Showing posts with label 11 Tamuz6. Show all posts
Showing posts with label 11 Tamuz6. Show all posts

Saturday, 7 January 2017

*MAJIRA NA NYAKATI ZA KUISHI JUU YA UMBO


Wakili wa MUNGU leo ameanza ibada kwa kutangaza kuanza Rasmi kusimamishwa kwa chujio la Haki namba tatu.

Amesema kusimamisha majira na nyakati za Umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa imetufikisha kuwa juu ya umbo. Kizazi cha 1 hadi 4 wote waliishi kwenye mwili. Kizazi cha nne Eliya Ad2 alituingiza kwenye viungo.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU aliongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya kuondoa vya Mti, udongo na vile ambavyo havina heshima.

Nakusema kuwa kila ambacho sio cha heshima kwako leo ni mwisho kwa sadaka maalumu ya leo.

Sadaka hii inasimamisha vya fedha, dhahabu na mawe ya thamani vyenye heshima na utukufu 2Tim2:20-21 na 1kor 3:10-12. Vyombo vya miti, udongo vimefutwa maana havina heshima.

Kila aina ya mila na desturi tabia ya lugha ukoo kabila vilivyokuwa vinazuia wewe kutoka leo vinaungua kwa sadaka hii, hata kama umbo la mila na desturi lilizuia kichwa wako kuokoka leo yanaungulia hapa.

Mwenye nyumba halisi ametinga ndani ya nyumba yake Mt 21:41, mafarakano kwenye agano lako leo mwisho, yote uliyowahi kuona wameshindikana leo ni mwisho, yote uliyowahi kujiuliza sana ndani yako leo unapokea majibu.

Malaika wa kusachi kuondoa maumbo yote kinyume na MUNGU. Kila aliyekanyaga hapa na kila anayesikia sauti hii imtoe kila mahali alipokuwa amekwamia.

Akifafanua kuwa kila jambo lisilofaa linateketezwa hapa kwa sadaka tunayompa MUNGU.

Sheria iliyokuwa imeng'anga'ania leo tumetoka tupo juu ya umbo, ubishi ndani ya Agano la kichwa na kanisa binti na kijana leo tumeshinda.

Ikiwa ni pamoja na kutawaliwa na mabwana wengine leo mwisho, umbo la ukoo, kabila, mila na desturi leo zimefutwa milele kwa Damu ya MUNGU. Sio saa ya mishale bali ni saa ya shangwe nderemo nk.

Kizazi cha 1-3 kwasababu

🌺Kizazi cha 1 kilikuwa manung'uniko na malalamiko.

🌺Kizazi cha 2 kilikuwa na sheria ya dhambi.

🌺Kizazi cha 3 kilikuwa NENO lililovaa mwili kanisa nalo lilikuwa mwilini.

🌺Kizai cha 4 tulitolewa mwilini na kupelekwa kwenye viungo.

🌺Kizazi cha 1-4 wote tulikuwa tunakutania kwenye umbo.

*Aidha Wakili wa MUNGU amefunua mambo 12 ambayo ni halisi ndani ya wenye haki baada ya kufuta kabisa mwili, viungo na umbo*

1.) Ufunuo 22:4 tutakuwa tukimwona MUNGU uso kwa uso.
2.) Ufunuo 21:3 Yohana katka miaka 2000 iliyopita akiwa patmo aliona maskani ya MUNGU ikiwa katikati ya "watu"

3.) Ufunuo 1:8 mimi ni mwanazo na mwisho niliyekuwepo niliyepo nitakayekuja sasa amekuja na kila jicho litamuona. Na sasa amekuja kuishi na wenye haki.

Kwenye dini hatujawahi kuambiwa kuwa MUNGU amesema atakuja ila walituambia Yesu atakuja. Amekuja ili wote tufanye kazi nae, mwendeshe gari nae, muimbe wote, mcheze wote nk.

4.) Ufunuo 20:6 watakao mwamini watakuwa Makuhani wa MUNGU na Kristo wake. Amesema kinacholeta shida mikoani sasa ni kwasababu walishazoea kuamka na kwenda kuongea wanachotaka wao kumbe wasijue MUNGU alishakua.

5.) 1kor15:25-28 ni sharti amiliki yeye. Atakuwa ni Kichwa cha Kanisa.

6.) Mathayo 21:41 alisema akija ataangamiza vibaya wabaya wote imekwishatokea ila ni kwa wale tu waliokubali kuishi juu ya umbo.

7.) 1Petro3: 13-14 akija mbingu zitaungua yaani mifumo yote itaungua viumbe vya asili vitatketea. Mtapata mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki yakaa ndani yake.

8.) Isaya 65:20-25 simba kula nyasi. Ukijenga nyuba utakaa, ukilima shamba utakula wewe, hutazaa kwa taabu, hatutapata taabu maana amekuja mwenyewe aliye chanzo cha Baraka.

9.) Mathayo 16:16-19 hasa "18" sasa Kanisa linatawala malangfo ya kuzimu kwa uhalisi. Maana ni majira ya MUNGU kulijenga Kanisa ambalo malango ya kuzimu hailishindi.

10.) Yohana 4: 23-24 Yesu alisema saa ipo ambayo waabuduo watamuabudu MUNGU katika roho na kweli. Na kituo cha uhalisi tumeshafika yaani yote ambayo MUNGU aliahidi sasa ni muda wa kuyapata.

11.) Ebr 8:10-12 wote watamjua MUNGU aliye mdogo na aliye mkubwa hivyo dhambi na uovu kufutwa milele.
NB:-
*TUMEFIKA MAHALI PA UWEPO WA VITU PALE MLIMA WA MOTO HAVITAPUNGUA*

12.) Yeremia 50:20 na Ebr 8:12 uovu kufutwa ndani ya Kanisa. Utatafuta dhambi hutaiona. Tumehama kabisa kituo cha umbo tunaishi juu ya umbo.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU alisema ndani ya Kanisa bado kuna umbo la Edeni Mwa 2&3 Ambapo alisema bado kuna mwingiliano wa safu kati ya kichwa, kanisa na watoto katika familia.

Aidha Wakili amesisiiza kila familia kutenga kiti maalumu cha kukaa baba wa familia tu na kiti maalumu cha kukaa mama wa familia tu ambapo viti hivyo visikaliwe tena na yeyote mwingine kwenye familia.

Lakini pia ameshukuru kwaajili ya kila waliotii NENO la kushiriki karamu kwa umoja na kusisitiza kuendelea kila familia kushiriki karamu kwa mkono pamoja ikiwa ni Agano la umoja kwa familia nzima.

Mwa 18: amesema umoja huo ndio ambao unaitwa KUSHIRIKI pamoja na MUNGU, Kristo na Kanisa na kuongeza kuwa "nataka mataifa yote wajue kuwa kuna kizazi cha MUNGU na ijulikane kuwa tabia ya MUNGUna Kristo ndani ya Kanisa imesimama"