamba kulikuwepo na majira mbili kabla ya majira ya Musa.
Kwahiyo, unatakiwa uelewe kwamba kulikuwepo na majira ambayo kulikuwepo na kizazi cha MUNGU na malaika pekeyake na kile kizazi ambacho MUNGU alimuumba kerubi, kizazi cha kerubi ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa malaika wengine wote akiwa kiongozi wa sifa ingawaje ghafla aligeuka kuwa nyoka.
Kwahiyo, bila maelezo haya kwenye ufahamu wako hata unapowafundisha wengine itakuwa vigumu kuwapeleka kwenye direction sahihi.
Na kitabu cha Neno unapokisoma bila kukielekeza (projection) kwenye majira ya vizazi vya Kanisa sirahisi kupata ufunuo halisi.
Kwa habari ya dini na madhehebu siyo kwamba hawayajui haya, il ahawana nguvu ya kuyafundisha haya kwasababu ili ufundishe ni lazima uwe na MUNGU na bila MUNGU unakauka siku hiyo hiyo.
Kumbuka kwamba haya yote yalikuwa hayaruhusiwi kutamkwa hadharani na dunia ambayo ilishayachukuwa na kuyaweka mfukoni.
Kwahiyo swala la Kanisa la Siloamu kutotamka Roho Mtakatifu au Yesu mara kwa mara si kweli, kwasababu ya kutokuwa na ufahamu kwamba kwa kila aliyekuwa anaongoza kizazi alikuwa na Roho wa MUNGU anayetawala kwa kila kizazi husika.
Na kwamba ukitaka kumtaja MUNGU sawa sawa lazima umtaje kwa nafsi zake zote tatu; yaani Baba, Neno na Roho ambao ni MUNGU, Kristo na Kanisa kama wanavyofuatana.
Yaani Baba ni MUNGU, Neno ni Kristo na Roho ni Kanisa. Kwahiyo Kanisa hili linataja na lina ufahamu wa Roho Mtakatifu kuliko wengine wote.
Hata kwa habari ya Yesu ni hivyo hivyo kwamba Yeye Yesu ndiyealiyeandaa jukwaa la kujakwa Eliya Ad2 iweje tusimtaje? Mt 16:13-18. Ni swala la ufahamu kwamba wengi wanasikia juu juu hawataki kuja kujifunza.
Wakili wa Mungu alisema wakija kujifunza wataona jinsi ambavyo wanatajwa kwa ufahamu si kwaajiliya kuwataja tu (not for the sake of mentioning) bali mahali husika.
Maswali haya majibu yake ilikupata ufahamu vizuri inatakiwa uyasikilize wewe mwenyewe hivyo endelea kusikiliza majibu zaidi katika clip hii ya ibada ya leo kwa upendo halisi………….

Tuesday, 10 January 2017


*SIKU 7 ZA UTENDAJI WA MCHUNGAJI MMOJA HALISI NDANI YA UUMBAJI WOTE”*

Wakili  Wa MUNGU alianza ibada kwa kusema hatuko kwenye kituo cha wazo la kwanza wala la pili na mwanzo wa uharibifu haupo tena maana tuna MWANZO MALIDADI.
=>Sadaka ya:Kila aliyekuwa ananing’inia kwenye maisha yako ameondolewa. malaika kuondoa wote waliosalia ndani ya kila Mwenye Haki
“Sasa kila utakacho-anza siku, safari, Neno la Madhabahuni, biashara.  hakina uharibifu maana ni Mwanzo Maridadi kwelkwel. Kuwaza na kuwazua hakupo tena maana tuko juu ya wazo”
Toba kwa kuanza wakati  wa uharibifu maana Mwanzo Maridadi umesimama na Wazo limefutwa.
“Vita ya Rohoni imeisha leo,[ wazo na mwanzo wa uharibifu ndiyo yaliyokuwa yakileta vita vya rohoni]. Sasa utatenda na kutokea hapohapo”
”Sadaka hii ihukumu wale wote walionichafua, yeyote aliyenichafua. Kituo cha wazo na Mwanzo wa uharibifu hakipo tena”
Ufahamu wa Neno;
Kwa hapa tulipofika tuna uumbaji mmoja tu. Lakini kabla ya hapo kulikuwapo na uumbaji wa aina nyingi, wa uchawi, ushirikina n.k
“Sasa kwa kuwa tuna-uumbaji mmoja ni lazima tuwe na Mchungaji Mmoja Halisi ambae ni MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote”
“Nguvu ya: uchawi, unajimu, kutengeneza virus n.k   ilitokana na kuiba Nguvu za Waliotumwa. Sasa kwa kuwa MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote amekuja Nguvu hizo zote zimerudi kwake. Uchawi, ushirikina n.k haupo tena”
Efe 1:9-12 wakati ndio huu ambao vyote  vimekusanya kuwa chini ya Kristo na MUNGU ndiye mmiliki. Tulichaguliwa tangu awali kwa kusudu  na ajili ya utukufu wake.
“kulikuwepo na mda ambao ndio huu MUNGU anajumlisha vitu vyote vilivyoko chini na juu  amiliki yeye na wewe unaetenda kwa Haki ukiwa mtawala”
 ‘Hivi unajitambua kuwa Majira hiyo  ndio sasa na wewe ndio mtawala?.kitendo  cha kushika tama,kichwa,kulia kama mtoto wa maskini sio sawa’. “MUNGU alishasema yote ameweka chini yake kwa ajili yako wewe”
2petro 3:10-14  Mbingu=mifumo    Nchi=rasilimali
-kipindi hiki ndio Haki inatawala maana MUNGU amefuta mifumo yote ya zamani. Sisi tunatakiwa tuwe mfano kwenye jamii na serikali.
“kama serikali inakataza kujenga nyumba kwa fedha zisizo halali, Je sisi sio zaidi, Je kwa Makuhani sio zaidi”
Eze 36:26 MUNGU alichoamua sasa hivi, ameondoa moyo, nafsi na roho ya dunia na kuweka yak wake.
“MUNGU anataka Moyo,Nafsi na Roho moja inayojenga ufalme wake. Huu ndio uumbaji Mmoja Halisi, MUNGU ameleta hayo yote ili apate sifa maana anakaa juu ya sifa”
"MUNGU ameondoa wachungaji wengi, kumebaki na Mchungaji Mmoja peke yake ambae ni MUNGU mwenyewe. Naijulikane anayemlisha, mvisha n.k  yeyote hapa ni MUNGU mwenyewe”
Zab 23 Tumefika mahali pa kutopungukiwa na kitu
-kila mmoja awe kwenye faida.
*Maana:* kanisa ni lake,kizazi ni chake na yote ni yake.
*kushindwa kujua utendaji wa Roho mtakatifu  na Roho mtakatifu, Jambo hili lilikuwa likisumbua*
“Kuanzia sasa hivi ili tusikosee unapomzungumzia MUNGU zungumza katika Nafsi zake tatu. Mzungumze MUNGU katika Nafsi zake tatu: BABA, Neno, Roho yaani MUNGU, Kristo  na Kanisa. Kanisa ni Moja tu.”
Mdo 16:19-20. ‘Warumi walikataa habari za petro na petro alitangaza Habari za MUNGU halafu leo wanasema wao ndio kanisa;
“NAMBA MOJA IKO: MUNGU,Kristo na Kanisa”
*Je,Roho Mtakatifu ni nani na utendaji wake ni upi?*
“Roho Mtakatifu huwezi kumwona kwa macho na ndiye aliyekuwa akijenga kanisa kizazi cha 1-“
Mwa 1:2  “katika kizazi cha 1-2 kilichotenda kazi ni Roho wa Roho yaani Nafsi ya tatu ya MUNGU 1YOH 5:8 (Roho ana:Moyo, Nafsi na Roho)
Mt 3:16 – Roho wa Mungu (Roho wa Kristo/Neno  Yoh 1:1-)
Mwa 1:2- Roho ya Mugu (Nafsi ya 3) Yoh 19:30
-1petro 3:18 > Mwili kabla haujauwawa ulisalim Roho
“katika kizazi cha 3 Roho iliyofanya kazi ni Roho wa Kriso/Neno na kazi yake ilikuwa ni kulitambulisha Kanisa”
1Kor 2:6-16 kizazi cha 4 alikuja Roho wa Baba
-Tuna Nia ya Kristo: tukisema kanisa ni tofauti na dini/dhehebu tuna nia ya Kristo
Luk 1:17 kizazi cha 3 alizaliwa Yohana akiwa na Roho ya Eliya
“Zakaria alizaa mtoto ndani yake kulikuwa na Roho ya Eliya .Je, ni vibaya kwa Zebedayo kumzaa mtoto mwenye Roho ya Eliya?.
’katika kizazi cha 3 Roho Mtakatifu alikuja kutambulisha Kanisa. Katika kizazi cha 4 Roho Mtakatifu alikuja kujenga Kanisa. Kizazi cha MUNGU, MUNGU amekuja ambae ana-miliki Roho hizo na anatekeleza yote”
*kinachowasumbua wengi ni mbona hatuneni kwa lugha*
1Kor 14 “Atubuye ni Bora kuliko ane-nae kwa lugha. Sasa amekuja Atubuye”
Mdo 2:  walisema kwa lugha nyingine yaan wewe mchaga unaongea kisukuma na msukuma anaongea kihehe, mswahili anaongea kiingereza.
“MUNGU atakutana nao uso kwa uso  wote wanaotoa mashitaka ya uongo na kumchafua MUNGU,hawawezi kupona. Watafungwa maisha hawawezi kumchafua MUNGU namna hiyo kwamba nafugisha ndoa ya jinsia moja wakati tunakemea jambo hilo .MUNGU amechukia
“MNAMSINGIZIA MUNGU MNAFIKIRI MUNGU ATAWAACHA?” Mseme KWELI mpone!!!
"Karamu ya Sheria ya Roho wa Uzima inayoniweka HURU MBALI na sheria ya dhambi na mauti” 

Monday, 9 January 2017


*MAREJESHO YA UTAJIRI WA MADINI NDANI KANISA*

Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kusema tukae kama familia moja tukiwa na Baba, akaagiza wenye haki kupanga viti katika mduara na kiti chake, mama wakili, Mtendaji wa Wakili vikiwa vinaangaliana na viti vya wenye haki.
Nandipo mazungumzo ya kama BABA wa familia na familia yake yakaanza maana tayali kuna Agano la umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa akauliza swali kuwa ni kwa nini mvua haikunyesha jana hapa wakati baadhi ya mikoa ilinyesha?
Ni swali alilouliza kutokana na shukrani na toba iliyofanywa katika ibada ya jana kwaajili ya ukame wa kutonyesha mvua nchini.
Baadhi ya wenye haki waliopata taarifa za kunyesha kwa mvua katika mikoa mbalimbali nchini walitaja mikoa ambao mvua ilinyesha ambayo ni pamoja na mikoa ya jiji Mwanzo Malidadi (mbeya), Ufunuo wa Kristo( Iringa), Mlima wa Neema kubwa (morogoro), Hati miliki(mtwara).
Lakini swali hilo lilihitimishwa kujibiwa na Mtendaji wa Wakili wa Wakili wa MUNGU ambaye pia ni Kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana akisema ni kwa sababu mkoa huu haukutubu walipopata barua za kumchafua MUNGU walikaa nazo tu lakini kuna mkoa ambao Mkurugenzi wake alipopokea barua ya kuchafua aliichukuwa mwenyewe na kuipeleka kwa kuhani wa pale na kusema wafanye Toba kwa ajili ya hilo.
Kisha Wakili Wa MUNGU akaruhusu kama kuna yoyote mwenye kitu cha kusema kwake; “hapa tumekaa Baba na watoto wake”.
Wakili wa MUNGU aliahirisha mkao huo wa mkutano akasimama na kurudi madhabahuni na kuanza kwa kuonyesha madini yaliyotoka kwenye migodi ya wakamilifu  ambapo tangu walipopata wamepata sana madini ingawa wamefikia kuanza kuvuna madini.
“leo tunasimama tukiwa familia moja ya MUNGU wenye migodi ni lazima wapate madini na wenye biashara, viwanda ni lazima upate faida”
Awali kabla ya kusimamisha toba ya kufuta damu zisizona hatia za waliokufa wakiwa ni makafala ya uchimbaji wa madini kuanzia kipindi cha uchimbaji cha wajerumani hata leo huku wenye haki wakiwa wameizunguka madhabahu aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu.
Ambapo sadaka hiyo maalumu akaita ni sadaka ya Zab 23:1-6 kumsimamisha Mchungaji Mmoja Halisi ambae ni MUNGU Aliyetuma Wote Vizazi Vyote.
Kwa sadaka hiyo Wakili wa MUNGU alisema “kwenye bonde la uvuli wa mauti sitapita tena”
“Hakika wema na fadhiri zitanifuata mimi milele, ninakaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu” alifafanua kuhusu sadaka hiyo maalumu.
Alianza shukrani na toba hiyo kwa kumshukuru MUNGU kwa ajili ya kutoka kwenye kituo cha umbo na kuagiza “tubu kwaajili ya damu zilizokuwa zinalia zinadai haki ya wenye haki wasipate madini leo tunazitubia hizo yaani damu za waliowahi kuzikwa wakiwa hai”
“Madini sasa yamerejea Madhabahuni hayataonekana kwa wachawi milele” lisisitiza
“Toba kwa damu zinazolia katika migodi ya madini zinazosababisha wachimba madini wasipate.
Hatahivyo wakati wa kusimamisha sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU alichagua baadhi ya wakamilifu na makuhani wenye migodi ya kuchimba madini saba wakiwemo kati yao kiongozi wa Makuhani Njia za Bwana na kuhani Njia za MUNGU kushiriki kuinua kapu la sadaka hiyo maalumu mbele za MUNGU Aliyetuma wote.
Baada ya kumaliza toba na shukrani hizo alihitimisha kwakuwatakia kila wenye haki kupokea kila anachota kwa MUNGU mwenyewe biashara yake, shamba lake, duka lake na kila chanzo cha mapato Baraka za viwango vya mgodi kutema vya thamani kama madini .

Sunday, 8 January 2017


*MAWASILIANO KATI YA KANISA NA MUNGU ALIYETUMA WOTE VIZAZI VYOTE KTK MAJIRA NA SAUTI YA SABA*
Wakili wa MUNGU alianza ibada kwa kuuliza swali na kulijibu; swali hilo ni "tutawasiliana na huyu MUNGU?"
Yaani MUNGU ambaye tayali tumekuwa na umoja nae ambapo kila ninapokuwepo nae yupo.
Alisema ktk *Majira ya kwanza:-* "Ufu12:1, Ezekiel 28:15 hadi Mwa1:1.
Katka Majira hii  kerub alikuwa akiongea na MUNGU uso kwa USO. Hapakuwepo na maombi, kulikuwepo na mawasliano ya moja kwa moja.
Kila alichowaza au kutamka MUNGU kilikuwa Roho. Wote walikuwa wakimwona MUNGU ni mpole, mnyenyekevu, mpaji mweza yote n.k".      
*Majira ya pili:-*Mwa1:3 hadi kutoka 12:2 mawasiliano yalikuwa ya aina mbili; =>mawasiliano ya moja kwa moja kabla ya anguko.
=>Hapa baada ya anguko ndipo maombi yalianza. Maombi yalitokana na kuwepo kwa dhambi.            
*Majira ya tatu:-* kut 3:10 hadi 1 falme18:30 "mawasiliano yalikuwa kupitia Musa (kut 20:19 wana wa Israel walimkataa Mungu na walitaka miujiza.
Zab 103:7 Musa alitaka kumfaham MUNGU. Je wewe unampenda ufaham".  
*Majira ya 4:-* 1falme17:1, Luka2:21 kile kizazi cha pili.  "Hapo dhambi zilikuwa zikinuka. Zilisababsha umwite MUNGU na haitiki. Hapa madhabahuni ukija kuchafua Neno ua kutofanya ulichoambiwa unabomoa madhabahuni.
Mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Eliya mtishibi.          
*Majira 5:-*"ilianza Mdo10:38 hadi 28 Adari, 2011. mawasiliano yalikuwa kupitia kwa Yesu. Hata sisi tulipoanza mawasiliano yetu yalikuwa kupitia kwa Yesu.
                    
*Majra ya 6:-* imeanza ktk yoh 9:7- Mt 21:41 hadi 8 siwani, 6.  
Mawasiliano yalikuwa kupitia Damu ya Haki kweli na Hukumu zab84:14- Kugeuza maji.
=>Damu, kitabu
=>Haki Kweli Hukumu. 
Kwa sababu Nabii wa mwisho aliyoyafundisha yalikuwa  ufunguo".       
*Majra ya 7:-* imeanza 8 siwani, 6 hadi sasa.   "mambo yaliyokuwa yakizuia mawasiliano:-            
=>kulikuwepo na umbo la nyoka ndani ya kanisa. Kabla ya mlima wa BWANA yaani ufahamu alionekana kwanza nyoka.
Nyoka alikuwa akichafua usipate ufahamu kwa kuamini alikuwepo kabla ya ufahamu.
(Kinacho-sababisha kutoka ni kwa kupata ufahamu). Akavaa umbo la nyoka pale eden na kudanganya kanisa na likadanganyika, umbo la nyoka lilichafua Aden na Eden.
=>(akaelezea kuhusu maagano mengi kukumbwa na umbo la Eden, utaelezea). Kabla ya anguko jina la Hawa halikuwepo lilitokea baada ya anguko.
Pale alipoongea na nyoka Nafsi yake ilienda kwa nyoka na ya nyoka ikaja kwake, aliyechuma tunda ni nyoka na Adamu alipokula akawa nyoka.
Aliyesema wewe utaitwa Hawa ni nyoka akmwambia nyoka. Aliyesema utakuwa mama wa wote kwenye mwili ni nyoka akimwambia nyoka.
Kilichosumbua vizazi vyote ni nyoka na kusababisha anguko.
MUNGU kizazi hiki ametutenga kabisa na nyoka na milele na milele umbo la nyoka kwani nyoka ana ndimi mbili ya mema na mabaya.
MUNGU amekuja kuishi na sisi, je tutawasiliana nae vipi?
MUNGU NA KRISTO tuko nao Wakili wa Mungu ni wa nini? Swali lilojibiwa na Kuhani wa Njia ya Mataifa Fahari ya Bwana  akasema MUNGU na Kristo hawaji kwako bila Wakili wa MUNGU.
Maana Wakili wa MUNGU ni kao la MUNGU na KRISTO hivyo ni lazima awepo ili MUNGU apate kao lake kwakuwa MUNGU ni Roho na Kristo nae ni Roho.
Awali akijenga msingi wa ibada hiyo WAKILI wa MUNGU aliongiza wenye haki kutoa Sadaka Maalumu ya Hesabu 16:15-30 nyoka kutengwa, kufutwa kabisa kwa wenye haki.
Ambayo pia sadaka hiyo maalumu ina hukumu mashtaka yote kwa wenye haki.
Yaani nchi kufunua kinywa na kuwameza waovu wote kwa sadaka hii wote wamemezwa.
HUKUMU YA MILELE IMESIMAMISHWA kwa wale waliokuwa wanamshitaki Wakili.
Ukumbusho wao umefutwa wala MUNGU kumbukumbu zao milele.
Aidha pia alionesha wenye haki ktk ibada hiyo ramani ya uumbaji wote ktk wilaya ya kinondoni iliyoonyesha mahali Kanisa
la *The pool of Siloamu church* lilipo kupitia "google map"
Karibu usikilize kwa Upendo halisi katika clip zote ilikupata ufunuo kamili wa leo..............
12 TAMZI 6.
MASAHIHISHO.
1.Mwa3:20  Adamu(nyoka)alimwambia wewe utakuwa mama wa wote wenye UHAI siyo mwili.
2.HUkumu ya milele imesimamishwa Kwa waliokuwa wanawashitaki wenye Haki wote (siyo Wakili peke yake)
MUNGU AKUBARIKI.

Saturday, 7 January 2017

*MAJIRA NA NYAKATI ZA KUISHI JUU YA UMBO


Wakili wa MUNGU leo ameanza ibada kwa kutangaza kuanza Rasmi kusimamishwa kwa chujio la Haki namba tatu.

Amesema kusimamisha majira na nyakati za Umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa imetufikisha kuwa juu ya umbo. Kizazi cha 1 hadi 4 wote waliishi kwenye mwili. Kizazi cha nne Eliya Ad2 alituingiza kwenye viungo.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya kuondoa vya Mti, udongo na vile ambavyo havina heshima.

Nakusema kuwa kila ambacho sio cha heshima kwako leo ni mwisho kwa sadaka maalumu ya leo.

Sadaka hii inasimamisha vya fedha, dhahabu na mawe ya thamani vyenye heshima na utukufu 2Tim2:20-21 na 1kor 3:10-12. Vyombo vya miti, udongo vimefutwa maana havina heshima.

Kila aina ya mila na desturi tabia ya lugha ukoo kabila vilivyokuwa vinazuia wewe kutoka leo vinaungua kwa sadaka hii, hata kama umbo la mila na desturi lilizuia kichwa wako kuokoka leo yanaungulia hapa.

Mwenye nyumba halisi ametinga ndani ya nyumba yake Mt 21:41, mafarakano kwenye agano lako leo mwisho, yote uliyowahi kuona wameshindikana leo ni mwisho, yote uliyowahi kujiuliza sana ndani yako leo unapokea majibu.

Malaika wa kusachi kuondoa maumbo yote kinyume na MUNGU. Kila aliyekanyaga hapa na kila anayesikia sauti hii imtoe kila mahali alipokuwa amekwamia.

Akifafanua kuwa kila jambo lisilofaa linateketezwa hapa kwa sadaka tunayompa MUNGU.

Sheria iliyokuwa imeng'anga'ania leo tumetoka tupo juu ya umbo, ubishi ndani ya Agano la kichwa na kanisa binti na kijana leo tumeshinda.

Ikiwa ni pamoja na kutawaliwa na mabwana wengine leo mwisho, umbo la ukoo, kabila, mila na desturi leo zimefutwa milele kwa Damu ya MUNGU. Sio saa ya mishale bali ni saa ya shangwe nderemo nk.

Kizazi cha 1-3 kwasababu

🌺Kizazi cha 1 kilikuwa manung'uniko na malalamiko.

🌺Kizazi cha 2 kilikuwa na sheria ya dhambi.

🌺Kizazi cha 3 kilikuwa NENO lililovaa mwili kanisa nalo lilikuwa mwilini.

🌺Kizai cha 4 tulitolewa mwilini na kupelekwa kwenye viungo.

🌺Kizazi cha 1-4 wote tulikuwa tunakutania kwenye umbo.

*Aidha Wakili wa MUNGU amefunua mambo 12 ambayo ni halisi ndani ya wenye haki baada ya kufuta kabisa mwili, viungo na umbo*

1.) Ufunuo 22:4 tutakuwa tukimwona MUNGU uso kwa uso.
2.) Ufunuo 21:3 Yohana katka miaka 2000 iliyopita akiwa patmo aliona maskani ya MUNGU ikiwa katikati ya "watu"

3.) Ufunuo 1:8 mimi ni mwanazo na mwisho niliyekuwepo niliyepo nitakayekuja sasa amekuja na kila jicho litamuona. Na sasa amekuja kuishi na wenye haki.

Kwenye dini hatujawahi kuambiwa kuwa MUNGU amesema atakuja ila walituambia Yesu atakuja. Amekuja ili wote tufanye kazi nae, mwendeshe gari nae, muimbe wote, mcheze wote nk.

4.) Ufunuo 20:6 watakao mwamini watakuwa Makuhani wa MUNGU na Kristo wake. Amesema kinacholeta shida mikoani sasa ni kwasababu walishazoea kuamka na kwenda kuongea wanachotaka wao kumbe wasijue MUNGU alishakua.

5.) 1kor15:25-28 ni sharti amiliki yeye. Atakuwa ni Kichwa cha Kanisa.

6.) Mathayo 21:41 alisema akija ataangamiza vibaya wabaya wote imekwishatokea ila ni kwa wale tu waliokubali kuishi juu ya umbo.

7.) 1Petro3: 13-14 akija mbingu zitaungua yaani mifumo yote itaungua viumbe vya asili vitatketea. Mtapata mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki yakaa ndani yake.

8.) Isaya 65:20-25 simba kula nyasi. Ukijenga nyuba utakaa, ukilima shamba utakula wewe, hutazaa kwa taabu, hatutapata taabu maana amekuja mwenyewe aliye chanzo cha Baraka.

9.) Mathayo 16:16-19 hasa "18" sasa Kanisa linatawala malangfo ya kuzimu kwa uhalisi. Maana ni majira ya MUNGU kulijenga Kanisa ambalo malango ya kuzimu hailishindi.

10.) Yohana 4: 23-24 Yesu alisema saa ipo ambayo waabuduo watamuabudu MUNGU katika roho na kweli. Na kituo cha uhalisi tumeshafika yaani yote ambayo MUNGU aliahidi sasa ni muda wa kuyapata.

11.) Ebr 8:10-12 wote watamjua MUNGU aliye mdogo na aliye mkubwa hivyo dhambi na uovu kufutwa milele.
NB:-
*TUMEFIKA MAHALI PA UWEPO WA VITU PALE MLIMA WA MOTO HAVITAPUNGUA*

12.) Yeremia 50:20 na Ebr 8:12 uovu kufutwa ndani ya Kanisa. Utatafuta dhambi hutaiona. Tumehama kabisa kituo cha umbo tunaishi juu ya umbo.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU alisema ndani ya Kanisa bado kuna umbo la Edeni Mwa 2&3 Ambapo alisema bado kuna mwingiliano wa safu kati ya kichwa, kanisa na watoto katika familia.

Aidha Wakili amesisiiza kila familia kutenga kiti maalumu cha kukaa baba wa familia tu na kiti maalumu cha kukaa mama wa familia tu ambapo viti hivyo visikaliwe tena na yeyote mwingine kwenye familia.

Lakini pia ameshukuru kwaajili ya kila waliotii NENO la kushiriki karamu kwa umoja na kusisitiza kuendelea kila familia kushiriki karamu kwa mkono pamoja ikiwa ni Agano la umoja kwa familia nzima.

Mwa 18: amesema umoja huo ndio ambao unaitwa KUSHIRIKI pamoja na MUNGU, Kristo na Kanisa na kuongeza kuwa "nataka mataifa yote wajue kuwa kuna kizazi cha MUNGU na ijulikane kuwa tabia ya MUNGUna Kristo ndani ya Kanisa imesimama"

    

   

Thursday, 5 January 2017


      KUISHI JUU YA UMBO


WAKILI wa MUNGU leo ameanza ibada kwa kujibu maswali mawili ambayo jana aliulizwa na Wakamilifu kwa lengo la wote tupate ufahamu kwa pamoja.

Swali aliloulizwa ni “kanisa tunafuta umbo la nyoka lakini umbo la nyoka hatujawahi kuliona kanisani?”

Akajibu kwa kusema “nyoka ana ndimi mbili, maana yake ni:-
  1.) ulimi mmoja ni wa mema.
  2.) ulimi wa pili ni wa hila.

Alisema tunaposema umbo la nyoka maana yake ni hila. Kanisani kulikuwa na wenye ndimi mbili. Hivyo MUNGU amefuta wale wenye ndimi mbili kanisani.

Hao wenye hila walikuwa wanachaua wenye haki wasimfahamu Wakili ni nani kwasababu wanajua usipo mfahamu huwezi kupokea kutoka kwa MUNGU.

Waovu walikuwa wakiwavulia wenye haki uchafu wao na kusababisha wenye haki kukosa haki zao ingawa wanaomba kwa bidii. Sasa MUNGU ameweka mwisho wa hizo ndimi mbili.

Swali la pili:-
Nitajuaje kama nina umbo la nyoka ? alijibu kuwa kulikuwepo na waliouza nafsi zao kwa kujua na wengine waliibiwa bila kujua.

Wapo waliouza nafsi zao kwa kerubi wakaja kanisani wakiwa na moyo na roho hawana nafsi ili waishi lazima waibe nafsi ya wenye haki kwa kuwavulia matakataka yao hivyo ndivyo MUNGU amefuta kuibiwa.

Hatahivyo aliongoza wenye haki kutoa sadaka Maalumu ya wote kuja kujisalimisha kwa MUNGU Madhabahuni kwakuwa MUNGU ni halisi, waabuduo halisi na kanisa ni halisi.

Sadaka hiyo inarejesha wote waliondoka kwa kudanganywa ikiwa ni pamoja na kuwaleta ndugu zetu tunaotaka waje kwa MUNGU Aliyetuma wote.

Aidha Wakili wa MUNGU ametaja aina za chujio la Haki ambalo kanisa tumepitishwa na MUNGU mwenyewe hadi kufika mahali pa kizazi cha MUNGU kimefika:-

1.)Chujio la kutenga kondoo na mbuzi. Mbuzi na kondoo hao kuchujwa kupitia malaika wa MUNGU, kristo na wa Wakili wa MUNGU.

2.) Chujio la Toba ya MUNGU. Ambayo imeondoa magugu.

3.) Chujio la umoja wa Baba, Kristo na Kanisa kutusafisha kwa upya ili kuondoa umbo la nyoka.

Mt 12:32 makuhani wa MUNGU kizazi cha MUNGU ni Roho atakae mgusa anashuhulikiwa na MUNGU mwenyewe.

UMBO
Wakili wa MUNGU amesema tunapozungumzia umbo maana yake ni zile tabia tulizokuwa nazo kutoka kwenye kabila, koo, lugha, taifa nk.

Lakini MUNGU anataka wenye haki tutoke mahali pa umbo laaina yoyote na tuende kuishi juu ya umbo maana umbo linasababisha tusimwelewe MUNGU.

Mwanzoni kanisa tulikuwa tunajipatanisha au kuungana na Nabii yaani hapo Nabii alikuja kwakuwa alitumwa lakini Sasa hatuungani tena bali tunamwalika Wakili wa MUNGU ili kuja na jeshi lote la MUNGU hapo ulipo.

Amesema tumekuwa tukishindwa kuwaleta wengine kanisani kwasababu tumekuwa na umbo kama wao wakati tunatakiwa kuishi juu ya umbo.

Faida ya kuishi juu ya umbo ni pamoja na:-
#kutetewa na MUNGU na uumbaji wote.
# Mhub3:14 Najua maana yake Hakika (ufahamu)kila anachofanya Wakili ni MUNGU anafanya.
#Kila kazi aifanyayo MUNGU itadumu milele. Kuzifuta kazi hizo haiwezekani.
#Hauwezi kuiongeza kitu chochote.
#Hauwezi kupunguza kitu.
#MUNGU amefanya hivyo ili wamche yeye.

Mhubiri 3:17-22 Wakili wa MUNGU alichukia kuishi kwenye viungo na umbo kwa kuwa hakutaka  kufanana na mnyama.

Aidha amemtaka kila mwenye haki kukubali kuhama kuishi kwenye umbo kwani kuishi kwenye umbo ni maisha ya kufanana na mnyama hivyo uishi juu ya umbo.


KUSIMAMISHA SIKU 7 ZA ADENI NA EDENI ISIYO NA UMBO LA NYOKA


Wakili wa MUNGU amesema kila siku ina msingi wake na jengo lake ambapo kazi ya msingi ni kuchora ramani.

Aidha alizungumzia Eb1:14 na Eb 1:5 kuhusu utendaji wa ibadi kubwa ya malaika ambao MUNGU amewaachilia malaika wengi wasio na idadi kwaajili kumuhudumia kila mmoja.

Yaani kwajili ya somo, kukuongoza, uponyaji, kuelewa, fedha, Baraka na kila kitu kulingana na mahitaji yako 1 Petro2:9-10 sisi tuna ukuhani wa kifalme ambao tunahudumiwa kwa kila kitu.

Kuna malaika wanaonihudumia na kuhakikisha ninapata kila ninachokihitaji isaya 44:26 kwamba MUNGU anathibitisha NENO litokalo madhabahuni Isaya 45:7-8 MUNGU anathibitisha NENO ninalotamka hivyo nitamke ili kuumba siku yangu kwani nina nguvu hiyo.

1yoh4:17 kama MUNGU alivyo ndinyo tulivyo hivyo tamka vitu vizuri na halkikisha unaweka ulinzi kwa kila unachotamka kwa akukiumba kila siku.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya kusimamisha siku 7 za kufuta umbo la nyoka ndani yetu.

Uumbaji wote tunaouona upo katika Adeni na Edeni. Mlima wa BWANA inamaanisha BABA, NENO na Roho.

Adeni ina maana ya mkusanyiko wa NENO la MUNGU na Edeni ni Bustani ya BWANA.

Adeni ni marejesho ya vituo vyote vya Rohoni (mkusanyiko wa Ufahamu wa NENO ambao haujaibiwa.)

Edeni ni Bustani ya Kanisa. Edeni ni nafsi inayomjua MUNGU. Maisha yote yanapatikana ktk Adeni na Edeni.

Kanisa lilitakiwa kukaa katka Adeni na Edeni lakini walitolewa zikaa dini na madhehebu na dunia.
Biashara yako na kazi yako ikiwa ni pamoja na kila kinachotajwa kwa majina yako kinatakiwa kukaa Adeni na Edeni.

Kukaa Adeni ni kukaa na BABA na NENO na mimi nikiwa ni Roho. Kukaa Edeni ni mimi au nafsi yangu kumjua MUNGU.

MTIRIRIKO WA UUMBAJI WA MUNGU
Ufu 12:1 mwanamke
Ufu 12:3 nyoka
Ezekel 28:15 Adeni.
Mwa 1:1 mbingu na nchi
Mwa 1:3-31
Mwa 2:1-4
Mwa 2:15 Edeni
Mwa 3:1 nyoka

Kutoka MUNGU kilichofuata ni nyoka. Kabla hujakutana na MUNGU nyoka na kabla ya kumjua MUNGu ulimjua kerubi na nyoka kwanza.

Kaba ya kukutana na Wakili wa MUNGU anaezuia ni nyoka. Nyoka anakusababisha nafsi yako isimjue MUNGU kwa maana ya kukaa Edeni.

"kabla sijaja mimi hapa mnatakiwa mpige kwanza nyoka anayevuruga ufahamu usielewe wala kukumbuka na MUNGU hawezi kukupa kile usichokifahamu wala kukikumbuka" alisema Wakili wa MUNGU.

"MUNGU amekuja kuishi na sisi akiwa ni BABA hivyo usikubali shida yoyote ikufanye usiwe na furaha wala kukosa amani maana MUNGU anasovu yote hayo" amesema Wakili wa MUNGU.

"Jambo lolote usipolipiga halitoki na ulipige katika majira yake, sasa majira ya kupiga umbo la nyoka imefika piga umbo hilo ili MUNGU atamalaki katika maisha yako" aliongeza Wakili wa MUNGU.

Kulikuwa taasisi Fulani zimeweka nembo ya nyoka kwa kuwa wajua ya kuwa nyoka ni mwelevu. Ndio umbo la nyoka lilikuwa linaendelea kufanya kazi.