Tuesday, 3 January 2017


MADHABAHU YA UMOJA WA MUNGU, KRISTO NA KANISA


Wakili wa MUNGU leo amesema tumefika mahali pa kuachana na umbo la vizazi vilivyopita Mdo2:34- kwani lile umbo la mwili lilisababisha Kristo kwenda mbinguni na maadui ndio maana aliambiwa kaa pembeni kwanza mpaka maadui zake awaweke chini ya miguu.

Utawala wa amani umesimama na MUNGU amekuja ndipo adui anakimbia uso wa MUNGu kwa mimi kutolipa kisasi kwa kuwa kisasi ni cha MUNGU.

Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kujenga madhabahu ya umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa 1wafalme 13:4-6.

Kwa sadaka hii itadhihirisha wazi wale wenye wepesi wa kuonea wengine na kupiga wengine na kusema "yeyote anayetaka kukupiga kofi mkono utakatika, atakaye kunyoshea kidole mkono utabaki hivyo hivyo na atakayeomba maombi mabaya na kumsengenya mwingine mdomo utaenda upande na atakuwa bubu".

Aidha kabla ya kutoa sadaka maalumu hiyo alilivua Kanisa mwonekano wote wa zamani kwa Toba ilithibitisha MUNGU yupo juu ya nchi yaani anayekugusa akutane na MUNGU kwa kushughulikiwa saa hiyohiyo. Lazima kuhakikisha mwenye haki analindwa na jambo hili lazima litokee.

Amesema dunia ilichukua nafasi ya MUNGU kwa kuchukua namba moja ili kanisa lisifike majira ya saba tuishie majira ya sita kwa mahesabu ya saba kutoa moja kanisa likabaki na majira ya sita hadi hapo MUNGU alipolifunulia kanisa kuhusu majira ya saba na sasa tumeingia kwa uhalisi maana namba moja imepatikana.

Hatahivyo alifanya ufafanuzi wa vizazi vyote na utawala wake kuwa kizazi cha kwanza hadi cha nne kilitawaliwa na mwili,viungo na umbo.

Alisema viungo ni vya ndani, kwa nje ni mwili na umbo linaonesha tabia yako ambapo kulikuwa na ushirikiano kati ya mwili, viungo na umbo ambao sasa tunaushirikiano wa MUNGU, Kristo na Kanisa lakini ni baada ya kufuta ushirikiano wa mwili, viungo na umbo.

Amemshukuru MUNGU kwa kizazi hiki kuwa juu ya mwili, viungo na umbo ambapo sasa Kanisa kwa ushirikiano wa MUNGU, Kristo na kanisa halina mwili, viungo wala umbo ambapo sasa MUNGU yupo kila mahali mwenye haki alipo na anafanana hivyo hivyo ilimradi mwenye haki huyo anatenda kwa haki.

Aliyataja Mambo ya kushughulikia ili kufuta kabisa mwili, viungo na umbo kwa kila mwenye haki kuwa ni pamoja na:-
Moyo- kwa kuungana na moyo wa MUNGu

Kiuno- kufunua mambo mazuri.

Tumbo-lizae vitu vizuri.

Macho-yaone mazuri tu.

Kifua- tupokee haki ya MUNGU.

Damu- kuugua, magonjwa hayapo tena.

Pumzi- utamke Baraka.

Mabega- yawe ya haki, furaha na amani.

Masikio- kusikia NENO na lizae matunda.

Kitovu- kurithi kutoka kwa MUNGU.

Uti wa mgongo-tumaini lako liwe MUNGU tu

Ulimi- unene NENO tu.

Sauti- yako iungane na sauti ya saba.

Mikono-kazi zote ziwe kwa utukufu wa MUNGU.

Koromero- utoe sauti ya MUNGU tu.

Aidha Wakili wa MUNGU alihitimisha ibada hiyo kwa kufafanua umbo la kufuta katika agano la kichwa na kanisa lililokuwa likimzuia MUNGU asitamalaki katika familia ambalo akaliita Umbo la bustani ya edeni.

Alisema hilo ni la kila mmoja ndani kanisa analotakiwa kulifuta kuwa ni kwamba Adamu ingawa alipewa maelekezo yote na MUNGU kuhusu kila kitu cha kulima na kutunza bustani ya edeni lakini yeye hakutoa taarifa na maelezo yote kwa mkewe Hawa na kusababisha kukalia kiti cha aliyepewa maelekezo yote ambae ni Adamu.

Hata hivyo Wakili alisisitiza kila mmoja kutanguliza toba ya kina kuanzia bustani ya edeni kwaajili ya kichwa kutokutoa taarifa kamili kwa kanisa wake, kanisa kukalia kiti cha kichwa na kichwa kikalia kiti cha kanisa kwa lengo la kurejesha Mlima wa Bwana na mahali pa Bustani ya Edeni kwa uhalisi Ezek 28:15 na Mwa 2:15.

Na ndipo alijenga Madhabahu hiyo ya Umoja wa MUNGU, Kristo na Kanisa ambayo itasimamishwa kwa siku saba. 


KUFUNULIWA KWA KANISA AMBALO NI UMOJA NA MUNGU NA KRISTO MILELE


Kiti cha MUNGU, Meza ya MUNGU na fimbo ya MUNGU vimerejea ndani ya kanisa (Mlimani kwa MUNGU).

Akijenga msingi wa Ibada hiyo Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu inayonipa kuketi pamoja na MUNGU nikiwa namilikiwa na (Baba, Neno, Roho na Kanisa) iliyounganishwa na hakika ya NENO na Heshima ya NENO.

Neno lililozuia nisipotee lipo ktk 2 wafalme 5:20-26.

MUNGU anatuona lakini tumekuwa tukimdanganya Wakili wa MUNGU nakakwamba hatuoni kila tunapokuwa.

 Amesema dunia imetengeneza makuhani wamdanganye Wakili wa MUNGU ili alie lakini Wakili wa MUNGU halii.

MUNGU nakushukuru kwa kuwa umoja wako umeonekana ndani yangu kila mahali nitakapokuwepo.

Umbo la kizazi cha kwanza ni manung'uniko, malalamiko, vilio na kumchukiza kiongozi.

Umbo la kizazi cha pili ni kufundishwa kweli na kuikataa na kuvunja madhabahu ya MUNGU.

Umbo la kizazi cha tatu lilikuwa ni kuendelea kukataa yale yanayofunuliwa kama ilivyokuwa katka Yoh 6:30- hasa kilichosababisha kutopokea ufunuo ni tabia ya mwili.

Umbo la kizazi cha nne lilikuwa la tabia za vizazi vyote kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha tatu.

Rumi8:4-7 nia ya mwili ni mauti hata vile tulivyoingia zaidi ya viungo kwa kuwa tulikuwa na nia ya mwili ilikuwa ni lazima mauti ingetupata, lakini MUNGU anataka tuwe na Roho ya Uzima kwa kuwa nia zetu ni za Roho ambayo ni uzima.

Kuongea na kuhoji hoji sio tabia ya MUNGU. MUNGU atanionyesha mambo mengi iwapo nitakuwa na tabia ya kunyamaza kimya na kusubiri majira hivyo niache tabia ya kuona jambo na kuongea nilichoona.

Kila mwenye tabia ya kushindana na mwingine ni kwakuwa anatabia ya au kile kilichompata Hawa.

Mambo ya kufuta yanayofatana na mwenye umbo la mwili:-
Mwa 3:1-6 hiki ndicho kilichompata Hawa kutaka kukalia kiti cha MUNGU.

Mwa 5:3 tabia ya mtu ya kupanda na kushuka.

Tabia ya kujitetea ni tabia ya Adamu na ni tabia isiyofaa mbele za MUNGU kwani imesababisha wengi kujitetea na kuwa sukumia makosa wenegine.

Kujitetea ni tabia ya mwili au umbo la mwili na viungo hivyo nilazima nitoke kwenye viungo na umbo la mwili.

Tunaweza kuishi kama Wakili wa MUNGU kuto kuwa na principle za maisha ya mwili na viungo na umbo lake. Sitakiwi kuadilika badilika tabia.

Habari ya Musa Kut 32:1-6 na Hesabu 2:9-10 Musa alikuwa mwepesi wa kutubu kwaajili ya wengine lakini kwaajili yake alikuwa hawezi.

Hiki ndicho kinachompata Yule anae tubu kwaajili ya wengine lakini yeye mwenyewe hatubu inasababisha kuchoka kutenda mema.

Tubu kwa kile ulichofanya na usichofanya huo ndio utakatifu MUNGU anaoutaka. Tuwe na tabia ya toba binafsi.

Tabia ya kusanyiko la MUNGU la kizazi cha kwanza lilikuwa na manung'uniko.

"MUNGU tusamehe kwa ajili ya Kanisa la jangwani kwa kuwavusha lakini kwa muda mfupi walinung'unika.

Sisi leo kukatae tabia ya tumbo ya kutokusema asante Mt17:1-8.


UMOJA WA BABA, NENO NA KANISA

MUNGU ni Alfa na Omega ni mwanzo na mwisho, aliyepo atakayekuwepo ataendelea kuwepo Uf 1:8.

MUNGU aliruhusu NENO livae mwili. Luka 2:21 mtoto Yesu alipozaliwa aliitwa  Yesu ni NENO lililovaa mwili baadae NENO lilipakwa Mafuta ukaitwa Yesu Kristo NENO lina Moyo, Roho na Nafsi.

MUNGU kabla hajaumba chochote alikuwa na ufahamu wa NENO na alikuwa anafanya kazi peke yake. Tunda la roho ni heri tisa Mt 8:30 na Yoh1:1-5.

BABA=MUNGU –Roho, moyo, Nafsi
NENO - Moyo, Nafsi na Roho.
ROHO – ina Moyo, Nafsi, Roho.

Kitu ha kufurahisha leo ni kwamba “sisi leo tumepata Neema ya kuingia kwenye shamba”

Sasa Kanisa tumeingia ktk kituo cha uhalisi
*Kanisa
*Kristo
*MUNGU.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya kurejesha nguvu ya kutoa ikiwa ni pamoja na kutoa kupitia masirika mbalimbali ya misaada ya kimataifa.

Amefafanua kuwa dunia ndio ina mashirika ya kutoa misaada kwakuwa wenye haki hawakuwa na nguvu ya kutoa  ambapo sasa kuanzia leo mwovu hata jifiha kwenye Sadaka maana zote zimerejea kwa mpaji.

Yaani nguvu ya kutoa imerejea kwa MUNGU ambaye amempa Kanisa sasa.

Kurejea nguvu ya kutoa, maana kutoa ni:-
#Uhai
#Maisha
#Uzima
#Mafanikio
#Maongezeko
#Baraka
Nk. Vimehamia Madhabahuni.

Amesema vituo vote kanisa tumepita vikaibiwa leo kwa sadaka hii vitakuwa ni siraha ya kupiga waovu.

Yaani tuna hatua halisi ambayo ndio shamba. Leo wewe mwenye haki uliyeungana na MUNGU, Kristo na Kanisa unaAmri 1, hatma 1 halisi unatakiwa uwe na hakika zaidi.

Aidha Wakili wa MUNGU leo ametangaza mwisho wa mnyama asiyejulikana asiye na sura maalumu maana tuna uhalisi wa Isaya 62:1-3 kiti cha MUNGU hakikaliki akiwasambaratisha waliokaa popote walipokusanyana kinyume na kanisa.

Tunaungana na Jeshi la MUNGU kuondoa uchafu wote Amri 1 ya MUNGU ipo kazini kuondoa waovu wote.

Mwa 2:19 hata kama alimtuma Adamu alite yale majina aliita nayakawa ni yale yale akiwa amesimama hapohapo.

Kut 3:10 majira ya 3 MUNGU hakuwa na mahali pa kukanyaga kwasababu kila mahali palikuwa na pameharibiwa na kerubi.

Aliacha kukanyaga juu ya nchi kwasababu hakuona mahali pa kukanyaga akaona amtume Musa Kut 3:4-6.

Musa wakati anatumwa na MUNGU vitu vyote vilikuwa kwa kerubi na kerubi alikuwa ameshaathiri akili ya Musa.

Kwenye majira ya 5 wakamfuta Baba wakamuinua Yesu.

Hapawezekani kuwana kizazi pasipo kuwa na Mpakwa Mafuta, kwahiyo hata Musa alikuwa ni Kristo, mpakwa mafuta kizazi cha 1, Eliya Mtishibi alikuwa mpakwa mafuta kizazi cha 2 vitu vyote viligeuka kuwa mali ya kerubi.

MUNGU anakupaka mafuta kwa njia ya Sauti, kila kazi iliyofanywa na waliotumwa ni MUNGU alifanya.
Roho ndiye alikuwa wa Kwanza kumthibiti kerubi.

Yoh 20:1-9 alisema “Bwana wangu” sasa tambua anayeongoza kizazi siku zote huwa sio mtu. Hata kama utaona anafanana na wewe, anavaa kama wewe.

Yoh 19:30 akizungumzia kilichonyakuliwa 12 adar, 3 ni Roho ya Baba.
Amesema dunia ikiwa imekaa kuangalia macho juu kumsubili kristo mawinguni MUNGU aliwapiga chenga kristo akazliwa Kilimanjaro na sauti aliipata Kigoma akapakwa mafuta huko kwa agizo la kujenga kanisa.

Sauti ile ya MUNGU alipoipokea Eliya hakuwa tena mchaga bali NENO Kristo. MUNGU alianza na sasa anamalizia yeye mwenyewe ndio maana ni mwanzo a mwisho na alfa na omega.

Aidha akizungumziz kuhusu Eliya Ad2 na Wakili wa MUNGU amesema Zekalia 4:1-7 kuwa walikuwepo kabla ya misingi ya dunia kuwepo, kulia mwingine kushoto.

Aliongeza kuwa Eliya ndio sababu alipopata Sauti yaani majira ilipofika alienda kigoma kumtafuta miaka1000.

Hatahivyo Wakili wa MUNGU ameshirikisha wenye haki karamu ya umoja wa Baba, kristo na kanisa na kusema hakuna somo zaidi ya kushiriki pamoja kwenye sahani 1 bakuli 1kushiriki kwa mikono na ameagiza wenye haki wote kufanya hivyo.

Ambapo Wakili wa MUNGU alianza kuishirikisha familia yake ya viungo, familia ya mjumbe iliyowakirishwa na Mwaminifu, familia ya Mtendaji wa Wakili na makuhani wa NJia waliokuwepo na ndipo Kanisa zima tulishirikishwa karamu hiyo.


MAJIRA NA NYAKATI ZA HATMA HALISI KANISA LA  KWELI

Kanisa la kweli ni kusanyiko la watendao kwa haki. Yale aliyoyakusudia MUNGU tukiwa kwenye kiganja chake kuonekana kutimia kwa uhalisi sasa.

Awali akijenga msingi wa Ibada hiyo Wakili wa MUNGU aluimuhamisha kituo cha majina kiongozi wa makuhani ambapo sasa anaitwa "NJIA ZA BWANA" badala ya Njia za Bwana Ad2 MUNGU wa Majeshi" pamoja kuhani wa Kituo cha Ad2 "Kuhani YEHOSHANI".

Kinachowakamatia wengi ni kujiuliza maswali maswali kuwa Yesu ni nani? Eliya kizazi cha nne ni Nani na Miaka 1000 ni nani?

Ni MUNGU kabla ya majira ya 3 alikuwa hatumi bali alifanya mwenyewe.

MUNGU ana Nafsi 3 kwahiyo ukisema Nafsi ya MUNGU una maana ifuatayo 1 Yoh 5:8.

i)BABA ambaye ana moyo.
                               Roho
                               Nafsi

ii)NENO ambaye ana moyo.
                                Roho.
                               Nafsi.

iii)Roho ambaye ana moyo.
                                 Roho.
                                 Nafsi.                              

Huyu Baba ni MUNGU
        NENO- Kristo Mafuta.
        Roho - Kanisa

Hivyo kwa maana nyinge ukisema nafsi ya MUNGU un maana ya MUNGU kristo na Kanisa. Kwahiyo Kristo ni MUNGU na Kanisa ni MUNGU ndio sababu sio dini wala dhehebu.

Tunaenda mpaka mahali ambapomchawi, mzimu, ubya, uchafu haukubaliki ndani ya Kanisa kwasababu Kanisa ni MUNGU.

MUNGU ni mmoja
Nafsi ya 1 BABA
Nafsi ya 2 Neno - Kristo.
Nafsi ya 3 Roho - Kanisa.

Baada ya anguko hapa kwenye mlima wa MUNGU ndipo alipokuja na majira mpya mwanzo 1:3 siku zake 7.

 Akatengeneza Bustani ya Edeni. Anaposema tuumbe mtu kwa mfano wetu alikuwa na nani? Mwa 1:26 maana Nafsi yake ya 3 ambayo ni Roho tunamuona akiwa ni Mwa 1:2 kumthibiti kerubi aliyekuwa amekwisha geuka na kuwa shetani.

Mwanzoni tumemuona kuwa Baba ana nafsi ya:-
Baba - Moyo, Roho, Nafsi.
Neno - moyo, Roho, Nafsi.
Roho - moyo, roho, nafsi.

Katika Mwa1:26 alikuwa ni Roho wa Roho anaposema na tumuumbe. Baba wakati anamfukuza Ad1 pale bustani ya Edeni  katk Mwa 3:22-24.

Nguvu ya Moyo wa Roho. Roho na Nafsi ni moja. Wanaogopa Kanisa kwakuwa ni MUNGU hiyo ndio hatma halisi ya Neno.

Waliotumwa wote walikuwa ni wana. Kristo kizazi cha nne alikuwa na Roho ya Baba.

Mwa 18:3-10 Bwana akionekana kama watu watatu, ndio sababu nakuambia MUNGU anakula chips na mishikaki. Je pale kwa ibrahimu hakula?

Kumbe unaposema umezaliwa na mtu ni kosa, unaposema umefunuliwa Kanisa ni kosa kumbe MUNGU mwenyewe ndiye anayefunua Kanisa.

Baada ya kuiba nafsi hai ya Ad1 kerubi alienda kutengeneza majini. Mapepo, uchawi nk. Ndio maana Yesu ktk Mt 16:16 Nitalijenga Kanisa alikuwa na maana ya Roho.

Mt 3:15-17, 1 Petro 3:18 Roho wa kwa Neno.

Mdo 9:1-10, luka 24:50-51 aliyenyakuliwa ni Roho. Hivyo hivyo alivyoenda ndivyo atakavyorudi.

Yoh 17:4 Baba nimefanya kazi yako nirudishe kwenye utukufu wako wa kwanza kuwa NENO.

Yoh 9:7, Mt 21:40 Roho wa MUNGU ndio iliingia ndai ya Eliya akabadilika jina mpaka akakana malango ya mwanamke na mwanaume.

Aliyetufundisha kuhusu:-
*Vizazi vyote vine.
*Aliyevunja misingi mibaya.
*Aliyetuingiza kwenye majira mpya.
*Aliyesababisha tuvae vazi.
*Aliyekuja kujenga jukwaa la MUNGU kuja.
Alikuwa ni Roho wa BABA.

Kristo aliposema "Narudi kukaa kochi 1 na Baba ni Roho wa BABA. Huyo Roho alikuja na:-
#Matengenezo.
#Marejesho.
#Upatanisho.
#kujenga.
Huyo Baba ndiye mwenye hii Roho.

Kwahiyo hata huyo Roho wa Baba aliacha wenye hila na mashetani. Roho wa Baba ndiye alimwabia Miaka 1000 nimekuachia "wenye hila na mashetani usiwaogope waangamize waue wote"

Roho wa Baba hawezi kushindana na MUNGU ndio sababu Sasa tunaomba kwa Damu ya MUNGU.

Kanisa, Kristo na MUNGU ni kitu kimoja. Mimi ni Roho, Nafsi ya tatu ya MUNGU, nina Roho, moyo na Nafsi ya MUNGU.

Wakili wa MUNGU amesema kinachosumbua wengi ni kituo cha umbo la 1.

Aidha amewaonya makuhani kwa vituoni kumfafanua Wakili kama Aliyetumwa wakati yeye ni Aliyetuma kwasababu amembeba Aliyetuma ambaye anaishi kwake.

Kinachosumbua kingine kwenye maono ukimwona Wakili unasema leo nilimuona Miaka1000 kumbe ni MUNGU na Kristo. Amesema makuhani wengi wanapokwamia ni pale wanaposimama madhabahuni peke yao bila Wakili wa MUNGU wanajikuta wanafundisha vitu ambavyo ni vya level ya aliyetumwa ambavyo havimuamishi yeyote kituo.

"MUNGU hatambui kama niliwahi kuwepo majira ya 1-6, sauti ya 1-6 maana anajua hizo majira zote hazikuwahi kukupa haki ya kuishi, MUNGU anatambua kwamba majira hii ya 7 wenye haki ndio unaishi maana majira hii ndio inakupa haki ya kuishi.

Toba
Kutubu kwa MUNGU kwa roho tuliyokuwa nayo ya kulinganisha vitu na watu mwana nk.

OVYO
8 siwani,6 MUNGU amekuja kukaa nasi moja kwa moja. Tuwe tunaamkia madhabahuni. Sasa hivi MUNGU atakuwa anaua waovu wote.

Aidha Wakili wa MUNGU alihoji mwenye haki "kwani manataka kuishi au kufa?"

Hatahivyo Wakili wa MUNGU aliliongoza Kanisa kutoa Sadaka maalumu ya majira na nyakati za Hatma Halisi Kanisa la Kweli.

Ambapo pia Kiongozi wa Makuhani aliliongoza Kanisa toba ya kina ambayo ilihitimishwa kwa kutoa sadaka ya amani kati ya MUNGU na Kanisa.


THAMANI NA FAIDA YA KUACHANA NA UMBO LA KWANZA LENYE UHARIBIFU.


Wakili wa MUNGU amesema Hatma ndio kusudi la kila mmoja ambalo amemkusudia kwani majira hii Kanisa linatakiwa kuwa juu ya Umbo ambalo ulianza nalo.

Kuna jinsi MUNGU atakutoa kwenye Umbo la kwanza maana kila ulichonacho kina nafsi na mahali MUNGU alipotupeleka ni juu sana mahali alipotukusudia tangu mwanzo.

Aidha Wakili ameongoza Wenye haki kutoa Sadaka maalumu ya kutengwa na mwanzo wa umbo lenye uharibifu.

Hatahivyo  ametaja sababu za MUNGU kutupeleka juu zaidi ya viungo kuwa ni pamoja na kututenga na wale ambao wamekataa kuhama vituo na kutupeleka mahali ambapo hakuna umbo.

Maana tukiwa na umbo ni rahisi kupigwa na Yule mnyama mwenye umbo lisiloeleweka maana mahali tulipo ni juu ya viungo nilivyoanza navyo. Watoto wapo juu ya viungo vilivyoanza.

Nitaanza kupendeza zaidi. Maumivu ya kizembe zembe hutayasikia ndipo utakapo kuwa juu umehama kituo.

Hatma ya ila Mwenye haki atendaye kwa haki 1Yoh 5:8-9

Kumkamilisha MUNGU. Maana MUNGU ni MUNGU lakini bila Kristo na Kanisa hakamiliki. Ukamilifu wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa.

Umoja wa MUNGU unakamilishwa na Kanisa. Namba 1 aliyokusudiwa na MUNGU na inakamilishwa na Kanisa. Hiyo namba 1 ni Kanisa.

Kwahiyo kama ulikuwa huliombei Kanisa sasa utaliombea. hatma 1 halisi ni kumkamilisha MUNGU.

Kuhakikisha Kristo anatawala na Kanisa  juu ya nchi.

Uf 20:6. Ufu 22:4 watamuona uso kwa uso akiwa nyumbani kwako, shambani kwako nk.

Ukitembea kwa mguu
                    Kwa ndege}
                    Kwa gari  
MUNGU ataonekana hivyo hivyo.

Haya yalikuwa hayawezekani mpaka utoke kwenye umbo la 1 la uharibifu na uingie juu zaidi  pasipo kuwa na umbo lililotangulia.

Mwa 18:1 ilitokea Israel kwa Ibrahimu majira hi MUNGU anataka tuonekane kila mahali tukiwa na MUNGU na Kristo.

Math 19: 23-25 Israel ya mwilini ndio ilikuwa urthi wake. Hawataki taifa hili liitwe urithi wa MUNGU. Hawataki Hatma halisi ya Kanisa kwani utajiri halisi utaonekana ndani ya taifa kwa sababu ya nguvu ya hatma ya Kanisa.

Ukikutana na anayezuia mafanikio haya utafanyaje? utampeleka kwa MUNGU amtambue yeye mwenyewe.

Hivyo shukrani zetu zibadilike ili haya yote yatokee kwa amri moja halisi.

Watakusalimia kwa heshima. Wataona wewe ndiye chanzo cha thamani nzuri. Hazina lulu na juya.

Milionea, trionea na bilionea huwa wanajifanya ndio madini, fedha, uchumi.

Kama umekubali kuwa na zaidi ya umbo la 1 basi utaonekana kuwa thamani halisi.

*NB:-*Karamu ya leo imegeuzwa kuwa ni Sheria ya Roho wa Uzima inayonitenga kabisa na sheria ya mauti.

Somo:AMRI MOJA HALISI.

Wakili alianza kwa kymshukuru Mungu kwamba Dan 2:35-44 imetimia , Zaidi sana alisema naanza kwa kusoma Zaburi 114:1-6 Kwa amri mmoja 1.Bahari itakimbia kwetu 2.Yordan imefutwa kabisa 3.milima lazima iruke kama kondoo waume 4.Nchi lazima itetemeke 5.vilima lazima viruke 6.miamba yote imesagika na kuwa ziwa LA maji 7.Jiwe gumu kuwa chem chem KITUO HIKI ni cha AMRI MOJA HALISI Mabaya yote Leo ni mwisho mwisho MAMBO YA KUSIMAMISHA SHUKRAN:na kufuta kabisa 1.Mataifa yote yaliapa kuwa Dan 2:35-44 haiwezi kutokea Goshen 2.sadaka mbali mbali zimetokea ili isay 2 2 isitimie 3.viapo na makufuru vimetamkwa kwa Taifa na kanisa wasifanye Kazi pamoja yaani math 21: 41-43 isitimie 4.kulikuwa na hila za kila namna kuwa kanisa LA kweli halitakubalika kamwe Goshen ingawa limetokea hapo 5.saini mbali mbali za kuzuia kanisa LA kweli kupokelewa 6.uumbaji wote kusainishwa kiunajimu kuwa usikubali kanisa wala Wakili wa Mungu 7.Mashindano makuu na Mungu ndani na NNE ANza shukrani sasa . Leo umbo LA kerubi Leo limefutwa kabisa Na maumbo ya kila aina . Futa na wew hayo yote kwa shukrani

HATMA MOJA HALISI


Wakili wa MUNGU amefunua kuwa ilikupata hatma moja halisi ni lazima kutubu kwaajili ya kufuta Agano la mfanano milele na kufuta umbo la kwanza milele.

Wakili wa MUNGU amesema Leo kitabu kinaandikwa na tofauti kati ya mwenye haki na mwovu lazima ijulikane. 2.) anayemtumikia Bwana na asiyemtumikia lazima ajulikane.

3.) Sasa  mimi nimeachiliwa kuwa hazina ya MUNGU. Amesema MUNGU anataka wote tuwe na hatma moja halisi. Na iwapo tukiwa na hatma moja hakuna mwenye kumkanyaga mwingine.

Kila mmoja nyumbani kuwa na amani na furaha kwa afya nzuri itokayo Madhabahuni. Hatma moja halisi ni zaidi ya viungo. Na ukishatoka kwenye umbo la kwanza utaona ugonjwa uliokuwa unakusumbua unakukimbia.

Aidha Wakili wa MUNGU ameongoza wenye haki kutoa sadaka maalumu ya Madhabahu iliyosimamisha hatma moja halisi zaidi ya viungo.

Sadaka hiyo inakutoa kwenye hatma ya kwanza na kukupeleka hatma moja halisi. Inakutoa kwenye umbo la kwanza na kukupeleka kwenye juu ya viungo.

Hata umbo la kwanza la MUNGU, Kristo, Wakili wa MUNGU,  kizazi na Taifa tunatoka hapo na kuwekwa kwenye hatma moja halisi juu ya viungo.

Efeso 1:18  macho ya mioyo yetu yatiwe akili yapate kuona. Kushukuru kwaajili ya kuwa:-
+ Mti wa uzima.

+Na njia ile iendayo uzimani tunayo.

+Hakuna anayepita katika njia hiyo.

 Awali akijenga msingi Wakili wa MUNGU amevitaja na kufafanua vituo ambavyo Kanisa tumepita katika mwezi siwani mwaka 6.